Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

Pengine jina lake ndio limemponza lkn kiukweli ukiongelea mapinduzi ya Zanzibar huwezi kumuweka pembeni J.O.......hata hivyo nadhani jamaa hawajaamua kusema kama wana baba wa Taifa la Zanzibar.
 
Bramo na Waberoya
===>Wazanzibari wana hulka ya ubinafsi na ubaguzi,nenda tandika,magomeni,kariakoo na tanga maeneo ya chumbageni (Mtupie) utaona jinsi life style ilivyo,uchoyo,ubinafsi kujitenga tenga ndio chachu ya mfumo wao wa maisha
===>Siwalaumu maana nafikiri ni urithi walioachiwa na baba au babu zao,hata zanzibar wako hivi hivi wenyewe wenyewe tu,
===>Namshukuru Mungu Tanganyika yangu hiyooo inakuja tutachora mstari muda si mrefu na heshima itarudi mahali pake.
Mkuu acha CHUKI hizo ni Hasira zako binfasiiiii!! yaonyesha Chuki zisizo na msingi !! Baseless hatutishiki yametukuta kulikoni.... Ardhi ya Mungu ina wasaa !!
 
Cheche Mtungi


Hawa Jamaa ni wabinafsi na wana Roho Mbaya sana aisee.
Kwa kweli, huu labda ni urithi kutoka kwa Babu zao
Jamenii mbona mnapayuka baseless remarks ? Wewe ndiyo mbinafsi hivo unaona wenzio kwa jicho lako !! Kawaida mwizi huona watu wote ni wezi!!!!!!!!! Tungelikuwa wabaya mgeweza ishii pamoja kama waTanzania (tumeunganisha makabila yenu yote, tumewafundisha kuzungumuza lugha moja, Tumewaridhishia utamaduni mmoja)) Oh God forgive my countrymen.AMIN
 
Siku Field Marshal John Okello alipotimuliwa Zanzibar
YAFUATAYO ni masimulizi mafupi ya kipindi kifupi cha Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari, 1964 yaliyoipindua serikali ya ubia ya chama cha Zanzibar Nationalist (maarufu Hizbu) na kile cha Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP).

Tunaangazia nini hasa kilitokea usiku wa Jumamosi Januari 11, yaliyojiri siku ya pili yake na mwezi mzima wa Januari, mwaka 1964.

Tumeyakusanya masimulizi haya baada ya kuzungumza na walioshiriki katika Mapinduzi hayo ambao baadaye walisaidia kudhibiti madaraka na kuunda taasisi zilizoziba pengo la Serikali iliyopinduliwa ya Waziri Mkuu, Muhammed Shamte Hamadi.

Usiku wa manane wa Januari 11, makada wapatao 200 wa Umoja wa Vijana wa Afro-Shirazi (Afro-Shirazi Youth League) walielekea kwenye kambi ya polisi ya Ziwani, nje kidogo ya mji huko Unguja.
Wakiongozwa na Yusuf Himid wapinduzi hao hawakukabiliwa na upinzani walipofika Ziwani ila waliikuta ghala ya silaha iko wazi na wakazinyakua silaha na kukimbia nazo hadi kwenye uwanja ulio nje ya jengo la Raha Leo.

Hapo ndipo palipokuwa makao makuu ya Mapinduzi kwa siku chache na ndipo wapinduzi walikokuwa wakipewa silaha. Studio za redio ya Serikali pia zilikuwa hapo.

Moja ya sababu zilizoyafanya Mapinduzi yafanikiwe haraka ni uamuzi wa viongozi wa Serikali iliyopinduliwa Sheikh Muhammed Shamte na Sheikh Ali Muhsin Barwani kuwataka wafuasi wao wasitumie nguvu kuyapinga.

Hivyo, mbali na mapigano yaliyozuka saa za asubuhi ya Jumapili Januari 12, mbele ya Steshini ya Polisi Malindi, hapajazuka mapigano Unguja kati ya waliopindua na waliopinduliwa. Pemba nako pia hakukuwa na upinzani ijapokuwa kisiwa hicho kilikuwa ngome ya vyama vya ZNP na ZPPP.

Wengi wa wapiganaji waliokuwa kwenye Stesheni ya Polisi ya Malindi walikuwa wakuu wa polisi Wakiingereza. Wakipigana na makada wa Umma Party ambao ndio pia waliouteka uwanja wa ndege, bandari pamoja na kituo cha mawasiliano ya nje cha Cable & Wireless, kilichokuwa kwenye jengo ambalo sasa ni Hoteli ya Serena Mji Mkongwe.

