Ukiambiwa wewe ni mpumbavu uso utakuparama kama uji wa limao... jitafakari na ujitazame kama hayo unayoyashabikia yana tija.Hoja inapate nguvu wakati wabunge wa upinzani wanapukutika tu
Chadema ndio imekufa kanda ya ziwa kwa ubinafsi wa Mbowe,.Bado huyo wa ukerewe anasubiri msiba uishe,chadema kinakua officially chama cha kikanda
Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.
Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.
Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.
Akitangaza kujivua uanachama amesema,
Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.
Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.
VIDEO:
Demokrasia ni gharama mkuu na fedha za uchaguzi zina bajeti yake.
Nafikiri kuna haja ya kupitisha sheria kwamba ukiacha ubunge hakuna kugombea tena mpaka awamu hiyo ipite au kama unataka kugombea basi lipia gharama zote za uchaguzi.. Huu ni upumbavu wa halo ya juu sana.. Kamekua kama kamchezo sasa.. Kodi zetu zinaenda kis*e**e tuuu
Yap. Hiyo itakuwa vizuri. Maana watu wameshaona ni kamchezo fulani hiv cha kujipatia pesa. Huku ni kuwatesa wananchiNafikiri kuna haja ya kupitisha sheria kwamba ukiacha ubunge hakuna kugombea tena mpaka awamu hiyo ipite au kama unataka kugombea basi lipia gharama zote za uchaguzi.. Huu ni upumbavu wa halo ya juu sana.. Kamekua kama kamchezo sasa.. Kodi zetu zinaenda kis*e**e tuuu
Wakati wa kupitisha bajeti sikusikia mbunge wa Chadema akiomba bajeti ya NEC ipunguzwe ili kuongeza mshahara wa watumishi au sikusikia ruzuku ifutwe ili kuongeza mishahara.Kwani kwa watumishi wa umma hakuna bajeti yake,mbona hakuna nyongeza wala kupanda madaraja.
Wewe hauko sawa.
Ndiyo wanasema: If you can't fight them, join them. Ameogopa dada zake kuolewa na mkurugenziAmeenda kuungana na fisadi ili waendeleze ufisadi. Ukimuuliza leo kuhusu ufisdi wa mkurugenzi, atakuambia mlimnukuu vibaya
Wakati wa kupitisha bajeti sikusikia mbunge wa Chadema akiomba bajeti ya NEC ipunguzwe ili kuongeza mshahara wa watumishi au sikusikia ruzuku ifutwe ili kuongeza mishahara.
Unafiki huu wa kuwakumbuka wafanyakazi unakuja nyakati hizi mnapoondokewa na wanachama?