Marekani na China zafikia makubaliano ya kibiashara baada ya mvutano wa muda mrefu

Marekani na China zafikia makubaliano ya kibiashara baada ya mvutano wa muda mrefu

Hii imenikumbusha trade war ya 2018.
China sasa hivi imeshakua giant HUWEZI tumia sera za kupambana na Myanmar kiuchumi dhidi ya China.
Huyu huyu China ambaye baada ya hizi tarrifs, JinPing akaanza ziara za ushawishi kwa Malaysia, Vietnam na Cambodia!? Au kuna China mwingine!?
 
Anaelewa kiasi gani soko la Marekani lilivyo muhimu kwa mataifa husika.
Sasa Trump kafaidika nini alipoanzisha vita vya tariffs?

Mbona karudi kulekule kama ilivyokuwa kabla ya Marekani kuipandishia tariffs China

Trump alikuwa anapigana vita ambavyo alishahindwa
​
 
Huyu huyu China ambaye baada ya hizi tarrifs, JinPing akaanza ziara za ushawishi kwa Malaysia, Vietnam na Cambodia!? Au kuna China mwingine!?
Vijana hawa hawajui kitu na sasa nimeamua kuwavalia njuga *****
 
That's just politics kaka.
Ila kiuhalisia USA haipendi waislam.
Tizama nchi za kiislam zilivyoharibiwa.
Leo hii mataifa ya middle east yasingeingiliwa kisiasa basi yangekua yametulia na kusingekua na kelele za refugees.
Hiyo ni vita yao wenyewe ya madhehebu, kwa hiyo wenye akili wanaitumia kwa faida yao. Ushia na Usuni. Vita ya Panzi, kinguru lazima afaidike.
 
Huyu huyu China ambaye baada ya hizi tarrifs, JinPing akaanza ziara za ushawishi kwa Malaysia, Vietnam na Cambodia!? Au kuna China mwingine!?
Unafikiri China inaendeshwa kama nchi yako Tanganyika kwamba wanaendeshwa tu na mihemko.

Ziara za Vietnam,Malaysia,Cambodia,Russia zimetangazwa kabla hata ya upuuzi wa Trump
 
M
Kama ambavyo China haina kosa kuwekewa vikwazo vya kibiashara na USA, ndivyo ilivyo kwa Lissu

Kuna mtu anaogopa mwenzake kuwa mkubwa
Mama aliyeleta maendeleo nchi nzima matibabu bure, simba kapewa boeing 787 bure akazurure nalo huko duniani amuogope Lissu kwa lipi?
 
Wachina wa mchongo humu leo nimeamua kuwakabili ,kama wewe ni mchina kidume nikabili
 
Ikulu ya White House imetoa taarifa ikisema kuwa Marekani imetangaza makubaliano ya kibiashara na China baada ya mazungumzo kati ya ujumbe wa Marekani na China kufanyika nchini Uswisi siku ya Jumapili.

Hata hivyo, haijawa wazi mara moja kama makubaliano hayo yamefikiwa rasmi.

Waziri wa Fedha, Scott Bessent, alisema wamepiga hatua kubwa katika mazungumzo hayo na taarifa kamili itatolewa kesho. Aliongeza kuwa mazungumzo yalikuwa ya mafanikio na kwamba Rais Trump amepewa taarifa kamili.

Mwakilishi wa Biashara wa Marekani, Jamieson Greer, alisema mazungumzo ya siku mbili yalikuwa ya kujenga na walikubaliana kwa haraka, jambo linaloashiria kuwa tofauti kati yao hazikuwa kubwa kama ilivyodhaniwa.

Baada ya kutangaza hali ya dharura ya kitaifa, Rais Trump alipandisha ushuru wa bidhaa kutoka China hadi 145%. Greer alihitimisha kwa kusema wana imani kuwa makubaliano hayo yatachangia kutatua hali hiyo ya dharura.



China huwa hana tabia ya kupiga sana kelele.wao ni watekelezaji tuu.Marekani ni domo kaya
 
Back
Top Bottom