Mara ya kwanza nakanyaga Kigoma na niliyoyaona huko

Yeah Sina hakika kwakua sikukaa sanaa lakini ndo nimesema pengine maana kule kasulu naskia wamepakana na Uganda Kwahy huenda biashara ikawa changamfu maana nilinunua vitu kwa bei Chee tofauti na kigoma mjini.
Kasulu imepakana na Uganda?? 😃😃😃 umefika Kigoma kweli au umesimuliwa tuu hadithi.. manyovu ndo imepakana na Burundi na ukivuka ziwa unaenda Congo na Zambia. Uganda haipakani kwa sehemu yoyote na Wilaya ya Kasulu achia mbali Kigoma yote. Hapa unatunywesha chai.

Uganda imepakana na Kagera rudi Kasome tena geography au hata historia ya vita ya kagera
 
Ulifika na Kibirizi, mji mwema, mulole, ujiji na Livingstone?
 
Ndo maana nikasema nimeskia. Kufika nimefika ila nilizunguka pale pale stand nikaingia kwenye soko la nguo n.k nikarudi.
 
Na haijui Kigoma anaongea assumptions zake
Assumption kama zipi!?. Kuna kuijua na Kuna kutembea. Siwezi kuijua kwakua sio mkaazi wa huko nilienda tu kutembea na niliyoyaona ndo hayo, katika hayo kipi hakina ukweli!?.
 

Umenikumbusha nilipoenda kikazi kigoma kutoa mkono wa kwaheri kwa watu tuliokuwa tunafanya nao kazi za utafiti, Kasulu a lovely place, Kitimoto inauzwa kwenye vibanda kama vya huduma za kifedha, asubuhi unakutana na supu ya migebuka na mihogo mchemsho. Kule kwa kina Mzamiru kunaitwa matyazo wale waha wanaoishi kule jeuri sana, wajivuni sana na ukiwauliza kwann wanakuwa wajeuri wanadai eti sababu airport ya kwanza ilikuwa hapo 🤣🤣

Mkuu kama ulienda kigoma na hujapanda mchomoko "Toyota pro box" basi bado hujafurahia kigoma vizuri, mbele mnakaa abiria wawili, nyuma mnakaa 6 afu kwenye boneti wanajaza madumu ya mawese kama 50 hivi, kuingia na kutoka kigoma ni lazima kitambulisho au barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa, kila baada ya kilometre kadhaa kuna block askari wanakagua watu vitambulisho.

Buhigwe na kibindo sio sehemu za kuishi zile, mzunguko wa pesa ni mdogo sana.

Wakati naenda barabara ya lami kutoka kigoma to kasulu ndio ilikuwa kwenye hatua za mwisho mwisho kumaliziwa na kasulu to kibondo ilikuwa hata mpango wa kujengwa hakuna, nadhan hizo wilaya mbili kwa sasa zitakuwa zimeunganishwa kwa lami.


Mulukoyoyo guest tulivamiwa na askari usiku wa manane tulitwanga maswali ya kijinga sana, Rushwa kwa askari hapo ni nje nje.

Kigoma saa moja na dakika 45 jioni ndio jua linazama kabisa na saa 11 alfajiri ni kama saa nane ya usiku.

Siku narudi waha walianza kubisha kuanzia geita hadi morogoro, waha ubishi upo kwenye damu yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…