Marekani: Ndani ya siku 100 tu deni la taifa la Marekani lafikia $35 trillion kutoka $34 trillion

Deni la taifa la Marekani, lililo katika dola za Kimarekani, wanazozi control na kuzichapisha Wamarekani, halina usawa na deni la taifa la nchi nyingine.

Kwa sababu wao ndio wana control na kuchapisha dola za Kimarekani.

Ni sawa na serikali ya Tanzania idaiwe katika shilingi za Kitanzania, hela ambazo ina uwezo wa kuzichapisha.

Kitu muhimu ni ku control inflation tu.
Kwanini basi wadaiwe wakati wangeweza kuchapisha Dollar pale wanapokuwa na uhitaji?
 
badala ya kuangalia nchi yenu inanuka madeni kila sehemu mnamwangalia tajiri anayewapa misaada kila kukicha,mijitu mingine bwana
 
Kwanini basi wadaiwe wakati wangeweza kuchapisha Dollar pale wanapokuwa na uhitaji?
Nimemalizia kwa kuandika "Kitu muhimu ni ku control inflation tu."

Kuchapisha sana dola kunaleta inflation, ongezeko la nei la kiujumla.

Kuna mengi zaidi ya juchapisha dola, nimeelezea kwenye posts zikizofuatiwa, soma article ya Paul Krugman nimeiweka hapa ime cover mengi zaidi kwa kina zaidi.
 
Deni la taifa la Marekani au kama wao wanavyoliita Federal Debt, Government Debt, National Debt, U.S Public Debt linapaa kwa kasi sana limefikia $35 trillion ambalo ni sawa na $104,082 kwa kila mtu anayeishi Marekani.​

View attachment 3067380
Deni la taifa la Marekani linakua kwa kasi zaidi kuliko uchumi.

Kuna sababu kadhaa zinazotajwa kuifanya serikali ya Marekani au unaweza kuiita the Federal Government ifikie hatua ya kukopa kutoka kwa wakopeshaji (creditors) wa ndani au wa nje ni kuongezeka matumizi ya serikali kuliko mapato yanayokusanywa.

Hii imepelekea Marekani iwe na ufinyu wa bajeti (deficit budget), bajeti ya serikali inapokuwa kubwa kuzidi mapato yake. Kwa mfano:

Mwaka wa fedha wa 2023 serikali ya Marekani ilitumia $6.13 trillion na kukusanya $4.44 trillion tu.
–The Fed

Mara ya mwisho Marekani kuwa na ziada ya bajeti (surplus budget) yaani matumizi ya serikali yanapokuwa chini ya mapato yanayokusanywa kupitia kodi, ilikuwa ni 2001.

Sehemu kubwa ya pesa ambazo Marekani inakusanya ili kufidia ufinyu wa gharama ni kwa kuuza bonds.

Kwa sasa kwa wastani Marekani inatengeneza deni la $1 trillion kila baada ya siku 100 au $10 billion kwa siku.
Machadema yatasema ni Mwigulu na Samia 😂😂
 
Deni la taifa la Marekani, lililo katika dola za Kimarekani, wanazozi control na kuzichapisha Wamarekani, halina usawa na deni la taifa la nchi nyingine.

Kwa sababu wao ndio wana control na kuchapisha dola za Kimarekani.

Ni sawa na serikali ya Tanzania idaiwe katika shilingi za Kitanzania, hela ambazo ina uwezo wa kuzichapisha.

Kitu muhimu ni ku control inflation tu.
Kama ni rahisi hivyo wangekuwa hawana deni kabisa maana wangechaoisha tuu 😂😂😂😂

Kwamba Kwa sababu tunachapisha Shilingi Kwa hiyo Nchi haiwezi Wala haitakiwi kuwa na deni la Shilingi si ndio? Akili za Machadema hizi ni mzigo 😆😆😆😆
 
US National debt imegawanyika sehemu mbili
  • Debt held by the public​
  • Intragovernmental debt​

Hapo kwenye debt held by public ndio kuna
  • Domestic holders of federal debt​
  • Foreign holders of federal debt​
Domestic holders of federal debt hawa ni creditors wa ndani kama mutual funds, commercial banks, pension funds, insurers, corporations na private investors.

