Marekani na Israel ni mataifa tofauti yenye baadhi ya siri za pamoja, bila kulijua hilo, Iran au yeyote dhidi yao, ni mfu atembeaye!

Marekani na Israel ni mataifa tofauti yenye baadhi ya siri za pamoja, bila kulijua hilo, Iran au yeyote dhidi yao, ni mfu atembeaye!

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Hili si suala la ushabiki wala kiimani. Uungwana siku zote ni kujitendea haki mwenyewe kwa kuukabili ukweli hata kama ni mchungu.

Sote ni wafu watarajiwa na kwa mola tutarejea. Hata ipo tofauti linapokuja suala la kurejeshwa na binadamu wengine, ndiyo maana kelele zinapigwa.

Rejea "Operation Plasma" ya MOSSAD kumhusu Mohamed al-Mabhouh kamanda wa HAMMAS, aliyeuwawa Dubai 19 January 2010:

The Dubai Operation: Mossad, Murderer & Mayhem in the Desert

Hiyo ni case moja yenye kufanana na nyingi za namna hiyo, zenye kuwahusisha Israel au Marekani.

Pattern ni hiyo hiyo kote, kila mmoja wa wawili hao akiguswa popote. Si vigumu kutambua iko kama sheria isiyo rasmi (rule of the thumb) kuwa:

"Ukimwua au kujaribu kumwua mwisrael au mmarekani au ukiyatishia mataifa yao au watu wao popote; tokea muda huo, tambua wewe ni mfu unayetembea, na watakuondoa."

Ya kwamba watakusaka pamoja kukuondoa wao duniani, bila kujali muda wala gharama. Ya kuwa kwenye hilo tangia mataifa yao yamekuwapo kwenye hilo hawajawahi kushindwa!

Yale yale ya akina Osama bin Laden, Mula Omari, General Farrah Aideed, Saddam Hussein, Muamar Gaddafi nk.

Angetoboa Haniyeh, Nasrallah au Sinwar? Watatoboa Ali Kamenei, yule wa Houthi, au nani?

Kwa sababu mataifa wawili hawa kwenye haya ya kutishiana nyau ni wamoja, ziko namna mbili tu za kushughulika nao kwa mafanikio:

1. Kusalimu amri kama UAE, Saudi Arabia nk yaishe kama unataka kuishi. Au:

2. Kupambana nao relentlessly bila pause ukafe mkipigana, kama ni nia yako japo kuwagawia nao maumivu ya kutosha kwa kadri iwezekanavyo.

Hili la pili ndipo alipokosea Hezbollah na ndipo anapokosea Iran kwani hawako tayari kusalimu amri. Ni wazi wamekuwa tayari kufa lakini wame "pause" na sasa cha mbwa koko kitawakuta.

Kwamba watapigwa surprise? Kwa hakika lile la aina ya "pagers na walkie talkies" si muda mrefu litawakuta Iran.

Kumbe kipi kipo salama nao chenye technolojia yoyote ya mmarekani? Ni TVs, computers, magari au gadgets zozote zenye chipsets zozote zenye lolote na wamarekani?

Kutowatokea wote wawili hawa bila kukoma (in hot pursuit) na kuwapelekea moto vilivyo sasa, yatamkuta Iran kama ya Hezbollah, asishangae hatakuwa na uwezo hata kurusha ngumi.

Alipoletewa moto rasmi Hezbollah, maelfu ya wapiganaji wake walikuwa tayari ni mahututi hosipitalini: vipofu, mikono hamna, miguu hamna, matumbo yamefumuliwa, nk.

Kwamba Hezbollah alianzishiwa vita rasmi, makamanda wote wakuu wakiwa marehemu na hawezi kutumia vifaa vyovyote vya mawasiliano.

Haihitaji macho ya kinabii kumwona Iran naye yulee ..., kama Hezbollah au kama kuku bandani akisubiria zamu yake ya kuchinjwa!

"Na huo ndiyo ulio ukweli mchungu ."
 
Kwa Iran hapana, sikubaliani na wewe!
Sioni namna Israel anaweza kuishinda Iran bila Tel Aviv kugeuzwa majivu.

Covert operations haziwezi kumpa ushindi dhidi ya Iran, zitampa tu ujiko machoni kwa wapuuzi.

Kwa Hezbollah na Palestine sawa, hapa nakubaliana na wewe, hawa shughuli yao imekwisha, anayefuatia ni Yemen.
 
Israel anapelekea moto mataifa matatu kwa mpigo
Kashamkalisha hamas wa palestina
Anashambulia wa Yemen na hezbollah
Na Iran yupo kwenye list.
Kama ambavyo USA hana uwezo wala uthubutu wa kuingia vitani na Russia, na Israel hana uwezo wala uthubutu wa kuingia vitani na Iran, anachoweza kufanya Israel ni covert operations kupitia MOSSAD, na hata hizo covert operations zake zikifanikiwa bado hatoweza kuchukua credit kuwa ni yeye amefanya.
 
