Marekani: Donald Trump ajeruhiwa kwa risasi akihutubia mkutano wa hadhara

Marekani: Donald Trump ajeruhiwa kwa risasi akihutubia mkutano wa hadhara

Trump : Risasi zinapigwa kalala chini fasta.

Viongozi wa Africa: risasi zikipigwa wanaanza kutoka nduki, unaanza kuwapa kazi vijana wa usalama kukukimbiza. walivyo na vitambi sasa inakua tabu tupu.
Acha dharura
 
Kushinda atashinda tu mbele ya puttin, hata huyu wa uingereza aliemshinda mhindi nnaamini kabisa ni mkono wa babu puttin
 
Sasa mkuu? Hio ndio fact?
Mic ilikuwa haijazimwa na sauti za hao secret service zilisikika kabisa wakimwambia twende, twende.
Trump akawaambia subiri nichukue viatu vyangu, kasema tena subiri, ndipo akaanza kunyoosha mikono, nadhani ilikuwa ni ishara kuwaonyesha wananchi ye ni mzima , yupo strong .

Lakini yote hayo yanafanyika ni kwa sababu tayari kuna secret service mmoja alisema pale jukwaani akisikika kwamba muuaji amemalizwa, nahisi ndicho kilimpa Trump nguvu ya kuamka na kuanza kunyoosha mikono, lakini kama haitoshi kuna secret service mmoja alikuwa akimkinga Trump kwa mikono kichwani kama uliona wakati wakishuka ngazi.
 
Urais ni taasisi hapo ndo panapoleta shida!
Trump ana misimamo yake ambayo taasisi nayo ina misimamo yake! Basi tabu tupu Trump anaonekana hafai mana sio Puppet
 
Mpo bize sana na nchi isiyowatambua, wao hawana time na sisi, marekani weusi wameuawa huko kwao ila mmpo tu nyuma yao kuwasapoti kwa maujinga yao.
Wewe umefuata nini kwenye huu uzi? mlioko TZ si ndo mlikuwa mnalilia unga wa ngano toka ukraine?je ukraine iliwatambua? kujua yanayotokea nchi nyingine ni muhimu sana.
 
Kingine why Trump afanye igizo wakati Biden hakubaliki? Hata Trump asipofanya kampeni kuna mtu mwenye akili timamu anaweza mchagua Biden?
Yaani Biden ana hali mbaya kiasi hiki ?.....basi Kamala Harris apeperushe bendera tu ili kuiokoa democrats....
 
Mbona lisu hamkumpa kura za huruma

USSR

Nyie Chawa wa Mama Samia wakati mwingine muwe mnaona hata aibu basi kupanua midomo yenu kusema au kuandika ujinga kama huu...

Kwani huyo baba yako Magufuli mwaka 2020 alishinda au alijitangaza kwa nguvu?

Alipigwa na Tundu Lissu kwa mbaaali sana kiasi cha kuona hata aibu kuweka wazi matokeo ya kura jimbo kwa jimbo kama sheria ya uchaguzi inavyotaka mpaka leo!!

Unataka ushahidi gani zaidi ya huu?
 
Nilikua simpendi Trump nikimuona kama mbaguzi sana.

Ila nilipomwelewa nikagundua huyu ni mimi mtupu, mtu flani asiependa Unafki

Mtu flani asie ogopa mtu, Raha sana ukiwa na Pesa na Unajiamini.
Hata mi naona Trump aendelee na urais, USA wengi wamekuwa vichaa ndio maana siku zinavyokwenda USA kiushawishi inashuka, yani watu wanataka kusikia upuuzi wa transgender na ushoga, mambo ya ajabu ajabu.

Yaani upuuzi umekuwa mwingi, Trump akiwaambia ukweli wanakuwa wakali, kwa mfano vita ya Ukraine na NATO ilikuwa haina umuhimu wowote, Trump akikaa pale ile vita inaisha.
 
Mimi nilishasema kwamba chama cha Democrat hakina tofauti kabisa na CCM!

Hao Democrats walianza na kujaribu kutaka kumwengua Trump kwenye baadhi ya majimbo. Hiyo ikashindikana.

Wakambambikia makesi kibao. Hiyo nayo haijaenda kama walivyotarajia.

Sasa wanatumia risasi. Kwa bahati nzuri, hiyo nayo haijafanikiwa.

Sasa nambie, hizo figisu zao zina tofauti gani na figisu za CCM?
ikatokea Trump akawa raisi, basi huku kwetu Lisu 2025,ccm wafungashe
 
FBI na CIA ni puppets WA deep state , unafikiri kwa nini walishindwa hata kudisclose kifo cha JFK mpaka leo ?
Sawa mchambuzi wa kibongo unayeijua Fbi na CIA kuliko wamarekani wenyewe

Ndo Raha ya kukaa bongo tunajiamini Sana tunaweza kuchambua habari yoyote na chochote hata KUTOKA white house
Tunaweza kubishana na mkuu CIA na Fbi na hatuambii Chochote tusichojua 😀😀😀😀

Welcome Fbi and CIA for more explanation of Trump attachment

47 people smart informer from Tz are here 😀 😀 😀 😀
 
Hao askari wapo makini sana, professional, skilled.

kuna yule muuaji Dar aliitwa Hamza, askari wa Tz walichokifanya pale kinatia huruma, yani muuaji huyu hapa na hapa jamaa wanamkosa risasi.
Sasa angalia hao secret service walivyofanya kazi chap sana, ingekua bongo hapo askari wangerusha mabomu ya machozi, mara field force wanaingia kuanza kutandika virungu watu, basi ingekua ni tafrani tu na muuaji anatokomea, mnaanza kupigwa search mlangoni ole wako ukutwe na kipisi cha bangi 🤣 utaelezea...
na yale maneno yao mara mtu asiyejulikana,oh mara uchunguzi unaendelea yaani taabu tupu
 
Back
Top Bottom