Wewe mwerevu sana, unafikiri huyo Marekani anaweza kuishi bila ya dunia?
Uzi unasema wazi ikitokea Marekani akapigwa vikwanzo ina maana wakubwa wa dunia walikaa chini wakajiuliza hayo yote uliyoyaandika na solutions zake ndio maana wakafikia hilo hitimisho. Sasa wewe mwerevu sana ina maana wewe una akili sana ya kujua vyote hivo kuliko hao superpower ambao wataamua kuweka hivyo vikwazo? Na hivyo vyote ulivyoeleza hapo kwani hakuna mbadala wake? Au ni Marekani pekee ndiye ana watu special wa kutengeneza hizo patents na wengine hawataweza?
Kama wana teknolojia si waunde vitu vipya vyenye uwezo zaidi na waache kuitegemea Marekani. Samsung ilianza 1938, unadhani hawajawahi kuwaza hivyo unavyoweza wewe leo? Tangu 1938 hawana mbadala wa hizo patents waje wazipate from nowhere leo 2022 kisa wamewekewa vikwazo unadhani ni rahisi. Umeshindwa kulima ukiwa na shibe, chakula kikiisha ndio unaanza kulima.
Watu gani duniani waliwahi kaa wakajadili kuitenga Marekani.
Marekani ndio nchi pekee iliwahi kopesha Ulaya kwenye vita ya pili ya dunia, na bado ikapeleka jeshi na wakashinda. Marshall Plan ya Marekani ilitoa mikopo kwa nchi za Ulaya kwenye vita ile mpaka mkopo wa mwisho Uingereza iliulipa mwaka 2006, vita iliisha 1945 ila muda wote huo Uingereza ilikuwa inalipa mkopo uliokuwa na riba ndogo sana sikumbuki kama ilikuwa inafika hata 5% na hawakulipa miaka miwili tu tangu waanze kulipa. Uingereza aachane na Marekani wa hivi aungane na China?
Huo ni mfano tu. China ana nini ambacho kuna mzungu atambabaikia! Au Russia ana nini cha ajabu, kwani gesi ndio anauza peke yake? Nchi kibao duniani zinaweza toa gesi badala ya Russia. Its just a matter of time wazungu wako busy kutafuta replacement. Netherlands, Finland, Poland wamekatiwa gesi na Russia wala hujasikia wamekufa au wameandamana.
Hakuna nchi za kukaa duniani eti zimuwekee vikwazo Marekani. Marekani yeye mwenyewe ndio anaweza wekea nchi vikwazo ikapata inflation ya 1,000%. Mkate wa elfu 2 ukauzwa milioni 2 ndani ya miaka miwili. China au Russia hazina hata uwezo wa kumwekea jirani vikwazo, wanachojua ni kususa kuuza gesi. Na wakisusa hata hizo nchi hazipati inflation wala ya 20%, hizo ndio nchi unasema ziiwekee vikwazo Marekani.
Kwanza haya tunayowaza leo wao wameyawaza miaka mingi na kwenye archives na libraries zao wameyahifadhi. UK ilishaacha ndoto za kuwa superpower wala kubishana na Marekani tangu 1956 kwenye Suez crisis. Wote hao Ufaransa, Ujerumani, Italy na kina nani wanajua sana umuhimu wa Marekani. China ni newcomer, kibongobongo tunasema "hana connection".
Na kitu kingine China hana mawazo kabisa ya kuitenga Ulaya au Marekani. Uchumi wake unawategemea hao kuliko hata majirani ambao wote wana ugomvi naye kasoro Urusi tu ambao migogoro yao waliimaliza 2008.
Tunaisema Marekani ambayo Chairman wa Federal Reserve Bwana Jerome Power na Secretary of Treasury nadhani alikuwa huyu huyu Liz Trus walipendekeza na bunge likaidhinisha kutoa dola trilioni 2 mwaka juzi ili kupunguza madhara ya COVID-19 kwa Wamarekani, raia walipewa hela direct yani kila mtu Marekani inajua anapata kiasi gani kwa mwaka na kwenye shida walijua kila anayestahili apewe kiasi gani. Leo hii eti marais hawa wanaoenda kwenye birthday party za bongofleva waiwekee vikwazo Marekani?
Hiyo $2 trillion inaizidi hata bajeti ya Russia. Russia hii ambayo kiuchumi inazidiwa na California jimbo moja pale Marekani. Sasa inaanzaje kuiwekea vikwazo Marekani au ikiitenga inaathirika na nini