MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

Jamaa kagundua kua hata uchaguzi ukiitishwa Chadema watasusia atapita bila kupingwa.

Tubadili katiba, kama mtu anataka kuhama chama ahame bila kutuingiza kwenye hasara za uchaguzi.

Nchi hii bado masikini, vipaumbele ni vingi sana, pesa iende kwenye mambo ya msingi na sio kila siku ni uchaguzi.

By t way kuna majimbo zaidi ya 150 ya yanayoongozwa na ccm toka 2015, wabunge wake wanaunga mkono CCM since then, sioni tofauti yake ya maisha na majimbo yasiyo ya CCM. Kuunga mkono au kutounga sijaona tofauti.

Tufanye wabunge wote wa upinzani waunge mkono jitihada za rais, je itabadili hali yetu ya maisha na kua mazuri zaidi, Tanzania itaanza kutiririka maziwa na asali? Kwamba kutokuunga mkono ndio kunazuia hayo?

Mwalimu alipambana na matatizo kama ujinga, maradhi, nk lakini hili la ujinga bado ni tatizo. Mtu anasema akiunga mkono analeta maendeleo, mbona maendeleo hayapo kwenye wabunge ambao ni wa ccm toka 2015?
Tatizo ni Mbowe na group lake (Group of boys) Kabla ya katiba demokrasia ya ndani ya vyama isimamiwe
 
ngoja tuone wale wafia chama kama watapewa nafasi kugombea nafasi teule...
ANGALIZO: Ule mwendelezo niliousema hapo awali kuwa sasa FISIEM imeamua kuhamisha utawala kwa CDM kwa style ya kuwavalisha magamba wanaCDM na kuwapa nafasi kuongoza serekale.
NYIE WAFIA CHAMA ENDELEENI KUPIGA KWATA TU.
CC: jingalao Ruttashobolwa cocochanel stroke Ufipa-Kinondoni Pascal Mayalla UCD Makusudically Mshana Jr
Washabiki wa CHADEMA ni wakati sasa wa kujitambua kuwa chama kisiasa kilikufa wakati kilipompokea Lowassa na Dr Slaa (great thinker wake) akaondoka. Viongozi waliobaki ni wachumia tumbo wakimwogopa na kumsujudu Mbowe kama Mungu mtu.

Isitoshe wale waliohama CCM walimfuata Lowassa wakiamini angekuwa Rais na wao wakapata cheo. Sasa wanaona aibu kurudi CCM. Ni Masha tu amethubutu kurudi kwa kuwa ana uwezo kipesa. Naamini wakikosa Ubunge watajuta kama hawatafanya maamuzi magumu kwa sasa hivi.

Ukweli ni kwamba wanasiasa wa dhati walikuwa wakati wa awamu ya kwanza ya utawala wa nchi hii. Baada ya hapo wengi wao ni wachumia tumbo. Lakini bahati mbaya utawala wa sasa haukumbatii wanasiasa wachumia tumbo. Hivyo Uchaguzi Mkuu wa 2020 tutegemee kuona mabadiliko makubwa ya wagombea ubunge katika CCM kwani wengi ama watakatwa au hawatajitokeza kuomba kuteuliwa kugombea.
 
Elimu bure, ujenzi wa SGR, miradi ya ujenzi wa vituo vya afya na uboreshaji wa hospital nchini, miradi ya upatikanaji wa maji kwa wananchi mjiji na vijijini, miradi ya usambazaji umeme Mjini na Vijijini, vita dhidi ya ufisadi, rushwa na dawa za kulevya, usimamizi wa nidhamu na uwajibikaji kwa watendaji na watumishi wa umma, uzalishaji umeme wa gharama nafuu nk
Yapata miaka 57 sasa bado maji na umeme ni tatizo halafu tunajiita donor country, kuna vitu kiuhalisia ukivifikiria unajikuta unacheka pekeako kama mwendawazimu [emoji13] [emoji3] [emoji1]
 
5741-1.gif

icon_lol.gif
icon_lol.gif
icon_lol.gif
qRI8Gs7.gif
qRI8Gs7.gif
qRI8Gs7.gif
qRI8Gs7.gif
qRI8Gs7.gif
 

Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.

Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.

Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.

Akitangaza kujivua uanachama amesema,

Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.

Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.


VIDEO:

​

Leading without vision ni changamoto......
 
Yapata miaka 57 sasa bado maji na umeme ni tatizo halafu tunajiita donor country, kuna vitu kiuhalisia ukivifikiria unajikuta unacheka pekeako kama mwendawazimu [emoji13] [emoji3] [emoji1]
Toka umefikisha miaka kumi na nane mpaka muda huu umefanya nini cha maana bila dhuluma wa hila kwako binafsi na nchi yako kwa uraia wa kuzaliwa? Na wakati unafanya hayo ulikumbana na changamoto zipi? Je. katika harakati zako hizo uliwasaidiaje viongozi wa taifa lako kwa kuzaliwa kufanikisha azma yao ya kuboresha maisha ya raia wa taifa lako?

