Maoni: Ili kujenga uzalendo, Serikali ifute shule zote binafsi hapa nchini tubaki na shule za kata tu!

Kama serikali imeshindwa kuboresha shule zake itawezaje kuboresha shule binafsi???
Kwa kuwa baadhi ya shule binafsi ni bora, hii itakuwa chachu kwa serikali kuboresha shule zote kwa pamoja.
 
Unahitaji kuboresha Elimu au kuleta uzalendo?
Nahitaji kuboresha elimu kupitia uzalendo ulio bora. Huwezi kuboresha elimu ikiwa uzalendo wa raia upo chini. Na uzalendo ukiwa chini, sio rahisi kuboresha elimu. Vitu hivi wiwili vinategemeana.....ni kama kuku na yai.
 
Kwa kuwa baadhi ya shule binafsi ni bora, hii itakuwa chachu kwa serikali kuboresha shule zote kwa pamoja.
Yani umeshindwa kubeba kilo 10 alafu unaomba uongezewe ubebe kilo 100 ???

Hii reasoning ni ya kiwango duni sana.
Its too low to he here.
 
Hapo utakuwa umekosa uzalendo mkuu. Na ikiwa utawapeleka watoto wako Kenya basi uhamie huko huko. Hatutakutaka kurejea hapa nchini tena.
Kuna haja serikali/jamii ifanye utafiti wa kina, kujua ni kwanini idadi ya raia wajinga inazidi kuongezeka badala ya kupungua.
 
Nahitaji kuboresha elimu kupitia uzalendo ulio bora. Huwezi kuboresha elimu ikiwa uzalendo wa raia upo chini. Na uzalendo ukiwa chini, sio rahisi kuboresha elimu. Vitu hivi wiwili vinategemeana.....ni kama kuku na yai.

Kwa hiyo kuboresha Elimu ndio kufuta shule Binafsi?
Kumaanisha shule Binafsi ndio Sababu kuu ya Elimu yetu kuwa hovyo?

Kuwa Serious Mkuu
 
Kabla kuna wazazi walikuwa wanapeleka watoto wao Kenya na Uganda. Na wengine UK.
 
Kwa hiyo kuboresha Elimu ndio kufuta shule Binafsi?
Kumaanisha shule Binafsi ndio Sababu kuu ya Elimu yetu kuwa hovyo?

Kuwa Serious Mkuu
Mkuu naona bado hujanielewa. Simaanishi kufuta kama kufuta bali namaanisha kutaifisha au kuhamisha umiliki kutoka binafsi kwenda serikalini (umma). Ina maana hizi shule bado zitaendelea kutoa huduma zikiwa chini ya serikali. Na walimu wanaofundisha kwenye shule hizi pia watapewa ajira serikalini. Nadhani sasa nimeeleweka.
 
Kabla kuna wazazi walikuwa wanapeleka watoto wao Kenya na Uganda. Na wengine UK.
Haya mambo sasa ndio hatutaki. Tunataka tubanane humu humu ndani.......hakuna kutoka nje.
 
Serikali ijenge za kwake.
 
Teh! Bange + ugoro ni hatari kuliko cocaine na heroine
 
Kweli mleta mada, shule kama st Mary's, kemebos, st Francis, uwata girls, uwata boys na zingine za namna hiyo, futilia mbali majengo tuweke Kambi za jeshi na vituo vya afya... Elimu ni huduma not a means of gain, hatuwezi kuendelea na utaratibu wa kufanya elimu kama njia ya kuwaibia watu fedha.
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Mkuu hivi unaelewa mishahara wanayolipwa waalimu wanaofundisha hizo shule au unaandika humu?

Badala uishauri serikali ijenge mazingira mazuri ya utoaji Elimu, mishahara ya waalimu, zana za kufundishia na kujifunzia, n.k.

Mwalimu analipwa milioni 2 mpaka nne wa Private unataka akafundishe shule za government wanazolipwa laki 7?
 
Serikali ianzishe English medium zake za kulipia
 
UONGO Feza Primary Ada haifiki 10mil kwa Mwaka, hata A level haifiki hiyo ADA
 
Mkuu shule hizi hazifutwi bali umiliki wake unahamishiwa serikalini ili kuziboresha zaidi.
Unataka kuboresha shule ambazo tayari ni bora? Yani uichukue St.Francis uipeleke Serikalini ukaiboreshe?
 
No. Dhamira ni kujenga taifa lenye usawa wa kielimu na kimaendeleo kupitia kuboresha elimu ya umma kwa manufaa ya wananchi wote.
Chukua mfano kidato cha nne,darasa darasa lina watoto 800+ mikondo pengine hadi C au D,je darasa za kutosha walimu,wakutosha,je wanaweza kuhudumiwa vipi kwa idadi hiyo,wimbo wa ujenzi,unakwamia makooni mwetu,njoo kwenye namna ya ufikaji shule kwa idadi hiyo ya wanafunzi,hadi huruma,hili linachangia pakubwa utoro mashuleni na kulea tabia mbovu za kihuni,na ufaulu hafifu,kujaribu kuudhoofisha kwa namna yeyote watoa elimu,binafsi itakuwa ni kosa kubwa,sawa na kujikimu wenyewe πŸ€”
 
Nahitaji kuboresha elimu kupitia uzalendo ulio bora. Huwezi kuboresha elimu ikiwa uzalendo wa raia upo chini. Na uzalendo ukiwa chini, sio rahisi kuboresha elimu. Vitu hivi wiwili vinategemeana.....ni kama kuku na yai.
Naanza kukusoma kati kati ya mistari,naona umeamua kuwachokonoa na kuwadhihaki NECTA na zile sababu zao walizotaja za kutotaka kutangaza Shule 10 bora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…