MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.

Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.

Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.

Akitangaza kujivua uanachama amesema,

Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.

Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.

VIDEO:

​

Huyu tayari amefikia bei bado wako tena 2 wanafanya bagening price polepole alisema wako 3
 
kwani huyu ndie yule alieambiwa atoe mkono mfukoni? wakachukua na kisemeo? au sie?
 
Washabiki wa CHADEMA ni wakati sasa wa kujitambua kuwa chama kisiasa kilikufa wakati kilipompokea Lowassa na Dr Slaa (great thinker wake) akaondoka. Viongozi waliobaki ni wachumia tumbo wakimwogopa na kumsujudu Mbowe kama Mungu mtu.

Isitoshe wale waliohama CCM walimfuata Lowassa wakiamini angekuwa Rais na wao wakapata cheo. Sasa wanaona aibu kurudi CCM. Ni Masha tu amethubutu kurudi kwa kuwa ana uwezo kipesa. Naamini wakikosa Ubunge watajuta kama hawatafanya maamuzi magumu kwa sasa hivi.

Ukweli ni kwamba wanasiasa wa dhati walikuwa wakati wa awamu ya kwanza ya utawala wa nchi hii. Baada ya hapo wengi wao ni wachumia tumbo. Lakini bahati mbaya utawala wa sasa haukumbatii wanasiasa wachumia tumbo. Hivyo Uchaguzi Mkuu wa 2020 tutegemee kuona mabadiliko makubwa ya wagombea ubunge katika CCM kwani wengi ama watakatwa au hawatajitokeza kuomba kuteuliwa kugombea.
AHHAAAAA!!! SI NILISEMA! wafia chama wajuaji utawajua tu. endeleeni kupiga kwata[emoji12] [emoji12] [emoji22] [emoji22]
mtafia sana FISIEM. NYAZIFA NI MPAKA UWE MWANACDM.
We endela kupiga DOMOZEGE LAKO

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Hizi zama zitapita na huu ujinga utapita tu.

Hoja ya Zitto kuhusu kile kifungu inazidi kupata nguvu kadri siku zinavyokwenda.

Kamwe hamtakuja kuniona namuunga mkono huyu mtu maana ni sawa na mhujumu uchumi.
Kwani umeombwa kumuunga, baki hivo hivo.
 
Mbosso aliimba "Umenishika pabaya"... Hapa Mbowe kashikwa pabaya ha ha haaa
Ndugu uchaguzi mmoja wa marudio ni tsh 500 milioni, ndugu hii ni kodi yako, ambayo ingeondoa kero ktk sekta ya elimu km madawati,afya,maji nk.ni nani anaumia hapa? Unahisi Ni mbowe ? Hapana, ni wewe na mimi na watanzania wote. Mbowe hawazi mwanae atasomaje, hana shida ya kutibiwa popote duniani ataenda kutibiwa. Leo Mbowe nae anaweza kuunga juhudi mkono ataendelea kupiga mamilioni ya fedha ndani na nje ya bunge akapewa hata uwaziri, unahisi mbowe anashida Chadema ikifa? Anaweza kusikitika tu tena atawasikitikia wananchi maskini, nani atawasemea tena, yeye hana shida wala tabu ktk familia yake. Jisikitikie wewe ba wananchi maskini wanaotafuta maji ndoo moja kutwa nzima.BADILI NAMNA UNAVYOFIKIRI JAPO ANACHOPOST MTU HUMU JUKWAANI WAKAT MWINGINE KINAREFLECT UWEZO WA MTU WA KUFIKIRI PIA.
 
Toka umefikisha miaka kumi na nane mpaka muda huu umefanya nini cha maana bila dhuluma wa hila kwako binafsi na nchi yako kwa uraia wa kuzaliwa? Na wakati unafanya hayo ulikumbana na changamoto zipi? Je. katika harakati zako hizo uliwasaidiaje viongozi wa taifa lako kwa kuzaliwa kufanikisha azma yao ya kuboresha maisha ya raia wa taifa lako?

Karibu utupe majibu mujarabu.
WAFIA CHAMA MNAPATA TABUSANA[emoji12] [emoji61] [emoji574] [emoji574] [emoji90] [emoji571]

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
"Njooni kwangu ninyi nyoote msumbukao na mizigo ya kunyanyaswa, kubaguliwa, na kupelekeshwa na Mbowe nami nitawapumzisha"

"John Pombe Magufuli Rais wa Tanzania"
 
Ahame na ubunge wake,hizo pesa walipwe walimu wapya za kujikimu.
 
