Manyara UPDATE: Waliofariki kwa Mafuriko Wilayani Hanang wafikia 80 na Majeruhii 133
Hv nimeona taarfa kuw askar wa jwtz wanaanz ukoz kesho mean ukoz bado hakuw seriously na kwann kesho waazianze leo inaama majesh hayana utayr

Tangu lini jeshi la Tanzania likawa na utayari?. Wao wapo tayari kujazwa Zanzibar kutishia watu kipindi Cha uchaguzi. Ila kwenye majanga Kama haya huwezi waona mpaka wabembelezwe
 
Mv bukoba waokoaji walitoka afrika kusini
Tz kwenye mambo ya uokozi sifuri
Kabisa

Ova

Hata hili janga itabidi tuwaombe wamisri au Africa Kusini waje kutusaidia. Si unaona polisi baadala ya kuokota nao wamejificha kwenye paa.
 
Mambo ya Natural disaster tunachanganya na siasa, tunaharibu kabisa, majanga ya namna hii si ya kuibeza serekali kwani huweza kutokea popote pale, na huwa nje ya uwezo wa akili na sayansi zote za kibinadamu.
 
Unauliza swali la kijinga na kipumbavu Kwa kuwa hujui hata maana ya serikali na majukumu yake..!!

Upangaji wa makazi unafanywa na watu binafsi au na serikali?

Ina maana wewe hujui kuwa serikali ndiyo yenye jukumu la kuzuia watu kuweka makazi ktk maeneo hatarishi hata kabla ya maafa.?

Lakini kinachofanyika ni nini? Ni serikali kutoa vibali vya ujenzi hata katika maeneo ambayo inajua fika kuwa ni hatari Kwa maisha ya watu..!

Si hivyo tu, bali pia ni jukumu la serikali kuhakikisha inajenga miundombinu ya kuzuia mafuriko...

Lakini hebu nenda na angalia kwenye miji yetu mingi. Mambo yako hovyo hovyo sana, watu wanajijengea nyumba hovyo, hakuna mifereji ya kupitisha maji mengi...

Ukitaka kujua hatari inayokuja, nenda ktk mji wa Mwanza uone namna watu wanavyojijengea hovyo na kwenye maeneo hatarishi huku mamlaka za serikali zinazohusika na mipango miji zikiangalia tu...

Kwa hiyo, ni kweli Kwa kiasi kikubwa serikali inastahili kulaumiwa Kwa uzembe na kushindwa kuwajibika hata kutokea Kwa maafa haya..!!

Kwenye hili serikali Ina lawama kabla ya maafa na baada ya maafa. Kabla ya maafa serikali lazima ijue maeneo hatarishi hasa kipindi hiki Cha mvua na kuwaondoa raia na pia serikali imeshindwa kutumia hata chopa haraka kuokota hata wale ambao wangesalimika mapema.
 
Kwa hiyo huko ujerumani uchina na California ambako mafuriko hutokea wote ni wa HOVYO, ndio maana tunasemaga upinzani ni takataka hawana akili.

Upinzani unaingiaje hapa?. Halafu acha kulinganisha China au California na takataka ya CCM.
 
‼️Naweka kumbukumbu‼️
Machi 2023 Serikali kupitia kamati ya maafa ilipeleka msaada Malawi kufuatia maafa ya kimbunga Freddy


Msaada ulikuwa:
👉🏽Tani 1000 za unga wa mahindi (Tani 90 kutokea Dodoma na Tani 60 Iringa kuingia Malawi kila siku)
👉🏽Mablanket 6000, na mahema yasiyopungua 50
👉🏽gari la wagonjwa(Ambulance)
👉🏽karakana ya magari inayotembea(mobile workshop
👉🏽 malori makubwa ishirini yenye uzito wa tani 30
👉🏽 malori 10 yenye uzito wa tani zaidi ya kumi na nane(18)
👉🏽 Helikopta mbili
Katesh vipi mmeona hata ambulance huko?
@TZWaziriMkuu mpo?


#TutaelewanaTu lakini

Acha tu! Serikali za kinafiki Kama yetu zinaboa Sana. Nadhani ni muda Tanzania ipate Prince Johnson wa kwake, ili tuheshimiane huko mbeleni
 
Ni aibu kwa kwa mkuu wa Nchi kuendelea kula raha kwenye Hotel ya nyota tano, huku Nchini lipo janga lililowakumba Wananchi.

Dunia kote, hata Viongozi wa Mataifa yaliyoendelea Viongozi wao huguswa na janga lolote liwalo kwenye Mataifa yao. Na hata kama wapo safarini hurejea mara moja kuungana na wanao waongoza.

Ni aibu kwa Samia kuendelea kula raha Uarabuni huku kule Hanang Wananchi baadhi wameangamia kwa janga la asili.
 
Back
Top Bottom