Madhara ya kutohudhuria Masjid na kuacha kufanya swala ndiyo haya, unajikuta unaiona dunia katika uhalisia wake na kuuongea ukweli kama ulivyo ingawa ni mchungu.
 
Kwa Iran hapana, sikubaliani na wewe!
Sioni namna Israel anaweza kuishinda Iran bila Tel Aviv kugeuzwa majivu.

Covert operations haziwezi kumpa ushindi dhidi ya Iran, zitampa tu ujiko machoni kwa wapuuzi.

Kwa Hezbollah na Palestine sawa, hapa nakubaliana na wewe, hawa shughuli yao imekwisha, anayefuatia ni Yemen.
Mpaka sasa Israel bado ni Taifa lenye ngugu sana na hasa kiteknolojia, ogopa sana watu wako million 9 ambao ni wananchi pamoja na Jeshi humo humo lakini wana nguvu sawa na China,Russia,America pia,..Teknolojia kubwa za kivita na hata Satellite ni ujuzi wa kwao,japo Satellite iko America lakini wao ndo Controls.

Miaka kama 70 iliyopita kama sikosei,walivamiwa na majeshi matatu ya Syri,Jordan na Egypt na waliyashinda wakiwa watu laki 6 tu nchi nzima kwa maana ya Raia na Jeshi kwa ujumla

Tukirudi kwenye Imani kwa maana ya maandiko,ni kweli MUNGU aliwapa mapigo mawili makubwa iwapo wataenda kinyume naye, Magonjwa(Tauni) pamoja na kuwekwa mikononi mwa Adui,lakini wakirejea kwa MUNGU basi hakuna Taifa litaweza kuwashinda kivita,akili na uwezo wa juu wa kupambanua mambo.

Yote kwa yote vita vyao havituhusu,sisi ni watu wengine kabisa na maisha yetu
 
Hili si suala la ushabiki wala kiimani. Uungwana siku zote ni kujitendea haki mwenyewe kwa kuukabili ukweli hata kama ni mchungu.

Sote ni wafu watarajiwa na kwa mola tutarejea. Hata ipo tofauti linapokuja suala la kurejeshwa na binadamu wengine ndiyo maana kelele zinapigwa.

Rejea "Operation Plasma" ya MOSSAD kumhusu Mohamed al-Mabhouh jamanda wa HAMMAS, aliyeuwawa Dubai 19 January 2010:

The Dubai Operation: Mossad, Murderer & Mayhem in the Desert

Hiyo ni case moja yenye kufanana na nyingi za namna hiyo zenye kuwahusisha Israel au Marekani.

Pattern ni hiyo hiyo kote, kila mmoja wa wawili hao akiguswa popote. Si vigumu kutambua iko kama sheria isiyo rasmi (rule of the thumb) kuwa:

"Ukimwua au kujaribu kumwua mwisrael au mmarekani au ukiyatishia mataifa yao au watu wao popote; tokea muda huo, tambua wewe ni mfu unayetembea, na watakuondoa."

Ya kwamba watakusaka pamoja kukuondoa wao duniani bila kujali muda wala gharama. Ya kuwa kwenye hilo tangia mataifa yao yamekuwapo kwenye hilo hawajawahi kushindwa!

Yale yale ya akina Osama bin Laden, Mula Omari, General Farrah Aideed, Saddam Hussein, Muamar Gaddafi nk.

Angetoboa Haniyeh, Nasrallah au Sinwar? Watatoboa Ali Kamenei, yule wa Houthi, au nani?

Kwa sababu mataifa wawili hawa kwenye haya ya kutishiana nyau ni wamoja, ziko namna mbili tu za kushughulika nao kwa mafanikio:

1. Kusalimu amri kama UAE na Saudi Arabia yaishe kama unataka kuishi. Au:

2. Kupambana nao relentlessly bila pause ukafe mkipigana kama ni nia yako japo kuwagawia nao maumivu ya kutosha kwa kadri iwezekanavyo.

Hili la pili ndipo alipokosea Hezbollah na ndipo anapokosea Iran kwani hawako tayari kusalimu amri. Ni wazi wamekuwa tayari kufa lakini sasa wame pause na sasa cha mbwa koko kitawakuta.

Kwamba watapigwa surprise? Kwa hakika lile la aina ya "pagers na walkie talkies" si muda mrefu yatawakuta Iran.

Kumbe kipi kipo salama nao chenye technolojia yoyote ya mmarekani? Ni TVs, computers, magari au gadgets zozote zenye chipsets zozote zenye lolote na wamarekani?

