Vita Ya Kwanza Ya Dunia Ndiyo Ilikuwa Chanzo Cha Kuporomoka Kwa Uchumi wa Dunia (Great Economic Depression Mwaka 1929-1939) Na Hilo Anguko La Uchumi Ndiyo Lilichangia Vita Ya Pili Ya Dunia
Sasa Mwaka 2022 Tukiwa Tumetoka Kwenye Janga la Korona Lililotikisa Uchumi, Ilikuja Kutokea Tena Vita Kati Ya Ukraine na Russia, Hii Vita Kwa Baadhi ya Watu Ilionekana Kama Haiihusu Afrika, Lakini Ni Vita Yenye Mchango Mkubwa wa Kutikisika Uchumi wa Dunia Hususani Nchi za Afrika, Na Ndiyo Maana Baada ya Vita Ile Tulishuhudia Gharama za Maisha Zikipanda, Mafuta Na Kadhalika, Na Si Tanzania Tu, Nchi Nyinginezo Nyingi, Na Ndiyo Maana Kila Nchi Mnaona Watu Wanalalamika Maisha Magumu, Mfano; Nigeria, Kenya, na Nchi Nyinginezo
Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa Kuliona Hilo, Alichangia Fedha Kwenye Sekta Ya Nishati Ili Kupunguza Gharama za Mafuta Ambazo Kwa Kiwango Alichoweza Kupunguza, Alikusudia Kushusha Gharama za Maisha Hapa Nchini...
Hakuishia Hapo… ✍️
Ameweza Kupunguza Gharama za Maisha Kupitia Sekta Ya Elimu, Kwa Kuweka Unafuu wa Upatikanaji wa Elimu, Ambapo Kuanzia Ngazi ya Awali Hadi Kidato cha Sita Wanafunzi Wanapatiwa Elimu Bure, Na Vyuoni Mbali Na Kuweka Mikopo Vyuo Vya Kati na Vya Juu, Lakini Pia, Amefadhili Wanafunzi wa Vyuoni wa Masomo Ya Sayansi Kuweza Kupata Elimu Bure Kupitia Ufadhili wa Samia Scholarship Ambao Ni Ufadhili wa 100% Kwa Wanafunzi Waliokidhi Vigezo Vya Kuupata, Ambapo Kipindi Chote Wanachokuwa Masomoni Hadi Wanamaliza Hawachangii Fedha Yoyote
Ameweza Kupunguza Gharama za Maisha Kupitia Uwepo wa Mianya ya Ajira, Ambayo Imepunguza Wimbi La Vijana Wasio Na Ajira, Na Kuchochea Upatikanaji wa Nafasi za Ajira, Kwani Pia, Amepunguza Tegemezi na Kuzalisha Wategemewa. Lakini Mfano Kupitia Mradi wa BBT (Building Better Tomorrow) Leo Hii Tuna Vijana Wanaoshiriki Kilimo Na Wananufaika, Na Vijana Hao Ni Miongoni Mwa Wale Ambao Hapo Awali Hawakuwa Na Ajira, Lakini Leo Ni Wachochezi wa Ongezeko la Mazao (Vyakula) Nchini, Na Kuongeza Mauzo Ya Mazao/Vyakula Nje Ya Nchi (Exporters)
Niseme Tu. Hii Ni Moja Kati Ya Sababu Nyingi Ambazo Tunazo za Kumpigia Kura Dkt. @Samia_Suluhu_Hassan ✅