Kwa hakika, kinyume cha baadhi ya watu walivyoandika hapakutokea mauaji ya kimbari. Aliyeanzisha uvumi huo alikuwa John Okello aliyeandika kwenye kitabu chake kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar kwamba watu zaidi ya elfu kumi waliuliwa. Okello aliongeza kwamba aliamrishwa na Yesu Kristo kuwakomboa Waafrika wa Zanzibar kutoka kwa wageni.

Tutamrejelea Okello na wengine waliokuwa Raha Leo baadaye. Kwanza tukumbushe kwamba mkesha wa Januari 12, mwaka 1964, Zanzibar haikuwa na jeshi. Kulikuwa polisi waliokuwa wakiongozwa na Waingereza. Wengi wa askari polisi walikuwa raia wa Tanganyika. Serikali iliyopinduliwa ilikataa kuandikiana mkataba wa kijeshi na Uingereza kwa sababu ikihisi mkataba kama huo utaonekana kuwa wa kikoloni.

Hatuwezi kusema ni nani hasa aliyepiga risasi ya mwanzo au ya mwisho katika Mapinduzi. Naitoshe tusemapo kwamba kwa vile hakukuwa na upinzani, Serikali iliyokuwa madarakani iliporomoka kama nyumba ya karata.

Tuwarejelee sasa waliokuwa Raha Leo, makao makuu ya Mapinduzi kwa siku chache. Kwanza tumuangalie Okello ambaye sauti yake ndiyo iliyokuwa ikivuma kwenye Redio Zanzibar.
Hatuna uhakika nani alimpeleka Okello Raha Leo. Wengine wanasema ni Yusuf Himidi. Wengine wanasema ni Seif Bakari aliyetoa rai atumiwe kutoa matangazo kwenye redio kwa vile sauti yake ilikuwa na lafudhi ngeni ya kutisha.
Uhakika tulio nao ni kwamba Okello alipotokea Raha Leo na mabastola yake, Aboud Jumbe alishtuka na akauliza: Nani huyu? Katokea wapi?

Kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 27 hakujulikana kabla ya Mapinduzi. Alikuwa mtu asiyejua kuandika wala kusoma na akili zake zikimtosha mwenyewe. Hakuwa na sifa za uongozi na wala hakushiriki katika vuguvugu lolote la kisiasa.

Akijibandika cheo cha kijeshi cha Field Marshall ni yeye aliyetangaza kwamba serikali ya ZNP/ZPPP imepinduliwa.
Kwa hakika, kazi hiyo ya kutangaza kufanikiwa kwa Mapinduzi kwanza alipewa Ramadhan Haji, mmoja wa wapinduzi. Lakini alikataa. Jina la Okello lisingelisikika lau Ramadhan Haji angekubali kutangaza kwamba Serikali imepinduliwa na kwamba wapinduzi waliidhibiti nchi.

Waliokuwa wakiongoza mambo Raha Leo tangu Mapinduzi yaanze, hadi Jumatatu Januari 13, walikuwa Aboud Jumbe, mmoja wa viongozi wa chama cha Afro-Shirazi (ASP), Thabit Kombo (Katibu Mkuu wa ASP) na Badawi Qullatein wa Umma Party. Muda wote huo, Sheikh Abeid Amani Karume (kiongozi wa ASP), Abdulrahman Babu (mwenyekiti wa Umma Party) na Abdalla Kassim Hanga (ASP) walikuwa Dar es Salaam.
Mnamo siku hizo hizo liliundwa Baraza la Mapinduzi na Baraza la Mawaziri lililokuwa na mamlaka kamili ya kuiendesha Zanzibar.

Mabaraza hayo mawili yalikuwa taasisi kuu za Serikali ya kimapinduzi ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Na sio ile iitwayo Kamati ya Watu Kumi na Nne ambayo baadhi ya watu wanasema kuwa ndiyo iliyoandaa Mapinduzi.

Okello akipenda kujigamba kwamba ndiye aliyeyapanga na kuyaongoza Mapinduzi. Alikuwa akitoa matamshi ya kushtusha na ya ajabu-ajabu kwenye Redio Zanzibar. Kwa mfano, siku moja alidai kwamba alipwe mshahara mkubwa zaidi ya aliokuwa akilipwa Rais Karume. Siku nyingine akasema kwamba kasri zote alizokuwa akitumia sultani kupumzikia apewe yeye.

