Mapacha waliokiri kufanyiana mtihani chuo matatani, Chuo cha Ardhi wasema wanachunguza suala hilo

Mapacha waliokiri kufanyiana mtihani chuo matatani, Chuo cha Ardhi wasema wanachunguza suala hilo

Na kwanza walienda kuhojiwa kwa sababu ama dhumuni gani??Kwa sababu ni mapacha au ni nini kilikua kinaendelea??
Ni vizuri watu kabla ya kuenda maeneo kama hayo wajitafakari.....waweke hisia pembeni na wajiandae wanaenda kuongea nini??
 
Mkuu chuo kina wanafunzi 10k, kila mwaka wanafanya UE mara 2.. wana storage gani ya kutunza hizo karatasi za miaka yote hii. Hapo kuna mafile ya wanafunzi na ya staff ya chuo..
Sidhani kama ni possible kutunza vyote hivyo
Chuo gani kina wanafunzi 10k?
ARU 2020 kama walikuwa wengi basi 4k
 
Hapo hawawezi kukutwa na hatia ,ngumu sana kuwanasa hata miandiko ikitofautiana ,hapo ni kusema tu tulikuwa tunanogesha kipindi tu ili kualert watu wawe makini kwa mapacha kwamba kuna uwezekanao wa kufanyiana mitihani na si kwamba tulifanyiana.

Tatizo la wanawake/wanasiasa hawajui kitu gani cha kusema na kipi kutokisema wao wanaropoka tu baadae ikiback fire ndiyo wanagundua wamekosea.

Tujifunze kwamba kuna vitu si vya kusema hata kama unatania au una hasira kiasi gani.(Kwa wanawake na wanasiasa ili hawaliwezi).
 
Hii ni ishu ya kitaaluma uamuzi wa Chuo unaweza ukachafua Ama kuathiri chuo na sio hao graduate peke yake..

So chuo sio wajinga kutoa barua mapema hivyo..
Na hata uamuzi wa chuo wowote utaathiri baraza la kitaaluma na hata Baraza la senate la chuo hicho so lazma jibu lije baada ya kukaa na walengwa ili kutokuchafua taswira ya Chuo
Vyuo vyetu kama UDSM vingekuwa na nia ya kulinda heshima yao wangeanza kwa kuiweka tu maktaba ile thesis ya the late mheshimiwa na ya yule aliyedaiwa kuwa the late alinakiri kutoka kwake. That could be a good start.
 
Na vingepunguza PhD za Honorary maana ndo zinazowashusha hadhi wala Sio Supplimentary ya Wadada wa watu
 
Hivi unakiri vipi kwenye kweye TV inayotazamwa na watu wengi hivyo jambo linaloweza kukuingiza matatani? Haya sasa mambo yameharibika!

Chuo Kikuu Ardhi kimepata taarifa kupitia Wasafi FM, chaneli ya YouTube ya mahojiano kati ya waandishi wa habari na mapacha wawili wanaofanana. Mahojiano hayo yalirushwa siku ya Jumatano, tarehe 6 Machi, 2024 kwenye kipindi cha Jana na Leo.

Kwenye mahojiano hayo, mapacha hao walisikika kupitia chombo hicho cha habari kuwa walisoma “Chuo cha Ardhi” na kufanya mtihani wa Hydrolojia. Katika mtihani huo, mmoja wa mapacha hao alikiri kumfanyia pacha mwenzake mtihani wa marudio (supplementary) kwa kutumia kitambulisho cha pacha mwingine.

Chuo Kikuu Ardhi tunchunguza ukweli wa taarifa hizo na baada ya uchunguzi kukamilika, umma utajulishwa matokeo ya uchunguzi huo

Imetolewa na:
Prof. Evaristo Liwa
Makamu Mkuu – Chuo Kikuu Ardhi
7 Machi, 2024

View attachment 2927199

Pia soma: Chuo cha Ardhi kinapaswa kuchukua hatua dhidi ya mabinti mapacha waliokiri kufanyiana mitihani
Tunakwenda soma shule,vyuo ili kufuta ujinga na siyo kuja ajiriwa ndiyo msingi wa elimu kufuta ujinga. Ndiyo maana aliyesoma akifanya jambo la ajabu utasikia unakuwa kama hujasoma tofauti na ambaye hajaenda shule yeye akifanya maendeleo atasifiwa kuwa pamoja na hujaenda shule hongera umejitahidi.