Kutowatokea wote wawili bila kukoma (in hot pursuit) na kuwapelekea moto vilivyo sasa yatamkuta Iran kama ya Hezbollah asishangae hatakuwa na uwezo hata kurusha ngumi.

Alipoletewa moto rasmi Hezbollah, maelfu ya wapiganaji wake walikuwa mahututi hosipitalini vipofu, mikono hamna, miguu hamna, matumbo yamefumuliwa, nk.

Kwamba Hezbollah alianzishiwa vita rasmi Hezbollah, makamanda wote wakuu marehemu na hawezi kutumia vifaa vya mawasiliano.

Haihitaji macho ya kinabii kumwona Iran naye yulee ... kama Hezbollah kama kuku bandani akisubiria zamu yake ya kuchinjwa.

"Na huo ndiyo ulio ukweli mchungu .
Iran hatakufa kizembe. Anaondoka nao kama Samson
 
Kwa Iran hapana, sikubaliani na wewe!
Sioni namna Israel anaweza kuishinda Iran bila Tel Aviv kugeuzwa majivu.

Covert operations haziwezi kumpa ushindi dhidi ya Iran, zitampa tu ujiko machoni kwa wapuuzi.

Kwa Hezbollah na Palestine sawa, hapa nakubaliana na wewe, hawa shughuli yao imekwisha, anayefuatia ni Yemen.

1. Mkuu Sina hakika kama uliweza kunifahamu Aya ya kwanza pale kwenye mada:

"Hili si suala la kishabiki wala kidini."

Tuambiane ukweli kama watu wazima.

2. Zingatia hii si vita baina ya Irani na Israel tu. Kuna Marekani iliyokula yamini na Israel kwenye hili. Yamini hiyo ndiyo iliyogharimu Haniyeh, Nasrallah na wengine wote.

3. Iran atabondwa na Marekani kwenye mwamvuli wa yamini yao. Kabla ya kurusha lolote atakuwa amekuwa disabled.

4. Uliziangalia options 2 zile za namna ya kukabiliana na wawili hao?

Angalizo:

Binafsi nakerwa mno na maovu yao kwa wengine lakini je hata nisijiambie mwenyewe ukweli hata kama ni mchungu?
 
Kwa Iran hapana, sikubaliani na wewe!
Sioni namna Israel anaweza kuishinda Iran bila Tel Aviv kugeuzwa majivu.

Covert operations haziwezi kumpa ushindi dhidi ya Iran, zitampa tu ujiko machoni kwa wapuuzi.

Kwa Hezbollah na Palestine sawa, hapa nakubaliana na wewe, hawa shughuli yao imekwisha, anayefuatia ni Yemen.
Ungeuonyesha huo uwezo wa Iran kuigeuza Israel kuwa majivu angalau ungejitendea haki. Ni ndoto ya miongo mingi ya Iran kuifuta Israel, je ni kipi imekifanya hadi sasa ambacho kina angalau hizo dalili?
 
Iran hatakufa kizembe. Anaondoka nao kama Samson

Mkuu alikuwa nayo nafasi hiyo angekomaa sasa na kabla ya kushambuliwa.

Tatizo kubwa ametulia aguswe kwanza Ili ajibu.

Atajibu vipi pigo la kwanza likimweka kuwa marehemu au kiwete?

Tafadhali angalia options mbili zile; surrender au kufa nao. Kama ni kufa nao hakuna haja ya kuwasubili. Ni kuwafuata huko huko.
 
Mkuu naona akili zinaanza kukurudia mdogo mdogo umeandika ukweli mtupu japo najua ulikuwa unaandika huku umengata meno kwa uchungu kabisa

Tafuta popote au andiko langu lolote lililo nje ya common sense.

Si shabikii mtu wala dini kama ambavyo si bagazi mtu wala dini.

"Binafsi nakerwa mno na maovu yao kwa wengine["

HIvi hata hiyo "operation plasma" kwenye nada uliwahi kumsikia Ndugu?
 
Kwamba watapigwa surprise? Kwa hakika lile la aina ya "pagers na walkie talkies" si muda mrefu yatawakuta Iran.

Kumbe kipi kipo salama nao chenye technolojia yoyote ya mmarekani? Ni TVs, computers, magari au gadgets zozote zenye chipsets zozote zenye lolote na wamarekani?
Kwa Iran hapana, sikubaliani na wewe!Sioni namna Israel anaweza kuishinda Iran bila Tel Aviv kugeuzwa majivu.Covert operations haziwezi kumpa ushindi dhidi ya Iran, zitampa tu ujiko machoni kwa wapuuzi.
Nadhani hapa hukupasoma ukapaelewa,Israel anaweza akafanya uhuni kupitia hizi devices akajeruhi watu bila kujali siha zao kama ni wananchi wa kawaida au wanajeshi wakati taifa likiwa ktk taharuki ya tukio hili aka-attack vibaya Muajemi akagaragara mavumbini.

