Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 3,651
- 11,548
Deni la taifa la Marekani au kama wao wanavyoliita Federal Debt, Government Debt, National Debt, U.S Public Debt linapaa kwa kasi sana limefikia $35 trillion ambalo ni sawa na $104,082 kwa kila mtu anayeishi Marekani.
Deni la taifa la Marekani linakua kwa kasi zaidi kuliko uchumi.
Kuna sababu kadhaa zinazotajwa kuifanya serikali ya Marekani au unaweza kuiita the Federal Government ifikie hatua ya kukopa kutoka kwa wakopeshaji (creditors) wa ndani au wa nje ni kuongezeka matumizi ya serikali kuliko mapato yanayokusanywa.
Hii imepelekea Marekani iwe na ufinyu wa bajeti (deficit budget), bajeti ya serikali inapokuwa kubwa kuzidi mapato yake. Kwa mfano:

Mwaka wa fedha wa 2023 serikali ya Marekani ilitumia $6.13 trillion na kukusanya $4.44 trillion tu.
–The Fed
–The Fed
Mara ya mwisho Marekani kuwa na ziada ya bajeti (surplus budget) yaani matumizi ya serikali yanapokuwa chini ya mapato yanayokusanywa kupitia kodi, ilikuwa ni 2001.
Sehemu kubwa ya pesa ambazo Marekani inakusanya ili kufidia ufinyu wa gharama ni kwa kuuza bonds.
Kwa sasa kwa wastani Marekani inatengeneza deni la $1 trillion kila baada ya siku 100 au $10 billion kwa siku.