Mama Samia,
1. Unajua kuwa una maadui wa ile timu aliyoiacha "mwenzio"?
2. Unajua hao ndugu wa mwezio hawajaridhika Bado wewe kuwepo hapo?
3. Unajua kuwa kuna hujuma dhidi yako? Unahujumiwa nawe umejisahau.
Sasa mama umepigwa hujuma nzito, huku mtaani haunogi, wasikupambe hao wanaokubebea miavuli, wanakudanganya kulinda ugali wao. Watu wana chuki na wewe.
Fanya hivi.
(a) Mtoe FREEMAN MBOWE gerezani kupitia DPP, hapo umehujumiwa na hujashtuka(umepigwa kanyanga na wazandiki, mmoja huyo mvaa gwanda la policcm).
Ukitaka uupige mwingi, Mtoe mwenyekiti wa chama Chao hao CHADEMA na weka maridhiano nao, naapa utakuwa umeupiga mwingi.
(b) Kuna wajinga wanakuhujumu kwenye upandaji wa bidhaa, kaa chini, utafakari, una vyanzo vingi vya kupata taarifa, ila kwa hapa umepigwa.
Kidumu chama chenu Cha Mapinduzi!!!!!!!!