Kuna siku aliyotoa hukumu kwamba mzee mmoja wa zaidi ya miaka 60 afungwe kwa miaka 99. Alisema kama huyo bwana atakufa gerezani basi mwanawe afungwe ili kuendeleza kifungo na mwanawe akifa basi mjukuu wake afungwe mpaka itimie miaka 99.

Nyakati nyingine aliwaonya watu wazitie moto familia zao na wao wenyewe mpaka wafe kabla ya majeshi yangu kuja. Alikuwa akitoa vitisho visivyowahi kamwe kusikika Zanzibar.
Kuna siku alitangaza kwamba wakazi wa eneo moja ambako alikuwa apite, wajipange foleni barabarani wakiwa wamevaa chupi tu.
Okello alikuwa ni adha, kitisho, kichekesho na fedheha kwa Zanzibar. Viongozi wapya wa nchi walichoka naye na wakaamua kumchukulia hatua. Salim Rashid, mmoja wa viongozi wa Umma Party aliyekuwa katibu wa Baraza la Mapinduzi anasema kwamba, kwanza alilizungumza suala la Okello na Sheikh Karume. Halafu akalizungumza na Brigadia Yusuf Himid na mwisho yeye, Yusuf Himid na Kanali Ali Mahfoudh wakalitafutia dawa.

Ilisadifu kuwa siku moja Okello alisafiri kwenda Dar es Salaam akifuatana na Jaha Ubwa, aliyekuwa katibu wake. Walipokuwa wanatarajiwa kurudi Zanzibar, Karume, Yusuf Himid, Salim Rashid na Ali Mahfoudh walikwenda uwanja wa ndege kumsubiri.

Siku hiyo anaikumbuka vizuri Luteni Hashil Seif aliyekuwa ofisa wa zamu kwenye kambi ya jeshi huko Migombani karibu na uwanja wa ndege. Alipigiwa simu akitakiwa aende kwa haraka uwanja wa ndege. Hakuambiwa anaitiwa nini.
Alipofika ndipo alipoambiwa kwamba kuna ndege ya Shirika la Ndege la Afrika ya Mashariki iliyokuwa inakuja kutoka Dar es Salaam ndani yake wakiwemo pia Okello na Jaha Ubwa. Akaelezwa kwamba awaruhusu abiria wote pamoja na Ubwa washuke, lakini amzuie Okello asishuke. Halafu amwambie rubani ampeleke Okello Kenya.

Hashil naye akampigia simu komredi mwenzake Luteni Amour Dugheshina kumwita aende uwanja wa ndege amsaidie. Maluteni wote wawili walikuwa na bunduki za aina ya machine gun.
Ndege ilipotua walipanda ndani ya ndege, wakampokonya silaha Okello na kutekeleza amri waliopewa. Rubani wa ndege alikasirika sana. Uso wake ulighadhibika, utafikiri mnyama aliyekosewa risasi, alieleza Hashil.
Lakini rubani hakuwa na la kufanya ila kuiwasha ndege na kuelekea Kenya.
Huku nyuma Salim Rashid akampigia simu Oginga Odinga, Makamu wa Rais wa Kenya, kumuarifu kwamba wamemfukuza Okello na wanamrejesha Kenya. Alifanya hivyo kwa makosa kwa sababu kutokana na jina lake akifikiri kuwa Okello ni Mjaluo kutoka Kenya.

Kumbe alikuwa mtu wa kabila la Acholi aliyezaliwa Uganda na alikwenda Unguja kabla ya kuhamia Pemba ambako alikuwa mwashi, mtiaji rangi nyumba na mpasuaji mawe.
Swali la kujiuliza hapa ni; je, iwapo kweli Okello alikuwa kiongozi mpendwa wa Mapinduzi ilikuwaje wafuasi wake na wanamapinduzi wenzake wasimtetee alipoadhiriwa uwanja wa ndege na kufukuzwa nchini? Ilikuwaje akafukuzwa kwa urahisi hivyo?

