Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nahitaji kuboresha elimu kupitia uzalendo ulio bora. Huwezi kuboresha elimu ikiwa uzalendo wa raia upo chini. Na uzalendo ukiwa chini, sio rahisi kuboresha elimu. Vitu hivi wiwili vinategemeana.....ni kama kuku na yai.Unahitaji kuboresha Elimu au kuleta uzalendo?
Yani umeshindwa kubeba kilo 10 alafu unaomba uongezewe ubebe kilo 100 ???Kwa kuwa baadhi ya shule binafsi ni bora, hii itakuwa chachu kwa serikali kuboresha shule zote kwa pamoja.
Kuna haja serikali/jamii ifanye utafiti wa kina, kujua ni kwanini idadi ya raia wajinga inazidi kuongezeka badala ya kupungua.Hapo utakuwa umekosa uzalendo mkuu. Na ikiwa utawapeleka watoto wako Kenya basi uhamie huko huko. Hatutakutaka kurejea hapa nchini tena.
Nahitaji kuboresha elimu kupitia uzalendo ulio bora. Huwezi kuboresha elimu ikiwa uzalendo wa raia upo chini. Na uzalendo ukiwa chini, sio rahisi kuboresha elimu. Vitu hivi wiwili vinategemeana.....ni kama kuku na yai.
Mkuu naona bado hujanielewa. Simaanishi kufuta kama kufuta bali namaanisha kutaifisha au kuhamisha umiliki kutoka binafsi kwenda serikalini (umma). Ina maana hizi shule bado zitaendelea kutoa huduma zikiwa chini ya serikali. Na walimu wanaofundisha kwenye shule hizi pia watapewa ajira serikalini. Nadhani sasa nimeeleweka.Kwa hiyo kuboresha Elimu ndio kufuta shule Binafsi?
Kumaanisha shule Binafsi ndio Sababu kuu ya Elimu yetu kuwa hovyo?
Kuwa Serious Mkuu
Serikali ijenge za kwake.Mkuu naona bado hujanielewa. Simaanishi kufuta kama kufuta bali namaanisha kutaifisha au kuhamisha umiliki kutoka binafsi kwenda serikalini (umma). Ina maana hizi shule bado zitaendelea kutoa huduma zikiwa chini ya serikali. Na walimu wanaofundisha kwenye shule hizi pia watapewa ajira serikalini. Nadhani sasa nimeeleweka.
Teh! Bange + ugoro ni hatari kuliko cocaine na heroineHabari wakuu? Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kutangaza matokeo ya mitihani ya Kidato cha Nne (CSE), nimetafakari sana na kugundua njia nzuri ya kuboresha elimu hapa nchini ni ama kufuta au kutaifisha shule zote za binafsi ili wanafunzi wote wakasome kwenye shule za umma (shule za kata).
Mfumo huu sio mgeni hapa duniani. Nchi nyingi za Ulaya, Asia na Marekani hawa-entertain uwepo wa shule binafsi kwani waligundua zinachangia sana kudhoofisha kiwango cha elimu katika nchi zao. Ndio maana Mwalimu Nyerere aliona hili tatizo mara baada ya nchi kupata uhuru akaamua kutaifisha shule za wamisionari na kuzirudisha serikalini. Sasa wakati umefika Rais Samia afuate nyayo za Nyerere ili kulikomboa taifa hili kielimu. Kuna sababu kadhaa zilizonifanya nitafakari jambo hili kwa kina:
Mosi, ikiwa shule binafsi zitataifishwa, kutakuwa hakuna mashindano ya ubora wa shule kwa kuangalia ufaulu. Kwa hiyo, suala la ku-promote shule kwa kuzichuanisha kiubora litakuwa limekufa kifo cha mende. Na serikali haitapata tena wakati mgumu kutangaza shule bora kwani shule zote zitakuwa na viwango sawa au vinavyokaribiana.
