Hapana.
Hili ni tatizo la kifalsafa kati ya wale wenye mawazo ya kizamani kwamba hela zitaisha, au tutawarithisha madeni mengi vizazi vijavyo na wale wanaosema kuwa ukiwa una control ya pesa, hakuna tatizo hilo.
Ungemsoma Paul Krugman ungeona kuwa deni la Marekani hata kulipika linalipika kwa kuwa na kodi ndogo tu ambayo Wamarekani wanaweza kuilipa, tatizo ni siasa, Republicans hawataki kuongeza kodi.
Yani hao hao watu wanaojifanya hawataki deni, ukiwapa mpango wa kulipa deni kwa kuongeza kodi kidogo tu, hawataki kulipa kodi.
Tatizo la deni Marekani ni la kisiasa, si la kiuchumi.
Paul Krugman kaandika vizuri sana.
Tatizo Watanzania hamtaki kusoma.