Kuna uzushi mwingi kuhusu kipindi hiki kifupi cha historia ya Zanzibar. Kwa mfano, kuna filamu ya kubuni ya Wataliana inayoonyesha maiti chungu nzima za watu waliopigwa risasi. Filamu hiyo ilikuwa na lengo moja tu; kuonyesha ukatili na unyama wa Waafrika.
Hakuna ithibati yoyote kwamba watu waliouawa katika siku za mwanzo za Mapinduzi walifika elfu kumi. Ukweli ni kwamba jumla ya watu waliouawa siku hizo haipindukii 200, katika sehemu za mjini hawazidi 25.
Uzushi mwingine ni kwamba walipelekwa Watanganyika, Zanzibar wakiwa na silaha kwenda kupindua. Na si kweli kwamba Mapinduzi yalikuwa na msisitizo wa kikabila. Katika kipindi cha mwanzo cha Mapinduzi msisitizo ulikuwa wa kitabaka. Nyimbo zilizokuwa zikiimbwa kwenye Redio Zanzibar zikiwazungumzia wakwezi na wakulima na wafanyakazi kwa jumla na si makabila.

Mapinduzi ya Zanzibar yalianzisha taasisi mpya za utawala zikiwa pamoja na Baraza la Mapinduzi, Baraza la Mawaziri na ofisi ya Rais. Taasisi hizo zilikuwa zifanye kazi kwa muda wa mwaka mmoja tu kwa vile ilikwishaamuliwa kwamba Januari 1965 pafanywe uchaguzi wa kulichagua Bunge la Katiba, lililokuwa litunge Katiba ya kudumu ya Zanzibar.
Baraza la Mapinduzi la Zanzibar pamoja na Serikali mpya zilianza kwa ubia baina ya chama cha ASP na Umma Party.

Ingawa wanachama wa ASP ndio waliofanya Mapinduzi waliutambua mchango wa wafuasi wa Umma Party na hasa mchango wa makada wao waliopata mafunzo ya kijeshi nchini Cuba.
Vijana hao wa Umma walizitia wasiwasi serikali za Marekani na Uingereza na kuzifanya ziamini kuwa utawala mpya wa Zanzibar ulikuwa wa kikomunisti. Dhana hiyo ndiyo iliyosababisha kuchukuliwa hatua ya kuyachimba na kuyagandamiza Mapinduzi ya Zanzibar yaliyodumu kutoka Januari 12, hadi 26 Aprili, mwaka 1964.

Ahmed Rajab RAIA MWEMA 22-February, 2012
 
Tunapoelekea kwenye kilele cha sherehe za Mapinduzi ningependa tujiulize swali hilo ambalo limekuwa na mkanganyiko sana kutokana na Itikadi mbalbal za watu.

Je, baba wa Taifa la ZANZIBAR NI NANI KATI YA HAWA?
(a)John Okelo
(b)Abeid Karume
(c)Sultani bin Said

Zanzibar ni nchi ya Kiislam haina baba wa Taifa, mara nyingi nchi zenye kumfanya mtu baba wa Taifa ni nchi za Kikiristo. Wakiristo ndio hupenda kumtukuza mtu halafu wakamwita baba na humuabudu au kuchonga sanamu lake kisha wakaweka majumbani mwao wakimuabudu baba yao kama ilivyo Tanganyika leo wanavyomuabudu Julius Nyerere.
 
Dereva Tax akimpeleka mjamzito Hospitali na mama akajifungua salama , yeye Dereva Tax hawi baba wa yule mtoto

Niliwahi kumkuta jamaa mmoja na mke wake Jangwani mama akiwa hatua za mwisho kujifungua, nikawapeleka hospitali ya muhimbili, after 40 minutes baba/mme wa yule mama akanipigia simu kunishukuru

Okello alitumiwa tu na ndio maana historia yake haieleweki, Uganda, tanzania na kenya wote kwa nyakati Tofauti wame enjoy services za Okello

All in all dhana ya ubaba kwa taifa fulani is very very questionable and debatable

Usimfananishe Okello na dreva Taxi coz ktk story yako yule baba mwenye mke hakukimbia kwenda kujificha mpaka mtoto alipozaliwa bali alikuwa bega kwa bega na mama. Bali Karume yeye alikimbilia mafichoni hadi mapinduzi yalipoisha Okelo akamwita na kumkabidhi nchi
 
LOL!!!!Yani Wazanzibari mna hasara. Mapinduzi yametokea huyo Karume wenu yuko Dar kuomba akili kutoka kwa Julius( inasemekana Julius ndo alikuwa amemshikia Karume akili zake zote!) Kusikia Okello kapindua nchi ikabidi abane hadi mapinduzi yaishe mzee katoka tunduni mdogo kama piritoni!! Kakabidhiwa nchi hata hajui pa kuanzia!
Duh! Kama namwona vile anavyovibrate!! Poor u n him!
 
