MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

Nadhani watafiti wa sayansi ya siasa wangejaribu kufanya tafiti kuona namna ambavyo ulimwengu unatutazama kufaatia hama hama hii ya wanasiasa toka upinzani kwenda CCM na hasa kwa kuzingatia kuwa wengi wanaohama ni aidha wabunge au madiwani wa kuchaguliwa.
 
Hizi zama zitapita na huu ujinga utapita tu.

Hoja ya Zitto kuhusu kile kifungu inazidi kupata nguvu kadri siku zinavyokwenda.

Kamwe hamtakuja kuniona namuunga mkono huyu mtu maana ni sawa na mhujumu uchumi.

Mkuu tena huu ujinga ni wa daraja la juu sana na ina akisi safari ndefu ya mtu mweusi kwenda ktk kujitambua,period
 
Hongera sana Marwa Chacha, umetumia vyema haki yako ya kikatiba kuhama chama usichokitaka na kuhamia chama unachokitaka.

Haki hii ndio haki ile ile aliyotumia Lowasa kuhamia chadema,,,, achana na hao wanaosema umefika bei, labda tuwaulize, Lowasa na yeye alifika bei?

mwosha akioshwa eenhe
 
Haikawii kuambiwa amenunuliwa na tulimuona siku nyingi nyendo zake za kutaka kutusaliti kamati kuu ilikaa na kumuandia barua ya kujieleza lkn kabla ya kumfukuza kaamua kuondoka.
Acha uongo wewe, ubavu wa kumfukuza hawana
 
Jamani,naomba mwongozo,nami nikitaka kuama chama nafanyaje?naisi nikiunga mkono juhudi za mkubwa,naweza kunufaika kidogo
 
Basi asigombee tena awaachie wengine; vinginevyo jamani tuchukue hatua za kinidhamu dhidi ya watu wanaotupotezea muda na fedha zetu.
 
Jamaa kagundua kua hata uchaguzi ukiitishwa Chadema watasusia atapita bila kupingwa.

Tubadili katiba, kama mtu anataka kuhama chama ahame bila kutuingiza kwenye hasara za uchaguzi.

Nchi hii bado masikini, vipaumbele ni vingi sana, pesa iende kwenye mambo ya msingi na sio kila siku ni uchaguzi.

By t way kuna majimbo zaidi ya 150 ya yanayoongozwa na ccm toka 2015, wabunge wake wanaunga mkono CCM since then, sioni tofauti yake ya maisha na majimbo yasiyo ya CCM. Kuunga mkono au kutounga sijaona tofauti.

Tufanye wabunge wote wa upinzani waunge mkono jitihada za rais, je itabadili hali yetu ya maisha na kua mazuri zaidi, Tanzania itaanza kutiririka maziwa na asali? Kwamba kutokuunga mkono ndio kunazuia hayo?

Mwalimu alipambana na matatizo kama ujinga, maradhi, nk lakini hili la ujinga bado ni tatizo. Mtu anasema akiunga mkono analeta maendeleo, mbona maendeleo hayapo kwenye wabunge ambao ni wa ccm toka 2015?
Hiki ndio kipaumbele cha CCM.Hii ni mipango ya kuwa na bunge la chama kimoja ccm, bunge ambalo bw mkubwa ataliweka mfukoni bila upinzani wwte na baada ya hapo atapeleka muswada bungeni wa kuongeza urais na ubunge uwe miaka saba baada ya hapo watarekebisha tena kuondoa ukomo wa uraisi. Haya ni maandalizi.
 
H

Aya yote unaongea kujifariji..ukweli unaujua..hivi watoti wa mwenye nyumba na watoto wa mpangaji nani ana uhuru kwa baba mwenye nyumba..?? Je watoto wa mpangaji wana haki sawa sawa na watoto wa mwenye nyumba..?? Baki na ukweli kwa moyo wako.

Mfano ulio utoa hauendani na Uhalisia ,kuongoza Nchi sio kama kuongoza Familia.Fikiri zaidi ya hapo.
 
