Maoni: Ili kujenga uzalendo, Serikali ifute shule zote binafsi hapa nchini tubaki na shule za kata tu!

Hapo utakuwa umekosa uzalendo mkuu. Na ikiwa utawapeleka watoto wako Kenya basi uhamie huko huko. Hatutakutaka kurejea hapa nchini tena.

Wataenda, na wakirudi hapa nchini watapata ajira zenye mshahara mnono.
 
Tanzania ni nchi pekee inavichaa wengi waliosoma kuliko waliorogwa,niaminini mimi
 
Mkuu kutaifisha kutawafanya wananchi wote kuwa na collective responsibility katika kuhakikisha kiwango cha elimu kinapanda na kinaendelea kuwa juu.
collective responsibility itakuwa achieved lini? moja watu wakiona serikali imechukua upper hand watategea second hii move mpaka hio collective responsibility iweze kuadjust shule zile mbovu kimazingira na kiwango cha elimu duni kinachotolewa na shule hizo {ambazo ni nyingi} kiuhalisia it means elimu itakuwa rehani kwa kipindi fulani.

Sababu admistrative procedures za shule za kata zinadiffer masively na shule za private ku create even balance it means kuna wanafunzi watakaoloose .

Sioni sababu tuchukue hii difficult approach ambayo itawafanya ya wanafunzi wa loose. The better approach is not to disturb equilbrium bali serikali slowly kuboresha system iliyopo bila kuathiri wanafunzi na hii ni kwa kujenga shule zenye mazingira mazuri na kutafuta technic know how kutoka private schools ili kuimprove quality of education kwa shule za kata.
 
Habari wakuu? Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kutangaza matokeo ya mitihani ya Kidato cha Nne (CSE), nimetafakari sana na kugundua njia nzuri ya kuboresha elimu hapa nchini ni ama kufuta au kutaifisha shule zote za binafsi ili wanafunzi wote wakasome kwenye shule za umma (shule za kata).

Mfumo huu sio mgeni hapa duniani. Nchi nyingi za Ulaya, Asia na Marekani hawa-entertain uwepo wa shule binafsi kwani waligundua zinachangia sana kudhoofisha kiwango cha elimu katika nchi zao. Ndio maana Mwalimu Nyerere aliona hili tatizo mara baada ya nchi kupata uhuru akaamua kutaifisha shule za wamisionari na kuzirudisha serikalini. Sasa wakati umefika Rais Samia afuate nyayo za Nyerere ili kulikomboa taifa hili kielimu. Kuna sababu kadhaa zilizonifanya nitafakari jambo hili kwa kina:

Mosi, ikiwa shule binafsi zitataifishwa, kutakuwa hakuna mashindano ya ubora wa shule kwa kuangalia ufaulu. Kwa hiyo, suala la ku-promote shule kwa kuzichuanisha kiubora litakuwa limekufa kifo cha mende. Na serikali haitapata tena wakati mgumu kutangaza shule bora kwani shule zote zitakuwa na viwango sawa au vinavyokaribiana.

Pili, kwa kuwa hakutakuwa na sehemu mbadala ya kuwasomesha wanafunzi zaidi ya shule za kata, itawalazimu wananchi wote kuthamini shule hizi na kuhakikisha kuwa wanaziboresha kwa udi na uvumba. Kwa sasa sio watu wote wanaopenda kuona shule za kata zinakuwa bora kwani hata zikiendelea kuwa duni, wazazi wanazo shule mbadala ambako wanaweza kuwapeleka watoto wao kupata elimu bora. Wakikosa mbadala lazima tu wataboresha shule hizi ili watoto wao wapate elimu bora.

Tatu, kwa kuwa shule hizi zitakuwa zimewashikanisha watanzania wote kwa pamoja (kama ilivyokuwa kipindi cha Ujamaa na Kujitegemea), hii itasaidia kurudisha uzalendo wa kitaifa kwa wananchi ambao umeshuka kwa kiwango cha kutisha. Kwa mfano, imefika wakati sasa wazazi wenye uwezo wa kusomesha watoto wao kwenye shule binafsi hawaoni uchungu pale elimu kwenye shule za kata inaposhuka kwani wanaona hilo haliwahusu. Lakini wazazi wakishabanwa kusomesha watoto wao kwenye shule za kata (watake wasitake) lazima tu watakuwa na uchungu na maendeleo ya shule hizi.

Kwa mantiki hii, ipo haja ya serikali sikivu ya mama yetu mpendwa Rais Samia Suluhu Hassan kufuta shule zote za binafsi hapa nchini ili kila mtanzania mzalendo akamsomeshe mwanaye kwenye shule za kata. Hakuna namna nzuri ya kukuza uzalendo zaidi ya kuchukua maamuzi haya magumu. Najua wapo watakaonuna lakini hatimaye tutaelewana tu.