Wangeendelea kuunga mkono wakiwa huko lakini wanaogopa wataitwa wasaliti wa CDM. Labda ngoja avuke mstari ili wajue ameamua kuunga mkono juhudi.
 
ngoja tuone wale wafia chama kama watapewa nafasi kugombea nafasi teule...
ANGALIZO: Ule mwendelezo niliousema hapo awali kuwa sasa FISIEM imeamua kuhamisha utawala kwa CDM kwa style ya kuwavalisha magamba wanaCDM na kuwapa nafasi kuongoza serekale.
NYIE WAFIA CHAMA ENDELEENI KUPIGA KWATA TU.
CC: jingalao Ruttashobolwa cocochanel stroke Ufipa-Kinondoni Pascal Mayalla UCD Makusudically Mshana Jr

Unaniitia nini.. hii post nimeisoma tangu ikiwa na replies 8.. nikajikuta sikurudi.. haya ngoja nisome update kwenye post #1
 
AHHAAAAA!!! SI NILISEMA! wafia chama wajuaji utawajua tu. endeleeni kupiga kwata[emoji12] [emoji12] [emoji22] [emoji22]
mtafia sana FISIEM. NYAZIFA NI MPAKA UWE MWANACDM.
We endela kupiga DOMOZEGE LAKO

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
Kwa taarifa mimi si mfia chama chochote ila mzalendo na mchambuzi wa masuala ya maendeleo (siasa, elimu, afya, kilimo, uvuvi, tecnologia, nk). Hapa chini nakupa kitu kidogo tu kuhusu ninachojua na kuona.

Kiuchumi, Serikali inayoongozwa na Dr Magufuli iko katika njia sahihi, hasa ukizingatia inawekeza, kwa pesa zetu na mikopo, kwenye vichocheo vya kiuchumi km barabara, reli, ndege, vyombo vya majini, nk. Hii ni pamoja na usimamizi na uthibiti imara wa rasmali ardhi, km madini, wa nchi hii.

Tukiwa na miundo mbinu imara kutachochea shughuli zote za uzalishaji katika kilimo, uvuvi, viwanda nk. Itakuwa rahisi na haraka kufikisha mazao ya kilimo/uvuvi na bidhaa za viwandani kwenye masoko ndani na nje ya nchi.

Isitoshe kumekuwa na mabadiliko ya utendaji kazi ya viongozi wa kuteuliwa na Rais. Wakati awamu zilizopita za utawala wa nchi hii, viongozi waliona siasa ni utajirisho. Kwa sasa badala ya warsha zisizo na tija au safari za nje, tunawaona wakizunguka mikoani, kwa wananchi walengwa, kusikiliza na kutatua kero zao.

Wakati wa awamu za Serikali zilizopita, Ikulu ilikuwa kama hotel ya wenye fedha (matajiri), awamu hii Ikulu ni mahali patakatifu.

Wakati viongozi wa Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma, Serikali zilizopita, walifanya Taasisi hizo kama mali yao, sasa wanatumbuliwa hadharani wale wasiofaa au kutimiza wajibu wao ipasavyo. Ushahidi ni kwa Taasisi na Mashirika hayo kuanza kulipa gawio kwa Serikali. Cheo ni Dhamana, imani ya Chama Tawala, inayotekelezwa kwa vitendo.

Lakini, upande wa upinzani, japo wanaliona hilo, kwa kukosa agenda mbadala ya maendeleo, viongozi wake tunawashuhudia wakibwabwaja tu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Mashabiki humu, kama wewe MWALA, ni bingwa wa matusi. Vyovyote unavyofikiria, maendeleo yanayoonekana ni kwa faida yangu, yako na Watanzania wote.

MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPENI

WAKATI NDIO, KUPANGA NI KUCHAGUA.
 