Foreign holders of federal debt ni creditors wa nje hapa unazungumzia foreign central banks na foreign private investors walionunua bonds za Marekani. Ambapo kwa sasa mataifa yanayoshikilia sehemu kubwa ya deni la Marekani ni Japan na China wakifuatiwa na mataifa mengine
.

Intragovernmental debt ni deni la ndani ya serikali ya Marekani ambalo ni sehemu moja ya serikali inadaiwa na nyingine
Watanzania ni kama hamjielewi,yaani mnajua habari za deni la USA kuliko deni la Tanzania 😁😁
 
Kama ni rahisi hivyo wangekuwa hawana deni kabisa maana wangechaoisha tuu 😂😂😂😂

Kwamba Kwa sababu tunachapisha Shilingi Kwa hiyo Nchi haiwezi Wala haitakiwi kuwa na deni la Shilingi si ndio? Akili za Machadema hizi ni mzigo 😆😆😆😆
Jibu lako linaonesha huelewi uchumi.

Ungeelewa uchumi, ungeeleea nilishaangaliza kuwa si rahisi hivyo kwa kuandika "Kitu muhimu ni ku control inflation tu."

Kwa sababu ungeelewa uhusiano wa kuchapisha sana fedha na inflation.
 
Deni la Marekani liko kwenye mfumo wa bonds

Kwa hiyo unataka kumaanisha serikali za mataifa mengine ambao wananunua bonds za Marekani ni changa la macho?

Na investors wa ndani ya Marekani walionunua bonds nao wamepigwa changa la macho?

Mambo ya uchumi Kazi kwelikweli
Uchumi sio wa Kila mtu ila Kila mtu hujifanya anajua uchumi kisa ana duka la mangi na kampuni uchwara 😆😆

Hawajui kwamba debt management ni course ya semister nzima
 
Jibu lako linaonesha huelewi uchumi.

Ungeelewa uchumi, ungeeleea nilishaangaliza kuwa si rahisi hivyo kwa kuandika "Kitu muhimu ni ku control inflation tu."

Kwa sababu ungeelewa uhusiano wa kuchapisha sana fedha na inflation.
Inflation na deni wapi na wapi? Kama ishu ni kuchapisha,kwani lazima uchapishe harafu Uzi supply ndani ya Nchi? Si wangechaoisha wamlipe hata China ambae anashikilia Treasury bills na bonds zao nyingi tuu?

Hakuna kitu inaitwa kuchapisha hela ulipe deni,hujui kitu kwenye Uchumi.
 
Kwa hiyo dawa ni kuchapisha dollars sio?

Kwa hiyo the U.S Treasury na Federal Reserve waiamuru the Bureau of Engraving and Printing iprint notes walipe madeni?
Hawajui chochote kuhusu Uchumi hao nyumbu ila wanajifanya Wana maelezo meengi.

Uchumi sio formula za Force of Gravity
 
Inflation na deni wapi na wapi? Kama ishu ni kuchapisha,kwani lazima uchapishe harafu Uzi supply ndani ya Nchi? Si wangechaoisha wamlipe hata China ambae anashikilia Treasury bills na bonds zao nyingi tuu?

Hakuna kitu inaitwa kuchapisha hela ulipe deni,hujui kitu kwenye Uchumi.
Ukiongeza supply ya pesa kupita kiasi, bila kujali unaongeza ndani au nje, unasababisha thamani ya hiyo pesa ishuke.

Uki9ndoa suala tofauti la purchasing power parity, hakuna thamani ya dola ya ndani ya nchi na ya nje ya nchi. Yani ukiwa una trade forex, hakuna thamani ya dila ya ndani ya US na ya nje ya US. Thamani ni moja tu.

Pia, ukiongeza supply nje, huna jinsi ya kuzuia hiyo pesa isirudi ndani, kwa hivyo, unaweza kuwalioa Wachina, Wachina wakaja nazo US, zikashusha thamani ya dola dunia nzima.
 