Sasa hawa watoto chuoni walienda fanya nini? maana sikutegemea kabisa walichosema hapa. Msomi kweli unaweza kuja ongea ujinga huu tena kwenye media? Kila mtu ameshwahi chuo kufanya vituko lakini huwezi sikia mtu akiongea kwenye media ujinga kama huu wa hali ya juu. Kuna issue za kuongelea. Nilitegemea na usomi wao chuo cha ardhi labda wangekuja na issue za namna ya kuwa na mipango miji n.k. Sijui wazazi wao huko wapo katika hali gani. Kudanganya na unakiri umeidanganya JWT .Sasa kama kuna mchumba hapo ajipange maana nachelea kusema anaweza pigwa tukio na yeye au kashapigwa tayari
 
Wala hakuna kesi hapo, na chuo hakitakiwi kuthibitisha jambo lolote, wahusika wameshakiri wenyewe, kinachofuatia hapo ni kuwafutia hayo matokeo yao.

Ujinga unaenda kuwaharibia future hao watoto, kama matokeo yakifutwa maana yake hata vyeti walivyopewa kwa kufaulu masomo havitakuwa valid tena, na kwasababu hiyo, hata kazini kama walipata kazi kwa qualification zao, wataenda kupoteza ajira zao/yao.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Sio rahisi kiasi hicho, maneno tu ya mtu tena kwenye vyombo vya habari haiwezi kuwatia hatiani. Chombo chenyewe cha mzahamzaha.
 
Kuna kuunganisha dots, kama kweli mmoja alipata supplementary kwenye mtihani tajwa na alipifanya akafaulu, huu nao ni ushahidi tosha dhidi ya kesi yao.
Mbona wengi wanafaulu sup. Labda waanngalie miandiko na kuigananisha kama hiyo mitihani bado imehifadhiwa. Ila sio rahisi linaweza likapita kama mengine. Huujui nji hii wewe.
 
Ni ngumu sana,kwani mwandiko mtu si anaweza badili .Any kisheria ni haiwezekani kudhibitisha,labda kama msimamizi siku ya mtihani angeshtuka na kumkamata huyo Kulwa/Dotto. Otherwise hakuna case.
Wako wataalamu wa muandiko. Watapitia maandishi yako na kuoanisha na yanayotajwa kuwa yako. Hapa huwezi dangaya hata kidogo. Bahati mbaya muandiko hata uigize namna gani ni ngumu kubadilisha everything.
 
Hivi unakiri vipi kwenye kweye TV inayotazamwa na watu wengi hivyo jambo linaloweza kukuingiza matatani? Haya sasa mambo yameharibika!

Chuo Kikuu Ardhi kimepata taarifa kupitia Wasafi FM, chaneli ya YouTube ya mahojiano kati ya waandishi wa habari na mapacha wawili wanaofanana. Mahojiano hayo yalirushwa siku ya Jumatano, tarehe 6 Machi, 2024 kwenye kipindi cha Jana na Leo.

Kwenye mahojiano hayo, mapacha hao walisikika kupitia chombo hicho cha habari kuwa walisoma “Chuo cha Ardhi” na kufanya mtihani wa Hydrolojia. Katika mtihani huo, mmoja wa mapacha hao alikiri kumfanyia pacha mwenzake mtihani wa marudio (supplementary) kwa kutumia kitambulisho cha pacha mwingine.

Chuo Kikuu Ardhi tunchunguza ukweli wa taarifa hizo na baada ya uchunguzi kukamilika, umma utajulishwa matokeo ya uchunguzi huo

Imetolewa na:
Prof. Evaristo Liwa
Makamu Mkuu – Chuo Kikuu Ardhi
7 Machi, 2024

View attachment 2927199

Pia soma: Chuo cha Ardhi kinapaswa kuchukua hatua dhidi ya mabinti mapacha waliokiri kufanyiana mitihani
Furaha ya kushabikiwa kwa muda mfupi kwenye runinga itawaharibia reputation maisha yao yote
 
Tukiambiwa tatizo la afya ya akili linaongezeka kwa kasi tunakuwa wakali, sasa mambo ndiyo hayo, mtu anaiba anamkwepa mtu mmoja halafu anakwenda kujichongea kwa public

Hii inanikumbusha kijana mmoja huko Iringa aliua mtu akatorokea mji mwingine, kufika kule akaenda kutubu kanisani halafu akajiunga na kwaya, siku moja ile kwaya ikiwa ibadani Jumapili ikarekodiwa na ITV ikarushwa hewani, kwakuwa aliona kuonekana kwenye TV ni umaarufu akawapigia simu jamaa zake kuwa watazame kipindi cha dini ITV mchana kuna kitu amazing wataona asijue kuwa anajichongea, ndipo habari zikasambaa na polisi nao wakapita humohumo wakaenda kumdaka kama kuku
 
Inaesemekanaga wanawake hawana siri.mfano ni kama huo.Japo kuna wanaume pia wako hivyo.Sasa hapo walikua wanaona wanaongea vya maana kumbe ujinga.wakitoka hapo wanataka kua viongozi kisa ni wanawake.
 
Back
Top Bottom