Ndugu uchaguzi mmoja wa marudio ni tsh 500 milioni, ndugu hii ni kodi yako, ambayo ingeondoa kero ktk sekta ya elimu km madawati,afya,maji nk.ni nani anaumia hapa? Unahisi Ni mbowe ? Hapana, ni wewe na mimi na watanzania wote. Mbowe hawazi mwanae atasomaje, hana shida ya kutibiwa popote duniani ataenda kutibiwa. Leo Mbowe nae anaweza kuunga juhudi mkono ataendelea kupiga mamilioni ya fedha ndani na nje ya bunge akapewa hata uwaziri, unahisi mbowe anashida Chadema ikifa? Anaweza kusikitika tu tena atawasikitikia wananchi maskini, nani atawasemea tena, yeye hana shida wala tabu ktk familia yake. Jisikitikie wewe ba wananchi maskini wanaotafuta maji ndoo moja kutwa nzima.BADILI NAMNA UNAVYOFIKIRI JAPO ANACHOPOST MTU HUMU JUKWAANI WAKAT MWINGINE KINAREFLECT UWEZO WA MTU WA KUFIKIRI PIA.
Mbowe anawasemea maskini gani wakati yeye na viongozi wenzake Wabunge hufunga midomo, kususia vikao na kupinga bajeti?
 
Mimi hata Chadema wote wakiishia CCM mapenzi yangu juu ya Chama Cha Mapinduzi atabaki palepale.
 
Mbona hamkusema haya mapema na mmengoja ameondoka ndiyo sasa mnatutapikia hivi? Kataeni muwezavyo ila CHADEMA kuna tatizo la msingi ambalo kama msipokuwa makini nalo kuna uwezekano hadi kufikia mwaka 2020 huko akabaki tu mwenye Chama chake Mzee Edwin Mtei na Dalali wake Mkuu Freeman Mbowe na Wabunge wote wakarudi CCM. Yaani badala ya Kutafakari kwanini mnakimbiwa nyie mlivyo na akili fupi neno lenu la Kwanza na la Kujitetea ni kuwa ' Wananunulika ' na Serikali kupitia Chama Tawala cha CCM.Tukiwashaurini mnatudharau acheni sasa ' mkomeshwe ' labda mawazo yetu ya Kiuhalisia mtayakumbuka sasa na kubadilika.
Nani anawakomesha? Na kwa sababu ipi? Uchaguzi wa marudio ni hasara kwa nani na faida kwa yupi? Huyu mbunge angeweka mkutano akawaeleza wana wa Serengeti kuwa ili maendeleo yaje kuna moja, mbili, tatu tofauti na alivyodai 2015; awasikilize. Wangemjibu, wangemshauri. Kuna majimbo ya uchaguzi tangu kuundwa ni ya CCM. Yana tofauti gani na yale ambayo nayo tangu kuundwa kwake ni ngome ya upinzani? Gentamycine nisaidie jambo moja tu kuhusu biashara ya udiwani na ubunge. Ulimsikia Nassari na juhudi zake. Ulimsikia pia Mnyeti na tambo zake. Unapenda sana utambuliwe na ukubalike kama mtu makini. Toa ufafanuzi wa hili jambo leo, dunia nzima ikukubali au ikupuuze kama takataka nyingine. Kazi kwako.
 
Mbowe anawasemea maskini gani wakati yeye na viongozi wenzake Wabunge hufunga midomo, kususia vikao na kupinga bajeti?
Eleza kinagaubaga sababu za wao kufanya hivyo,Na km ulikuwa hujui ktk mabunge yote hasa haya ya jumuiya ya madola bajeti inapitishwa kwa kura. Nenda kenya nenda uganda na kokote kule. Pili ukiangalia bunge km una upeo wanachofanya upinzani ni kutaka marekebisho ktk maeneo kadhaa tena ktk mamb ya msingi. Na hata ccm wenyewe kuna mambo wnakuwa hawakubaliani nayo lkn wale wamedhibitiwa hawawez kufurukuta. Tatu najua wengi mnaotoa hizi hoja na lushangilia kila kitu ni wavulana ,Lengo kuu la kuundwa kwa chama cha siasa ni kushika dola. Hakuna jingine. Na upinzani hauendi bungeni kwenda kuisifu serikali na ukiona upinzani unasifu serikali jua hawajui wnachopigania. MWISHO NIKUULIZE KISWALI KIDOGO TU LA UFAHAMU: Unayaonaje au yatakuwaje maisha ya watanzania, au afya ya siasa za tanzania siku Upinzani utakapofutwa kabisa.
 
Back
Top Bottom