MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

Kwani mkurugenzi kakubali kuoa mmoja wa dada zake kama ilivyopendekezwa au?
 
MARWA CHACHA
Rudi nyumbani kumenogaaaa.......?
nategea kesho kusikia MBOWE na LISSU wakiimba wimbo wa KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Jamaa katongozwa mchana tena mwanaume akiwa Dar yeye yupo zake mbugani humo usiku kalegea mwenyewe.
 
Hii nimeinasa jikoni kabisa kutoka chanzo changu cha kuaminika!Picha iko hivii,huyu jamaa ameombwa atulie pembeni na asigombee uchaguzi wa marudio huku akitafutiwa fursa nyingine taratibu!
Hii ni kuzima hisia za wanaccm ambao wanaona kila anayeunga mkono juhudi anakula shavu immediately!
 
Rais mzima unakaa jukwaani ukiwashawishi wapinzani wahame ili wakuunge mkono una ajenda gani ya siri? Ila kwakuwa ulishasema kuwa wewe ni kichaa basi acha vichaa wakuunge mkono. Vichaa mkaungane huko muendeleze ukichaa wenu.
 
Nazidi kupata sababu za kutopiga kura 2020, 2015 was my first and as it goes, sidhani kama nitapoteza mda kupanga foleni tena.
 
Hebu tutathmini maendeleo yaliyopatikana kwa majimbo ya CCM kama ya Dodoma, Singida ili tujiridhishe kama hii hamahama ni rushwa au development based
Jamaa kagundua kua hata uchaguzi ukiitishwa Chadema watasusia atapita bila kupingwa.

Tubadili katiba, kama mtu anataka kuhama chama ahame bila kutuingiza kwenye hasara za uchaguzi.

Nchi hii bado masikini, vipaumbele ni vingi sana, pesa iende kwenye mambo ya msingi na sio kila siku ni uchaguzi.

By t way kuna majimbo zaidi ya 150 ya yanayoongozwa na ccm toka 2015, wabunge wake wanaunga mkono CCM since then, sioni tofauti yake ya maisha na majimbo yasiyo ya CCM. Kuunga mkono au kutounga sijaona tofauti.

Tufanye wabunge wote wa upinzani waunge mkono jitihada za rais, je itabadili hali yetu ya maisha na kua mazuri zaidi, Tanzania itaanza kutiririka maziwa na asali? Kwamba kutokuunga mkono ndio kunazuia hayo?

Mwalimu alipambana na matatizo kama ujinga, maradhi, nk lakini hili la ujinga bado ni tatizo. Mtu anasema akiunga mkono analeta maendeleo, mbona maendeleo hayapo kwenye wabunge ambao ni wa ccm toka 2015?
 
Unaweza ukaunga mkono juhudi za mheshimiwa rais hata ukiwa upinzani cha msingi ni kutokwenda kinyume na sheria jambo jema likifanyika upinzani hukaa kimya ila ikitioke kuna vitu tofauti vimefanyika ndo utasikia upinzani wakipiga kelele but mwisho wa siku ni maamuzi ya mtu #AMEAMUA
 
Time is the best judge, hayo mambo yana mwisho wake and the truth will reveal itself.
 
Hivi hakuna sheria inayomtaka mtu anayegombea nafasi ya uongozi wa kupigiwa kura awe mwananchama wa chama hicho kwa muda maalum? Mtu anaingia tu ndani ya chama na hapo hapo anapewa nafasi ya kugombea ubunge?
Siku hizi sheria ziko kwenye maandishi tu[emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28]
 
Hawa wasaliti wanapaswa kupigwa mawe, huu ni ukuda!
 
Hizi zama zitapita na huu ujinga utapita tu.

Hoja ya Zitto kuhusu kile kifungu inazidi kupata nguvu kadri siku zinavyokwenda.

Kamwe hamtakuja kuniona namuunga mkono huyu mtu maana ni sawa na mhujumu uchumi.
Toa boriti jichoni kwako kwanza maana uliyemnanga ana kibanzi tu.

Mvaa kiatu ndiye anajua kinapomminya sana na ni hao Madiwani na Wabunge wanaotoka CHADEMA na kuhamia CCM. Wewe ni shabiki tu wa humu JF, na kama una cheo huko CHADEMA, mwenzio akinyolewa nawe nywele tia maji.

Siamini wote hao ni watu wa hovyo. Wangekuwa hawafai, CHADEMA isingewasimamisha kugombea na wananchi wakawapa kura.

Amini usiamini CHADEMA kuna tatizo kubwa na siyo dogo.
 
Muache tu aende tulimsikia akisema "Msinizomee hata Mimi naweza kuwa CCM"
 

Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.

Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.

Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.

Akitangaza kujivua uanachama amesema,

Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.

Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.


VIDEO:

​

ngoja tuone wale wafia chama kama watapewa nafasi kugombea nafasi teule...
ANGALIZO: Ule mwendelezo niliousema hapo awali kuwa sasa FISIEM imeamua kuhamisha utawala kwa CDM kwa style ya kuwavalisha magamba wanaCDM na kuwapa nafasi kuongoza serekale.
NYIE WAFIA CHAMA ENDELEENI KUPIGA KWATA TU.
CC: jingalao Ruttashobolwa cocochanel stroke Ufipa-Kinondoni Pascal Mayalla UCD Makusudically Mshana Jr
 
Kumbe ndo huyu jamaa duhh /alimtuhumu mkurugenzi kuwa mwizi mbele ya Rais kumbe na yeye alikuwa kwenye list ya manunuzi ambapo kila tenda inayotangazwa ya kununua madiwani na wabunge then CCM lazima ishinde tenda hiyo/kweli we are in a right track
No Democratik election in tz under that circumstances[emoji41]
 
Back
Top Bottom