Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Tangu mwaka 2021 Rais Samia alipoingia madarakani akiba ya fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kuridhisha kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi.

Hadi kufikia July 2025, kiwango cha akiba ya fedha za kigeni kilifikia $6.4bn sawa na TZS16.7Trilioni ikiwa ni pamoja na dhahabu tani 6.7 yenye thamani ya TZS2TRILIONI zinaifanya Reserve ya Tanzania kuwa na thamani ya TZS18.7 ~ TZS19TRILIONI.

Wakati mwaka 2020 kulikuwa na akiba ya $4.8bn pekee sawa na TZS12Trilioni.
John mrema
John baptising
John Magufuli
Faru John
Ndege John
John msakuzi
 
Lazima uwe punguani sana kuliamini hilo. Lazima wewe ni empty brain kwenye taaluma ya fedha.

Nikuulize swali dogo la kupima uelewa wako:

1. Unafahamu kuwa currencies zote zina-depreciate against true money?

2. Unajua true money ni nini?

3. Unajua hiyo shilingi trilioni 19 ni sawa na true money kiasi kiasi gani?
4.Unafahamu thamani ya dola bilioni 5 miaka 21 iliyopita ni sawa na dola bilioni ngapi kwa sasa?

Kwa wasiofahamu, dola on average ina-depreciate kwa 20% kila baada ya miaka 7. Kwa hiyo ukitaka kujua thamani ya dola bilioni 5 alizoziacha Mkapa 21 years iliyopita, unatakiwa kuiongeza pesa hiyo kwa 20% kila baada ya miaka 7. Hivyo:
Miaka 7 ya mwanzo 1. 5b×20% = 1+5= 6b
Miaka 7 iliyofuata
6b×20% = 1.2+6= 7.2b
Miaka 7 iliyofuata
7.2b×20%=1.44+7.2=8.64b

Kwa thamani ya shilingi kwa sasa:
USD8.64b = TZS23.33 trilioni.

Hivyo kama utawala wa Samia una akiba ya trillion 19, ina maana ni kiasi kidogo kuliko alichokiacha Mkapa wakati anaondoka ikulu.

NB: Nchi imejaa machawa wajinga walioamua kuweka weledi pembeni, ndiyo maana wanamdanganya Samia kuwa eti uchumi wa Tanzania upo vizuri kuliko wa Marekani, na kuna wendawazimu wanaamini. Wakati ukweli ni kuwa uchumi wa Tanzania hata ukue kwa 10%, wa Marekani ukue kwa 0.1%, bado ongezeko la uchumi wa Marekani litakuwa kubwa maradufu ya lile la Tanzania.
Ongezeko la uchumi wa Marekani la 0.1% ni sawa dola billion 300, wakati ongezeko la 10% la uchumi wa Tanzania ni dola billion 8.5. Halafu kuna wendawazimu wataona dola bilioni 8.5 ni kubwa kuliko dola bilioni 300.
 
Tangu Rais Samia aingia madarakani akiba ya fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kuridhisha kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi. Hadi kufikia July 2025, kiwango cha akiba ya fedha za kigeni kilifikia $6.4bn sawa na TZS 16.7 Trilioni pamoja na Tani 6.7 za Dhahabu sawa na $719M au TZS 1.9 Trilioni zinaifanya Akiba kufikia TZS19 Trilioni.

Wakati Mwaka 2020 kulikuwa na akiba ya $4.8bn sawa na TZS12Trilioni.

Watanzania Oktoba Tunatiki✅
 
Attachments

  • IMG-20250710-WA0049.jpg
    IMG-20250710-WA0049.jpg
    437.6 KB · Views: 21
Wakati tuko mbioni kupata Rais mpya wa sita katika awamu ya tano. Tunamsihi sana apate kutekeleza majukumu yake katika Maslahi Mapana ya taifa. Na apate kutambua pia maana ya kauli ya Maslahi Mapana ya taifa. Maana viongozi wengi huamini Maslahi ya taifa Ni katika vitu tu hususa (miundo mbinu, rasili Mali vitu, n.k) na hukomea hapo.

Kiuhalisia si hivyo, Maslahi Mapana ya taifa huanzia kuunganisha taifa lipate kuwa kitu moja bila kujali itkadi za aina yoyote si za kisiasa na si za kiimani na si kikabila wala za kijinsia. Lengo hapa ni taifa lipate kushikamana na kushirikiana bila chuki Wala ubaguzi. Utawala uliopita ndani yake ulikuwa na chuki na ubaguzi wa wazi wazi.

Pili Maslahi Mapana ya taifa ni upande wa kuindaa rasili Mali watu (wananchi), katika fikra na mawazo ya kisasa na kuwaondolea ujinga (kiufupi ni kuwekeza taasisi za elimu katika elimu ya kisasa ya kuendana na Karne ya 21). Elimu ya Sasa iliyipo nchini Ni duni, maana kwa asilimia zaidi ya 80 Ni theory oriented. Wananchi ndio taifa lenyewe, hawa wananchi hutegemea wameandaliwa na elimu ya ubora aina gani.