Pili, kwa kuwa hakutakuwa na sehemu mbadala ya kuwasomesha wanafunzi zaidi ya shule za kata, itawalazimu wananchi wote kuthamini shule hizi na kuhakikisha kuwa wanaziboresha kwa udi na uvumba. Kwa sasa sio watu wote wanaopenda kuona shule za kata zinakuwa bora kwani hata zikiendelea kuwa duni, wazazi wanazo shule mbadala ambako wanaweza kuwapeleka watoto wao kupata elimu bora. Wakikosa mbadala lazima tu wataboresha shule hizi ili watoto wao wapate elimu bora.
Tatu, kwa kuwa shule hizi zitakuwa zimewashikanisha watanzania wote kwa pamoja (kama ilivyokuwa kipindi cha Ujamaa na Kujitegemea), hii itasaidia kurudisha uzalendo wa kitaifa kwa wananchi ambao umeshuka kwa kiwango cha kutisha. Kwa mfano, imefika wakati sasa wazazi wenye uwezo wa kusomesha watoto wao kwenye shule binafsi hawaoni uchungu pale elimu kwenye shule za kata inaposhuka kwani wanaona hilo haliwahusu. Lakini wazazi wakishabanwa kusomesha watoto wao kwenye shule za kata (watake wasitake) lazima tu watakuwa na uchungu na maendeleo ya shule hizi.
Kwa mantiki hii, ipo haja ya serikali sikivu ya mama yetu mpendwa Rais Samia Suluhu Hassan kufuta shule zote za binafsi hapa nchini ili kila mtanzania mzalendo akamsomeshe mwanaye kwenye shule za kata. Hakuna namna nzuri ya kukuza uzalendo zaidi ya kuchukua maamuzi haya magumu. Najua wapo watakaonuna lakini hatimaye tutaelewana tu.
Nawasilisha
Mkuu naona bado hujanielewa. Simaanishi kufuta kama kufuta bali namaanisha kutaifisha au kuhamisha umiliki kutoka binafsi kwenda serikalini (umma). Ina maana hizi shule bado zitaendelea kutoa huduma zikiwa chini ya serikali. Na walimu wanaofundisha kwenye shule hizi pia watapewa ajira serikalini. Nadhani sasa nimeeleweka.
UONGO Feza Primary Ada haifiki 10mil kwa Mwaka, hata A level haifiki hiyo ADAAkili yako ndogo sana!
Halafu mtu kama huyu akiambiwa atoe mchango wa elimu katika Shule zake hizo za kata,povu kama lote!
Uzalendo haujengwi kwa kusomea ktk Shule za kata!
Mwigulu Nchemba analala na tai ya bendera ya Taifa lakini watoto wake nadhani wote wanasoma Feza!
Analipa karibia Milioni 40 kwa mwaka kama school fees.
Unataka kuboresha shule ambazo tayari ni bora? Yani uichukue St.Francis uipeleke Serikalini ukaiboreshe?Mkuu shule hizi hazifutwi bali umiliki wake unahamishiwa serikalini ili kuziboresha zaidi.
Chukua mfano kidato cha nne,darasa darasa lina watoto 800+ mikondo pengine hadi C au D,je darasa za kutosha walimu,wakutosha,je wanaweza kuhudumiwa vipi kwa idadi hiyo,wimbo wa ujenzi,unakwamia makooni mwetu,njoo kwenye namna ya ufikaji shule kwa idadi hiyo ya wanafunzi,hadi huruma,hili linachangia pakubwa utoro mashuleni na kulea tabia mbovu za kihuni,na ufaulu hafifu,kujaribu kuudhoofisha kwa namna yeyote watoa elimu,binafsi itakuwa ni kosa kubwa,sawa na kujikimu wenyewe 🤔No. Dhamira ni kujenga taifa lenye usawa wa kielimu na kimaendeleo kupitia kuboresha elimu ya umma kwa manufaa ya wananchi wote.
Naanza kukusoma kati kati ya mistari,naona umeamua kuwachokonoa na kuwadhihaki NECTA na zile sababu zao walizotaja za kutotaka kutangaza Shule 10 bora.Nahitaji kuboresha elimu kupitia uzalendo ulio bora. Huwezi kuboresha elimu ikiwa uzalendo wa raia upo chini. Na uzalendo ukiwa chini, sio rahisi kuboresha elimu. Vitu hivi wiwili vinategemeana.....ni kama kuku na yai.