Nawasilisha
Ikiwa dhamira ni kutengeneza magoigoi,mbumbumbu na wahuni ndani ya taifa hili 🤔
 
No. Dhamira ni kujenga taifa lenye usawa wa kielimu na kimaendeleo kupitia kuboresha elimu ya umma kwa manufaa ya wananchi wote.
 
collective responsibility itakuwa achieved lini? moja watu wakiona serikali imechukua upper hand watategea second hii move mpaka hio collective responsibility iweze kuadjust shule zile mbovu kimazingira na kiwango cha elimu duni kinachotolewa na shule hizo {ambazo ni nyingi} kiuhalisia it means elimu itakuwa rehani kwa kipindi fulani.

Sababu admistrative procedures za shule za kata zinadiffer masively na shule za private ku create even balance it means kuna wanafunzi watakaoloose .

Sioni sababu tuchukue hii difficult approach ambayo itawafanya ya wanafunzi wa loose. The better approach is not to disturb equilbrium bali serikali slowly kuboresha system iliyopo bila kuathiri wanafunzi na hii ni kwa kujenga shule zenye mazingira mazuri na kutafuta technic know how kutoka private schools ili kuimprove quality of education kwa shule za kata.
Mkuu hata mbuyu ulianza kama mchicha. Sitakai kutakuwa na changamoto ndogo za hapa na pale lakini mwisho wa siku elimu ya umma itaimarika na kila mtu atafurahia matunda yake.
 
Kikubwa serikali iache kuendekeza umaskini na kudhoofisha elimu yetu kitu chochote kizuri kinapatikana kwa gharama. Rudisheni ada mashuleni wazazi wawajibike. Shule ni sehemu ya kukua kitaaluma na kufikia ndoto sio sehemu ya kukua ukisubiria kuolewa/kuoa.
Ada irudishwe ili elimu yetu iwe na thamani.
 
Habari wakuu? Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kutangaza matokeo ya mitihani ya Kidato cha Nne (CSE), nimetafakari sana na kugundua njia nzuri ya kuboresha elimu hapa nchini ni ama kufuta au kutaifisha shule zote za binafsi ili wanafunzi wote wakasome kwenye shule za umma (shule za kata).

Mfumo huu sio mgeni hapa duniani. Nchi nyingi za Ulaya, Asia na Marekani hawa-entertain uwepo wa shule binafsi kwani waligundua zinachangia sana kudhoofisha kiwango cha elimu katika nchi zao. Ndio maana Mwalimu Nyerere aliona hili tatizo mara baada ya nchi kupata uhuru akaamua kutaifisha shule za wamisionari na kuzirudisha serikalini. Sasa wakati umefika Rais Samia afuate nyayo za Nyerere ili kulikomboa taifa hili kielimu. Kuna sababu kadhaa zilizonifanya nitafakari jambo hili kwa kina:

Mosi, ikiwa shule binafsi zitataifishwa, kutakuwa hakuna mashindano ya ubora wa shule kwa kuangalia ufaulu. Kwa hiyo, suala la ku-promote shule kwa kuzichuanisha kiubora litakuwa limekufa kifo cha mende. Na serikali haitapata tena wakati mgumu kutangaza shule bora kwani shule zote zitakuwa na viwango sawa au vinavyokaribiana.

Pili, kwa kuwa hakutakuwa na sehemu mbadala ya kuwasomesha wanafunzi zaidi ya shule za kata, itawalazimu wananchi wote kuthamini shule hizi na kuhakikisha kuwa wanaziboresha kwa udi na uvumba. Kwa sasa sio watu wote wanaopenda kuona shule za kata zinakuwa bora kwani hata zikiendelea kuwa duni, wazazi wanazo shule mbadala ambako wanaweza kuwapeleka watoto wao kupata elimu bora. Wakikosa mbadala lazima tu wataboresha shule hizi ili watoto wao wapate elimu bora.

Tatu, kwa kuwa shule hizi zitakuwa zimewashikanisha watanzania wote kwa pamoja (kama ilivyokuwa kipindi cha Ujamaa na Kujitegemea), hii itasaidia kurudisha uzalendo wa kitaifa kwa wananchi ambao umeshuka kwa kiwango cha kutisha. Kwa mfano, imefika wakati sasa wazazi wenye uwezo wa kusomesha watoto wao kwenye shule binafsi hawaoni uchungu pale elimu kwenye shule za kata inaposhuka kwani wanaona hilo haliwahusu. Lakini wazazi wakishabanwa kusomesha watoto wao kwenye shule za kata (watake wasitake) lazima tu watakuwa na uchungu na maendeleo ya shule hizi.

Kwa mantiki hii, ipo haja ya serikali sikivu ya mama yetu mpendwa Rais Samia Suluhu Hassan kufuta shule zote za binafsi hapa nchini ili kila mtanzania mzalendo akamsomeshe mwanaye kwenye shule za kata. Hakuna namna nzuri ya kukuza uzalendo zaidi ya kuchukua maamuzi haya magumu. Najua wapo watakaonuna lakini hatimaye tutaelewana tu.

Nawasilisha
Kwa akili hizi tunayo safari ndegu mno.
 
Nadhani jitambuliahe kwanza tukuelewe
 
Back
Top Bottom