Kwa uchumi wetu hatuwezi kutoa elimu bure, na tukitoa elimu basi itakuwa Bora na si elimu Bora. Elimu Bora ni gharama.
Sasa Ni Bora tukawa wananchi elfu 20 wenye elimu Bora (quality education, compatible with 21 century environment) na tukawa wananchi million 60 wanaoujua kusoma na kuandika?

Tatu Maslahi Mapana ya taifa ni pamoja na Sera na Sheria wezeshi kwa wananchi wake. Mfano utawala uliopita Sera za Kodi Ni kandamizi, hazimuinui mwananchi. Tukumbuke mwananchi nae anapaswa kuendelea kiuchumi, na serikali inapaswa kuendelea kiuchumi. Sera za Kodi za Sasa so rafiki kwa mwananchi, Bali Ni rafiki kwa serikali. Kwa biashara za watanzania wengi hususa wa mtaji mdogo baada ya makato ya Kodi na Kodi ya pango hujikuta wamepata pesa ya kula, kuvaa, n.k hapati faida ya kumfanya hafungue biashara nyingine, kiufupi apigi hatua nyingine.

4: Maslahi Mapana ya taifa Ni pamoja na utawala Bora na taasisi imara. Tanzania haitaji kiongozi imara inahitaji taasisi imara za kiserikali. Maana taasisi hudumu Karne na Karne, lakini kiongozi ufa au humaliza muda wake. Ndio maana baada Magufuli alivyokufa watu wametandwa na hofu, yote Ni tokana hatuna taasisi imara, serikali ya awamu tano ilisimama si tokana na taasisi imara Bali raisi imara.

Taasisi imara husimikwa na katiba na Sheria za. Nchi, maanake ya Sasa katiba inapaswa kubadilishwa.
UMESHA ANZA KUJITOKEZA NA TAKWIMU ZENU ZA AJABU AJABU , MBONA HAMZUNGUZII DENI LA TAIFA KUPAA
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:

Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.

Pili, Mzee Magufuli amefariki, lakini spirit yake inaishi. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi, iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli amefariki lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana, usicheze nalo.

Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili, lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli inaishi. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.

Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60 kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.

Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
PIA AMEVUNJA REKODI YA DENI LA NJE KUWA KUBWA KATIKA KIPINDI CHAKE KIFUPI CHA UONGOZI
 
Mtapata taabu saana maana Mama Samia is the 'iron lady'! Ukiingia anga zake tu kuvuruga serikali iliyoyaanzisha chini ya JPM, ambayo yy naye alikuwa sehemu ya serikali hiyo lazima apite na weye!

Hamtaamini huyu mama atakavyokuwa zaidi ya Magufuli kwa kutokucheka na nyani! Mama Samia atapandisha viwango vya uongozi kiasi kwamba tutatamani aendelee kutawala kwa muda mrefu!

Nafasi ya mwanamke kuchukua madaraka makubwa inaenda kuhakikishwa kwa utendani bora wa Mama Samia! Wezi mmeula wa chuya! Hamna chenu hapa!
Mkuu umesahau kuweka Jina lako halisi na namba yako ya simu.
 
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:

Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.

Pili, Mzee Magufuli amefariki, lakini spirit yake inaishi. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi, iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli amefariki lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana, usicheze nalo.

Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili, lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli inaishi. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.

Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60 kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.

Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
REFORMS ni muhimu sana. HAKI huinua Taifa, HAKI ni Tunda la amani.
NO REFORMS, NO ELECTION.
 
.Rais Samia amejenga 81% ya ICU zote zilizopo nchini.

Wakati Rais Samia anaingia madarakani majengo ya ICU nchini Tanzania yalikuwa 14 tu, Miaka minne baadae zimefikia 73 tofauti ya ICU 59 sawa na 81%, Hii ni ishara ya Rais Samia kuwapenda na kuwajali zaidi Watanzania hii imepunguza vifo vya watu wote.

TANGU UHURU ICU 14 MIAKA MINNE ICU 59.
 
Usisahau kuongezea kuwa kateka, kapoteza, na kuua wapinzani, kazuia wakristo wa dhehebu linaloongozwa na Askofu Gwajima kufanya ibada.
 
.Rais Samia amejenga 81% ya ICU zote zilizopo nchini.

Wakati Rais Samia anaingia madarakani majengo ya ICU nchini Tanzania yalikuwa 14 tu, Miaka minne baadae zimefikia 73 tofauti ya ICU 59 sawa na 81%, Hii ni ishara ya Rais Samia kuwapenda na kuwajali zaidi Watanzania hii imepunguza vifo vya watu wote.

TANGU UHURU ICU 14 MIAKA MINNE ICU 59.
Huu ni uongo wa wazi kabisa
 
Alafu utasikia manyang’au wanasema huyu Rais Samia hajafanya kitu, ujue huyu Mama uongozi wake hauna kabisa demokrasia, mara sijui nini na nini.

Kwa ufupi tu, Mh. Rais Samia anawajibu kwa vitendo, sio maneno, kazi zake zinatoa majibu na wanafunga midomo kabisa, ila manyang’au yanajifanya hayaoni..!! Pumbaf kabisa manyang’au wote, pumbaf
 
Back
Top Bottom