MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

CCM ya sasa imeamua kutoa kafara kwa miungu iliyopo kwenye maji ili waweza kusurvive.
CHADEMA ya sasa hivi inafukuzana na vivuli tu. Kwa kifupi imepoteana.
Kwasasa CHADEMA ipo sababu upinzani dhidi ya serikali umeimarika sana na wapinzani halisi ni watu, hivyo CHADEMA inaishi kwa kivuli cha upinzani huu lakini wao kama chama na jinsi walivyo dhibitiwa na kubanwa kingekua kimeshajifia kitambo tu.
Ila nguvu watakayoamka nayo, ambayo watapewa na watu wa makundi yote itatisha sana
2 Wafalme 3:26-27. Naye mfalme wa Moabu alipoona ya kwamba wanashindwa vitani...ndipo akamtwaa mwanawe wa kwanza...akamtoa awe sadaka ya kafara ya kuteketezwa (ili aweze kushinda vita)
 
Tatizo sio mtu kuhama chama. Tatizo ni akili na fikra za wapiga kura/raia.
Wanahama na kushindishwa huko ccm kwa sababu sisi wapiga kura tunaonekana kama mazuzu/roboti tu.
Shame on us!
 
Sitashangaa akihama, kafara ya watu zaidi ya mia mbili si mchezo.
Hoja inapate nguvu wakati wabunge wa upinzani wanapukutika tu
Chadema ndio imekufa kanda ya ziwa kwa ubinafsi wa Mbowe,.Bado huyo wa ukerewe anasubiri msiba uishe,chadema kinakua officially chama cha kikanda
 
Naona ' Gheto ' ambalo kila mara huwa unakuja na ' nakupanua ' hilo ' Nyabe ' lako huwezi kulisahau. Karibu tena na leo utanikuta!
Nilijua tu lazima uongelee michezo yako ya jinsia moja, mkuu sikutegemea utakua addicted hv, lakin mjomba wako alikosea sana kukufundisha huo mchezo utoton

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
 

Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.

Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.

Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.

Akitangaza kujivua uanachama amesema,

Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.

Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.


VIDEO:

​
Taifa linapitia wakati mgumu sana, tumegubikwa na chuki, dhulma, ubinafsi, ubabe, kiburi, rushwa, vitisho na mauaji. Ee Mungu tunusuru waja wako!
 
Huyu nae kahongwa na serikali ya CCM. Hawa jamaa bwana, badala ya kupeleka hela za kununulia taa za kusaidia uokoaji wa watu wanaozama wao wanazipeleka katika kununua wabunge!!. Mambo ya ajabu kabisa.
 
Huyu ni yule aliyemwita Mkurugenzi Mwizi? Au siyo yeye kuna mbunge Alisema mkurugenzi Mwizi
 
Kuhama chama sio tatizo, kinachoniuma ni hizo pesa zinazoenda kutumika. Duniani kuna njia mbili tu za kukabiliana na adui either you fight until last or join them, Chadema sa hivi hakuna wanachopambania, hawana ajenda tena, waliobaki nao wamejawa uoga, mwisho wa siku kila mtu atahama.
 
Hizi zama zitapita na huu ujinga utapita tu.

Hoja ya Zitto kuhusu kile kifungu inazidi kupata nguvu kadri siku zinavyokwenda.

Kamwe hamtakuja kuniona namuunga mkono huyu mtu maana ni sawa na mhujumu uchumi.
Utamuunga mkono kupitia fake I'd?!??
 
Haikawii kuambiwa amenunuliwa na tulimuona siku nyingi nyendo zake za kutaka kutusaliti kamati kuu ilikaa na kumuandia barua ya kujieleza lkn kabla ya kumfukuza kaamua kuondoka.
Hiyo bado haibadili ukweli kwamba kuna kitu nyuma ya pazia ambacho sisi wanannchi wa kawaida hatuwezi kukijua!
 
Likiporomoka li chadema si ndo itakuwa vizuri mkuu ili li CCM litawale milele.
Kuiporomosha chadema ni kwa mtutu tu na sio kwa haki, mkitukia mtutu na kubambikia watu kesi kama mnavyofanya na tunaona, no comment
 
Hizi zama zitapita na huu ujinga utapita tu.

Hoja ya Zitto kuhusu kile kifungu inazidi kupata nguvu kadri siku zinavyokwenda.

Kamwe hamtakuja kuniona namuunga mkono huyu mtu maana ni sawa na mhujumu uchumi.
Utanyooka tu!! Karibu utabaki wewe tu
 
You (CCM) have created poverty for a purpose. And what you see is the result of the poverty strategy CCM created in TZ, it is bearing fruits.
Nashangaa CHADEMA wanashindwa kujua kwamba wanatatizo mpaka sasa?
Kama unateua wagombea ubunge wanaokuja kuhamahama kama hivi kwanini tusione wewe uliowateua na kuwapa ridhaa ndo unatatizo kubwa.
Au hawa walikuja huko Bahati mbaya na mafuriko yale ya 2015?
 
Duh kwl maisha hayana formula hawa jamaa c ndo wanasifikaga kwa misimamo mikali ya kutokuyumbishwa alianza lembeli akaapa kwa mizimu yote ya kwao mwishoni kalegea safari hii tutaona mengi
 
Elimu bure, ujenzi wa SGR, miradi ya ujenzi wa vituo vya afya na uboreshaji wa hospital nchini, miradi ya upatikanaji wa maji kwa wananchi mjiji na vijijini, miradi ya usambazaji umeme Mjini na Vijijini, vita dhidi ya ufisadi, rushwa na dawa za kulevya, usimamizi wa nidhamu na uwajibikaji kwa watendaji na watumishi wa umma, uzalishaji umeme wa gharama nafuu nk
...And yet we are one of poorest nations on planet earth.
 
Hii sio habari tena wala jambo la kushtua ila habari ni nani atasimama tena kwenye foleni ya kupiga kura wakati tayari anajua mshindi ni kutoka chama flani
 
Back
Top Bottom