Maoni: Ili kujenga uzalendo, Serikali ifute shule zote binafsi hapa nchini tubaki na shule za kata tu!

Ulishafikiria kuwa kuna kodi ambazo serikali ya samia inazichukua toka kwenye haya mashule ili kuendeshea mambo yake.

Kama kuna point ya msingi ya kukupuuza basi ni ikifika kwenye swala la kodi.

Kumbuka shule za serikali zinatumia gharama toka serikalini tu. Hazizalishi sababu zinagharamiwa zaidi. Ila shule za private zinajiendesha kwa ada.
 
Mzee baba, umefuka moshi wa kuni mbichi..!! Unakoelekea utataka;
1. Wanaosoma nje wote warudi wakasome UDOM etc
2. Wanaoishi nje nao warudi nyumbani wakaishi kishumundu
3. Wanaotibiwa nje wasiende kutibiwa huko, bali waende Mkuranga wakakutane na yule nesi aliyemnyima mjamzito vifaa vya kujifungulia
4. Wenye magari wote wayarudishe huko nje, wote tumiliki nyumbu
5. Computer zote zirudishwe kwao Japan na kwingineko, tubaki na BLACKBOARD zetu

If you think outside the box, hutawaza huo upuuzi unaouwaza in the name of UZALENDO
 
sasa utajue ubora wako kama hauna mshindani? kama hizi mlizonazo tu zimewashinda sasa mkitaifisha na hizo za private mtaziweza?
 
Mkuu unatakiwa kuwa mzalendo hata kama unalipwa mshahara kidogo unatakiwa upige kazi kwa uhakika.
 
Serikali inabid iboreshe hizo shule na sio kufuta shule binafsi,utakuta shule binafsi walimu wa hesabu wapo 3 tena wanafunzi sio wengi,sasa nenda serikalini mwalim wa hesabu mmoja tena huyo huyo kwa form one hadi 4 afu ukute darasa1 lina wanafunzi wengi,,Yan usiposoma tuition kuchomoka ngumu!
 
sasa utajue ubora wako kama hauna mshindani? kama hizi mlizonazo tu zimewashinda sasa mkitaifisha na hizo za private mtaziweza?
Sasa utashindanaje na mtu ambaye mazingira yenu hayafanani?
 
Sasa utashindanaje na mtu ambaye mazingira yenu hayafanani?
kwan wamezuiliwa kuziboresha? ndio waboreshe na wao kuanzia mazingira ya watumishi woa, mazingira ya shule zao nk ili waendane na washindani wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…