Kumbe tunakubaliana kuwa deni halilipwi Kwa ku print Dola kama mlovyodai hapo awali si ndio?
 
Deni la taifa la Marekani au kama wao wanavyoliita Federal Debt, Government Debt, National Debt, U.S Public Debt linapaa kwa kasi sana limefikia $35 trillion ambalo ni sawa na $104,082 kwa kila mtu anayeishi Marekani.​

View attachment 3067380
Deni la taifa la Marekani linakua kwa kasi zaidi kuliko uchumi.

Kuna sababu kadhaa zinazotajwa kuifanya serikali ya Marekani au unaweza kuiita the Federal Government ifikie hatua ya kukopa kutoka kwa wakopeshaji (creditors) wa ndani au wa nje ni kuongezeka matumizi ya serikali kuliko mapato yanayokusanywa.

Hii imepelekea Marekani iwe na ufinyu wa bajeti (deficit budget), bajeti ya serikali inapokuwa kubwa kuzidi mapato yake. Kwa mfano:

Mwaka wa fedha wa 2023 serikali ya Marekani ilitumia $6.13 trillion na kukusanya $4.44 trillion tu.
–The Fed

Mara ya mwisho Marekani kuwa na ziada ya bajeti (surplus budget) yaani matumizi ya serikali yanapokuwa chini ya mapato yanayokusanywa kupitia kodi, ilikuwa ni 2001.

Sehemu kubwa ya pesa ambazo Marekani inakusanya ili kufidia ufinyu wa gharama ni kwa kuuza bonds.

Kwa sasa kwa wastani Marekani inatengeneza deni la $1 trillion kila baada ya siku 100 au $10 billion kwa siku.

Hilo deni kwa Marekani ni dogo sana huwezi hata kidogo kulinganisha na haya madeni ya nchi za Africa
Nikupe mfano rahisi:
1. Muuza kibanda mtaani mwenye mauzo ya shs 20,000 kwa siku, akienda kukopa milioni 10 litakuwa deni kubwa sana na sio rahisi kukubaliwa (ndio Africa)
2. Mfanya Biashara wa kawaida wa kariakoo mwenye mauzo ya shs Milioni 3 kwa siku akienda kukopa shs Milioni 100, anapewa haraka na kuombwa achukue zaidi (ndio marekani)

Ni kwa sababu Mfanya Biashara wa kibanda anaweza kulipa deni lake kwa zaidi ya miaka miwili tena kwa kujitesa na mfanya biashara wa kariakoo anaweza kulipa deni lake kubwa bila shida ndani ya miezi sita
 
Kumbe tunakubaliana kuwa deni halilipwi Kwa ku print Dola kama mlovyodai hapo awali si ndio?
Serikali ya Marekani, au entity yoyote inayokopa kwenye hela inayoweza kuchapisha (kama EU na Euro), ni vigumu kuwa na debt crisis.

Kwa sababu, ina uwezo wa kuchapisha pesa za kulipa deni.

Kitu muhimu ni kutochapisha pesa nyingi kwa mkupuo na kusababisha inflation.

Debt crisis is essentially a crisis of confidence. Mdai kutoamini kwamba atalipwa. Mdai akishaamini tu kwamba atalipwa, hakuna debt crisis.

Kuna an op-ed article ya Paul Krugman kaelezea Mario Draghi, gavana wa benki ya European Union, alivyomaliza debt crisis ya Eurozone kwa maneno matatu tu. Alisema "Whatever it takes". Kwa kumaanisha kuwa EU itafanya lolote lile kuhakikisha madeni yake yatalipwa.

Debt crisis ya EU ikaisha. Kwa sababu watu walijua kuwa Draghi ana control flow ya Euro.

Nimeweka article nzima ya Paul Krugman anaelezea hiki jambo.

Paul Krugman ni mchumi, Nobel laureate wa Economics wa mkwa 2008, muandishi wa The New York Times. Nimeiweka article hapa watu wajue mambo mengi ambayo sisi Watanxania wengi hatujui tujifunze.