Karibu utupe majibu mujarabu.
 
Keshafika bei huyo... Wacha aondoke

Ni hake yake ya msingi na ndiyo ukomavu wa demokrasia. Nyalandu, Lowasa na wana CCM wengi tu walihamia Chadema siku za nyuma na hatukusikia watu kusema wamefika bei badala yake wengi waliunga mkono na kusema ni haki yao ya kidemokrasia kuhama chama.
 
Napenda kuchukua fura hii kukupongeza Mh Marwa Ryoba Mbunge ya jimbo letu la Serengeti kwa kufanya maamuzi magumu na ya busara kwa kujivua unachama wako wa CHADEMA na kuhamia ccm. Najua wasio na akili watakubeza lakini mi najua hutakaa hata siku moja ujutie uamuzi wako. Hata hivyo nawashauri madiwani wa CHADEMA wa wilaya ya Serengeti wakati ni huu sasa wa kufuata nyao na mheshimiwa Ryoba wahamie CCM ili waje tuijenge wilaya yetu ambayo iko nyuma sana kimaendeleo.
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Mbona inajulikana ni kuwa ni kijani tangu kitambo hata alishasema anaweza kuwa kijani ,ulitaka ishara IPI tena
 
Hivi unajua Marekani inadaiwa shilingi ngapi, siyo dola shilingi ? Kama hujui fuatilia link hii
http://www.usdebtclock.org/
Halafu urudi hapa ulete mrejesho. Hili uelewe maana ya saa hiyo ya madeni ya marekani linganisha tarakimu zenye rangi nyekundu na zile za kijani
Hujui chochote, jadiliana na vilaza wenzio.

Marekani kudaiwa inahusiana nini na Tanzania kuomba misaada na kutegemea misaada kutekeleza majeti yake?

Unatetea utegemezi wa Tanzania kisa Marekani inadaiwa? Hoja za kitaahira hizi jadiliana na majuha wenzio.

Ahsante.
 
Tatizo ni Mbowe na group lake (Group of boys) Kabla ya katiba demokrasia ya ndani ya vyama isimamiwe
Ni chama gani hapa nchini kinafuata katiba yake?
Ccm wanawapitisha kina Waitara kwa utaratibu upi? Mwenyekiti anachaguliwa kwa utaratibu upi?

Hakuna chama kinafuata utaratibu wa katiba yake.
 
Inagharama at the expense of leaving more.than 300 people dying in a sinking ferry for lack of modern rescue facilities.
Mkuu mbona nimechangia kwa kiswahili alafu wewe umenijibu kwakidhungu? Naona mapichapicha tu, naomba nifafanulie kiongozi. Tafadhari
 
Hujui chochote, jadiliana na vilaza wenzio.

Marekani kudaiwa inahusiana nini na Tanzania kuomba misaada na kutegemea misaada kutekeleza majeti yake?

Unatetea utegemezi wa Tanzania kisa Marekani inadaiwa? Hoja za kitaahira hizi jadiliana na majuha wenzio.

Ahsante.
Taratibu, taratibu...mkuu; huku sis hatuna 'maji' ukitupaka hilo povu tutajisafisha na nini? Halafu nakushangaa...umepewa 'assignment' nyepesi namna hiyo kichwa kinakuuma namna hii, sasa kweli tukikupa mamlaka ya kutanzua mtanzuo wa wana'kusadikika' si-ndo tutakupeleka ICU bila kupenda!!!
Nikirudi kwenye mada.
Hivi kama hauoni uhusiano wa Marekani (Yenye Umri zaidi ya mika mia) kudaiwa tena kwa kukopa sana (China), sasa unashangaa nini Tanzania yenye umri wa hiyo miaka 57 uliyotaja kukopa kutoka kwa wahisani wakopeshaji!!! Hivi na hili unataka wana JF wapige kura kuchagua ama wewe upelekwe kwenye kundi la majuha ama kundi la wapumbavu?? Ebu wahurumie wanaJF wana kazi nyingine muhimu za kufanya.
 
Yapata miaka 57 sasa bado maji na umeme ni tatizo halafu tunajiita donor country, kuna vitu kiuhalisia ukivifikiria unajikuta unacheka pekeako kama mwendawazimu [emoji13] [emoji3] [emoji1]
Yapata miaka 26 makao yetu makuu bado mithili ya banda la kuku.
 
Back
Top Bottom