Naheshimu mapinduzi,namheshimu hayati karume. Lakini sifurahishwi na kutomuenzi kwa jinsi yeyote field marshal okelo. Ukichukulia yeye ndie aliyeratibu na aliyeongoza mapambano ya mapinduzi. Basi hata picha zake tu zingebandikwa uwanjani.

Labda walivyomualika Yoweri Mseveni ni namna kumuenzi FM Okello kimya kimya!
 
Philemon umesema ukweli,

Historia ya Tanzania imekuwa na tabia ya kufuta michango ya wale ambao hawakupendwa na wakubwa: John Okello akiwa mmoja wao.

Ingawa sijasoma maandiko yaliyopo kuhusu historia ya Tanzania kwa muda mrefu ukweli wa kuwa majina kama ya Okello, Kambona, na Kanali Mahafudhi yamefutika kabisa katika historia ya Tanzania. Bibi Titi Mohammed alipata bahati baada ya kurudi CCM na hivyo kurudisha jina lake katika historia lakini nalo lilikuwa limeshapotea.

Tutafute utaratibu wa kutunza historia kamilifu ya nchi bila kujali uhusiano wa wahusika na "ukoo wa mfalme" ulikuwaje.

yeye alikua askari wa kukodiwa.mercanery.....hana utambulisho....ni mpiganaji wa kikristo aliekodiwa kwa niaba ya kanisa kuumaliza uislam zanzibar...haya mengine ni porojo tu...
 
Wanabodi,

Japo Shujaa wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni Sheikh Abedi Amani Karume, Kiongozi halisi wa Mapinduzi yale ni Field Marshal John Okelo.

Uthibitisho ni hii press conference ya Karume, Okelo na Babu, na wote wanamuelezea Okello kama ndie kiongozi wa Mapinduzi yale Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.

http://youtu.be/-sMDkCSC_5g





[h=1]Press Conference ya John Okello. [/h]








Kuona ni kuamini.

Tuacheni ubishi!. Karume hakuwepo Zanzibar, siku ya Mapinduzi!. Alikuja bara kuwapeleka shule wanaye Amani na Ali waliokuwa wakisoma kwenye nchini babu yao mzaa Baba!.

Nawatakia Mapumziko Memsa ya kusherehekea Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Pasco.
 




[h=1]الجزء الثاني زنجبار اندلس افريقيا Zanzibar Revolution[/h]





 
ndugu pasco, kuna uzi zaidi ya mitano inayoongelea swala hili na wewe ni mkongwe hapa sidhani kama kulikuwa kuna haja ya kuanzisha uzi ,badala yake ungechangia tu uzi zilizopo kuhusu Okelo na karume na zanzibar
 
wanabodi,

japo shujaa wa mapinduzi matukufu ya zanzibar ni sheikh abedi amani karume, kiongozi halisi wa mapinduzi yale ni field marshal john okelo.

Uthibitisho ni hii press conference ya karume, okelo na babu, na wote wanamuelezea okello kama ndie kiongozi wa mapinduzi yale matukufu ya zanzibar ya mwaka 1964.

‫





press conference ya john okello.










kuona ni kuamini.

Tuacheni ubishi!. Karume hakuwepo zanzibar, siku ya mapinduzi!. Alikuja bara kuwapeleka shule wanaye amani na ali waliokuwa wakisoma kwenye nchini babu yao mzaa baba!.

Nawatakia mapumziko memsa ya kusherehekea miaka 50 ya mapinduzi matukufu ya zanzibar.

Pasco.

kwa maelezo zaidi wasome kitabu hiki cha kijana msomi gharis ghassani
 




[h=1]الجزء الثاني زنجبار اندلس افريقيا Zanzibar Revolution[/h]






?;:€€^_^©€¢€°_©¶<>>^©€¢€©\<>^^°®¢€°©©\>==_^¶€°&#8730;&#960;÷_^€&#8730;&#960;°©\<=^°€•&#8730;÷×&#960;&#8730;€¢_=>¶®®\>_€=÷× Liberation
 
Ahsante Pasco. Nadhani mzizi wa fitna umekatwa. Wapo Wazanzibari wakisikia jina la Okello,povu linawatoka kama wametafuna sabuni,wapotoshaji wakubwa wa historia. Subiri waje kukanusha hata picha na sauti.
 
Field Marshal John Okello alikuwa kamanda aliye "engeneer" mapinduzi .
Mzee Karume, Hanga na Marehemu Babu walikuwa Dsm.
Shujaa wa mapinduzi kwa maana nzima ya kufanikisha ni Fm John Okello.
 
Back
Top Bottom