Kiukweli Tanzania nchi yetu inahitaji maombi Sana Sana na kwa haraka zaidi
 
Hizi zama zitapita na huu ujinga utapita tu.

Hoja ya Zitto kuhusu kile kifungu inazidi kupata nguvu kadri siku zinavyokwenda.

Kamwe hamtakuja kuniona namuunga mkono huyu mtu maana ni sawa na mhujumu uchumi.
Mkuu baada ya hii sarakasi kuisha yatatokea yafuatayo:
1:Tanzania itakuwa nchi ya chama kimoja CCM watatawala watakavyo na Bw mkubwa ataliendesha bunge atakavyo bila upinzani wwte. Mkono wa chuma
2:Wakishapata hii majority ya utakuwa sasa muda muafaka wa kupeleka muswada bungeni na kuufanya uraisi kuwa miaka 7,nani atapinga mbele ya Bw mkubwa. Hvyo hii hama ni maandalizi kuhakikisha muswada utapitishwa bila kelele pengine kabla ya2020 ili uchaguzi ukafanyike 2022.
3:Baada ya muswada wa miaka saba kupita itakuwa ni kipimo sahihi kwao kusoma upepo wa kisiasa na hatimaye watapeleka muswada wa marekebisho ya katiba kuondoa ukomo wa uraisi. NA HAPA ITATIMIA KAULI YA BW MKUBWA KUWA CCM ITATAWALA MILELE.
4:Baada ya yote haya tutashuhudia UDIKTETA KAMILI na kwa hakika hakuna atayekuwa salama ndani ya nchi hii. Hata hawa wanaoshangilia Leo kwa kujua au kutokujua, itakuwa ni kilio na kusaga meno. NI MAONO YANGU HAYA KULINGANGA NA TREND YA MATUKIO YA KISIASA NCHINI. Walianza na kampeni MAGUFULI BAKI kelele zikazidi wakaacha, akaja Juma Nkamia na kusudio la muswada wa miaka saba wakaona muda na hali ys bunge hairuhusu. Tafakari kabla ya kushangilia kila kitu.
 
Kwani lazima uhame chadema ndio umuunge magufuli mkono juu ya hizo "maendeleo" unasema, kaa wewe hukupewa hela si ungekaa tu chadema na uendelee kumuunga mkono magufuli, sio lazima uende ccm ndio umuunge mkono magufuli,hii ujinga utaisha lini, na ndio tz tunaendelea kuwa na umasikini wa hali ya juu na ajabu, sasa mamilioni itatumika kwa uchanguzi,mhe mbunge umepewa milioni ngapi na siulizi kwa ubaya pls
 
Huo ubao ulivyochafuka mpaka nimedinda medulla Imagine ni Schrödinger equations imetandazwa hapo!
 
Mkuu mbona nimechangia kwa kiswahili alafu wewe umenijibu kwakidhungu? Naona mapichapicha tu, naomba nifafanulie kiongozi. Tafadhari
Nimesema demokrasia ina gharama kiasi ambacho tumeshindwa kuwaokoa watu karibu 300 waliozama kwenye kivuko kwa kukosa vifaa vya uokozi ambavyo pia vina gharama. Maana yake ni kuwa gharama ya demokrasia ni ya muhimu kuliko ya kuwahudumia wananchi wetu
 
Nimesema demokrasia ina gharama kiasi ambacho tumeshindwa kuwaokoa watu karibu 300 waliozama kwenye kivuko kwa kukosa vifaa vya uokozi ambavyo pia vina gharama. Maana yake ni kuwa gharama ya demokrasia ni ya muhimu kuliko ya kuwahudumia wananchi wetu
Mkuu unaonaje tukiachana kabisa na mambo ya uchaguzi ili kukwepa gharama, je unadhani wanademocrasia watakubali?
 
Pesa za uchaguzi zitakuwepo ila zile za maafa hazikuwepo
 
Back
Top Bottom