Au hadi yeye ndio akutafute au akupigie na ukipigiwa unaanza kuwaza "anataka pesa huyu" au unaanza kuwaza kuwa atakuusumbua kukuliza maswali ya umeshapata mchumba? Kanisani/msikitini unaenda? etc
View attachment 3310163
Ebu jiulize kama tumeshapata visa vya laana ya mama ilivyo na nguvu vile vile ndani yake lazima kuwe na baraka ilio na nguvu. Vile vile kama ilivyo laana kuwa haitoki kirahisi rahisi hivyo hivyo hio baraka special ndani yake haitoki kirahisi rahisi.
Na baraka hii anakuombea kila siku ila naamini itakuwa maradufu kama pale utakapo mkumbuka mama yako kwa nama ilio special, mara kwa mara na ukimuombea afya njema (sala) mara moja moja pale unapokutana naye au kumpigia.
MPIGIE MAMA SASA HIVI NA UMTAKIE SIKU NJEMA.