MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

Inasemekana wengine huwa wanabakwa na kirekodiwa video wanatishiwa usipounga mkono juhudi tunaachia hii video raia waone ulivyofokolewa choo!
 
Mtu anashauri nchi wahisani wasitishe mikopo...ili miradi ya maendeleo isikamilike...unadhani huyo hazuii kupatikana 'maziwa na asali' nchini? Tena anaenda mchana kweupe na kujiapiza kuwa hataunga mkono juhudi za serikali, unategemea nini?
Maziwa na asali inayotegemea misaada na mikopo? Miaka 60 bado mnategemea kuiletea hii nchi maendeleo kwa kutegemea mikopo na misaada? Pathetic.
 
Pimbi tuliza mshono, hii mambo haitaleta nafuu yeyote kwny ugum wa maisha unaopitia hapo geto kwako yombo buza

Naona ' Gheto ' ambalo kila mara huwa unakuja na ' nakupanua ' hilo ' Nyabe ' lako huwezi kulisahau. Karibu tena na leo utanikuta!
 
Nafikiri kuna haja ya kupitisha sheria kwamba ukiacha ubunge hakuna kugombea tena mpaka awamu hiyo ipite au kama unataka kugombea basi lipia gharama zote za uchaguzi.. Huu ni upumbavu wa halo ya juu sana.. Kamekua kama kamchezo sasa.. Kodi zetu zinaenda kis*e**e tuuu
CCM hatuwezi kukubali
 

Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.

Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.

Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.

Akitangaza kujivua uanachama amesema,

Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.

Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.


VIDEO:

​
Kumbe huyu mwalimu anatumia mtilio wa kemia ya Mkandawile hahahaha
 
Hawa wanaohama na wanaowaunga mkono wote ni WAHUJUMU UCHUMI! Huwezi kuliingiza taifa ktk gharama zote hizo kisa kuunga mkono! Kwani huko ambako wanakwenda c kuna walioko huko? Jee huko kuna MAENDELEO GANI? Au huko Hakuna shida? Mbona kama ni malalamiko waTz wote tunafanana ktk malalamiko?
 
Mkuu unajua maana ya democrasia? Democrasia ina gharama zake.
Hii sio demokrasia,ni rushwa!Unamuahidi mtu madaraka ili ahamie kwenye chama chako kisa una dola!Hii inaitwa misuse of public office for private gain!!!!!!!Halafu private gain ni nini sasa,eti jiwe afurahie kuungwa mkono,yani nafsi yake ifurahi tu!
 
Unaongelea ubunge umesahau uraisi,Lowasa aliingia chadema vuuuu akapewa ugombea uraisi chap chap
Hawa jamaa sijui huwa wanatumia kiungo gani kufikiria. Wamesahau kabisa jinsi gia ya angani ilivyovunja katiba ya chadema na kuharibu upepo wa kisiasa nchi hii. 'Unavuna ulichopanda.
 
Hii sio demokrasia,ni rushwa!Unamuahidi mtu madaraka ili ahamie kwenye chama chako
Ulikuwepo muda akiahidiwa? Anahaki ya kuhamia popote kwa jinsi anavyoona inafaa. Mbona kina Lowasa walihamia chadema tukawadekia hadi barabara kwa shangwe?
 
Mkuu mbona unashangaa? Magufuli ni rais mzuri mno,hana kasoro yoyote ile,na Tanzania haitapata rais bora kama Magufuli,tangu aingie madarakani uchumi wa Tanzania umepaa kwa 45%,ajira zimeongezeka kwa 38%, Demokrasia imeshamiri,Uhuru wa vyombo vya Habari umekua,sasa kwa nini wapinzani wasimuunge mkono?
Napendekeza Magufuli atawale milele.
CCM HOYEEEEEEEE......!!!
Akamtawale mama yako milele hapo vp?
 
Ulikuwepo muda akiahidiwa? Anahaki ya kuhamia popote kwa jinsi anavyoona inafaa. Mbona kina Lowasa walihamia chadema tukawadekia hadi barabara kwa shangwe?
Hukusikia Waitara alichosema?Alisema "mimi nachojali ni ubunge wangu nilioahidiwa,hayo mambo ya gharama za uchaguzi hayanihusu"!
 
Jamaa kagundua kua hata uchaguzi ukiitishwa Chadema watasusia atapita bila kupingwa.

Tubadili katiba, kama mtu anataka kuhama chama ahame bila kutuingiza kwenye hasara za uchaguzi.

Nchi hii bado masikini, vipaumbele ni vingi sana, pesa iende kwenye mambo ya msingi na sio kila siku ni uchaguzi.

By t way kuna majimbo zaidi ya 150 ya yanayoongozwa na ccm toka 2015, wabunge wake wanaunga mkono CCM since then, sioni tofauti yake ya maisha na majimbo yasiyo ya CCM. Kuunga mkono au kutounga sijaona tofauti.

Tufanye wabunge wote wa upinzani waunge mkono jitihada za rais, je itabadili hali yetu ya maisha na kua mazuri zaidi, Tanzania itaanza kutiririka maziwa na asali? Kwamba kutokuunga mkono ndio kunazuia hayo?

Mwalimu alipambana na matatizo kama ujinga, maradhi, nk lakini hili la ujinga bado ni tatizo. Mtu anasema akiunga mkono analeta maendeleo, mbona maendeleo hayapo kwenye wabunge ambao ni wa ccm toka 2015?
Kula tano Mkuu
 
Mungu wangu sasa Saccos yetu itakuwaje?!!!, maana kila siku watu wanazidi kupungua.
 
Back
Top Bottom