Vita ni mbinu na Zayuni kwa upande huu ameweza.
 
Israel anapelekea moto mataifa matatu kwa mpigo
Kashamkalisha hamas wa palestina
Anashambulia wa Yemen na hezbollah
Na Iran yupo kwenye list.

Kumbuka huyo si Israel peke yake bali na msiri wake Marekani waliokula yamini ya aina yake kuwahusu wote wa aina Hamas, Houthi na Hezbollah.

Iran yupo jwe list si ya Iran bali ya umoja wa Israel na Marekani.

Options:

1. Kusalimu amri kama UAE na Saudi Arabia yaishe kama unataka kuishi. Au:

2. Kupambana nao relentlessly bila pause ukafe mkipigana kama ni nia yako japo kuwagawia nao maumivu ya kutosha kwa kadri iwezekanavyo.

Kwa mujibu wa mada:

"Au wewe hudhani hivyo Ndugu?"
 
Nadhani hapa hukupasoma ukapaelewa,Israel anaweza akafanya uhuni kupitia hizi devices akajeruhi watu bila kujali siha zao kama ni wananchi wa kawaida au wanajeshi wakati taifa likiwa ktk taharuki ya tukio hili aka-attack vibaya Muajemi akagaragara mavumbini.

Vita ni mbinu na Zayuni kwa upande huu ameweza.

Uliziona options hizi:

1. Kusalimu amri kama UAE na Saudi Arabia yaishe kama unataka kuishi. Au:

2. Kupambana nao relentlessly bila pause ukafe mkipigana kama ni nia yako japo kuwagawia nao maumivu ya kutosha kwa kadri iwezekanavyo.

Sasa alipo Iran amedhihirika kuwa hayuko option #1.

Mbaya zaidi hayuko pia option #2, Kwa sababu ame pause anasubiri apigwe kwanza.

Vipi pigo kwenye pigo Hilo akifanywa marehemu au kiwete?

"Kwamba Hezbollah alianzishiwa vita rasmi Hezbollah, makamanda wote wakuu marehemu na hawezi kutumia vifaa vya mawasiliano."

Uliyaona hayo kwenye mada?
 
1. Mkuu Sina hakika kama uliweza kunifahamu Aya ya kwanza pale kwenye mada:

"Hili si suala la kishabiki wala kidini."

Tuambiane ukweli kama watu wazima.
Nimekuelewa.
2. Zingatia hii si vita bainw ya Irani na Israel tu. Kuna Marekani iliyokula yamini na Israel kwenye hili. Yamini hiyo ndiyo iliyogharimu Haniyeh, Nasrallah na wengine wote.
Haniyeh wa Hamas, Nasrallah wa Hezbollah. Hawa wote ni wadogo sana kulinganisha na Israel, tumekuwa tukiwasapoti kwa chuki zetu tu dhidi ya ubabe wa Israel na USA.

3. Iran atabondwa na Marekani kwenye mwamvuli wa yamini yao. Kabla ya kurusha lolote atakuwa amekuwa disabled.
Atabondwaje, unamaanisha kupitia covert operations za CIA na MOSSAD?
Ili tuelewane vyema naomba unielekeze anabondwaje!
Iran ameshalipua kambi za jeshi za Marekani hapo middle east na bado Marekani hakumbonda, kwanini iwe sasa? Alikuwa anasubiri waungane na Israel kumpiga kwa pamoja? Unamaanisha Marekani peke yake hamuwezi Iran? Au unamaanisha Marekani ana uchungu zaidi na Israel kuliko taifa lake?

4. Uliziangalia options 2 zile za namna ya kukabiliana na wawili hao?
Ndio, vita ni gharama mzee!
Kila taifa linajaribu kuepuka vita kadri inavyowezekana.
Binafsi nakerwa mno na maovu yao kwa wengine lakini je hata nisijiambie mwenyewe ukweli hata kama ni mchungu?
Wasiwasi wako tu mkongwe!
Shida ni kwamba uliwekeza matumaini makubwa sana kwa Hezbollah, hiki kichapo wanachokula Hezbollah kinakufanya ujiulize maswali mengi, ni kawaida.
Ila ni vyema kujua, mtindo uliotumika kumpiga Hezbollah na Hamas hauwezi kufanya kazi kwa Iran.
 
2. Kupambana nao relentlessly bila pause ukafe mkipigana kama ni nia yako japo kuwagawia nao maumivu ya kutosha kwa kadri iwezekanavyo.
Iran bado hajapata sababu ya kufanya hivi.
Au mkongwe unaona ipo sababu ya Iran kuingia kwenye vita moja kwa moja dhidi ya Israel?
 
Back
Top Bottom