Nasikitika watu wengi wanajibizana kwa uzoefu wao tu bika kupitia maneno ya wachumi wasomi.

Tatizo ni nini? Watu hawajui Kiingerwza? Hawapendi kusoma? Hawapendi kujielimisha? Makala haionekani?

Hii hapa.

Serikali ya Marekani, au entity yoyote inayokopa kwenye hela inayoweza kuchapisha (kama EU na Euro), ni vigumu kuwa na debt crisis.

Kwa sababu, ina uwezo wa kuchapisha pesa za kulipa deni.

Kitu muhimu ni kutochapisha pesa nyingi kwa mkupuo na kusababisha inflation.

Debt crisis is essentially a crisis of confidence. Mdai kutoamininkwamba atalipwa. Mdai akishaamini tu kwamba atalipwa, hakuna debt crisis.

Kuna aop-ed article ya Paul Krugman kaelezea Mario Draghi, gavana wa benkinya European Union, alivyomaliza debt crisis ya Eurozone kwa maneno matatu tu. Alisema "Whatever it takes". Kwa kumaanisha kuwa EU itafanya lolote lile kuhakikisha madeni yake yatalipwa.

Debt crisis ya EU ikaisha. Kwa sababu watu walijua kuwa Draghi ana control flow ya Euro.

Nimeweka article nzima ya Paul Krugman anaelezea hiki jambo.

Paul Krugman ni mchumi, Nobel laureate wa Economics wa mkwa 2008, muandishi wa The New York Times. Nimeiweka article hapa watu wajue mambo mengi ambayo sisi Watanxania wengi hatujui tujifunze.

Nasikitika watu wengi wanajibizana kwa uzoefu wao tu bika kupitia maneno ya wachumi wasomi.

Tatizo ni nini? Watu hawajui Kiingerwza? Hawapendi kusoma? Hawapendi kujielimisha? Makala haionekani?

Hii hapa.

Debt crisis ya US na Baadhi ya Nchi za Ulaya zinazotumika Euro zinatoka wapi kama wanaweza kuchapisha na kulipa madeni?
 
Debt crisis gani? Toa mfano.

Soma article ya Paul Krugman, anakueleza it is next to impossible kwa nchi inayokopa kwa hela yake kuwa na debt crisis. Kapitia historia kakuta mfano mmoja tu wa Ufaransa ambao ulikuwa na other very complex factors, an outliers.

Debt crises hizi zikitaka kuanza tu, mostly kwa ujinga wa mivutano ya kisiasa kama habari za "debt ceiling", gavana wa benki kuu akiwapa watu assurance tu kama Mario Draghi alivyosema "Whatever it takes", crisis inamalizika hapohapo.

Soma article ya Paul Krugman mkuu, itamaliza maswali mengi unayoniuliza.
 
Debt crisis gani? Toa mfano.

Soma article ya Paul Krugman, anakueleza it is next to impossible kwa nchi inayokopa kwa hela yake kuwa na debt crisis. Kapitia historia kakuta mfano mmoja tu wa Ufaransa ambao ulikuwa na other very complex factors, an outliers.

Debt crises zikitaka kuanza tu crisis, mostly kwa ujinga wa mivutano ya kisiasa kama habari za "debt ceiling", gavana wa benki kuu akiwapa watu assurance tu kama Mario Draghi akivyosema "Whatever it takes", crisis inamalizika hapohapo.

Soma article ya Paul Krugman mkuu, itamaliza maswali mengi unayoniuliza.
Mwaka Jana mwanzoni Marekani ilikumbwa na shida ya mzozo wa madeni Hadi wakaongeza debt ceiling,kitu ambacho kilisababisha upungufu wa Dola Duniani.

Unajisahaulisha? 😂😂
 
Debt ceiling is a political problem, not an economic problem.

Hakuna hata haja ya kuwa na debt ceiling, debt ceiling crises are something uniquely American katika chumi kubwa. Wamejiwekea wenyewe speed governor.

Ndiyo maana huwezi kusikia mzozo wa debt ceiling Uingereza au Japan.
 
Back
Top Bottom