Maria Sarungi: Hili la ahadi ya JWTZ kumtii Samia Suluhu sio la kawaida

Ok..lakini kwa kuwa cheo anapewa na raisi hivyo hivyo raisi akiamua anamvua,,sema huenda ikawa chanzo cha matatizo mengine.
Bwn barafu ya moto nimeshindwa kuelewa umeniquote kwenye comment isiyo yangu lkn jina langu rass jeff kapita .... limetokea kwenye hii comment.Tafadhali mods sijaelewa huu ni utaratibu gani.... comment no 91
 

wengine tunaangalia tatizo kwa upana,tunaonekana haters[emoji19][emoji19]

tumchukie kwa urembo ule ili iweje!!!
 
Hiyo kauli ya kuwa yy ndio rais hata marhum mzee pombe alikua anaisisitiza sana kipind cha mwanzo wa urais wake kila anapohutubia
 
Ni lini jeshi lilishatoa kauli ya kutomtii Rais mbele ya hadhara kiasi ambacho tuone ajabu CDF kusema atamtii Rais?

Ndicho kinachomshangaza mleta hoja hii ili kila mmoja aumize kichwa kutafakari what's behind the scene...

Katika kujibu hili, in my opinion maelezo ya member mwenzetu huyu Alexander The Great hapa chini yana make sense kwa zaidi ya 90%
 
Kuna watu wanadai walijinadi kwa pamoja kwa wapiga kura, lakini wanashindwa kutambua kwamba kipindi wanajinadi nafasi zao zilikuwa zimeaininshwa; kwamba mmoja atakuwa rais na mwingine atakuwa makamu.....ndo maana wengine wanapendekeza katiba ifanyiwe marekebisho ili hiyo nafasi ikaimiwe angalau kwa miezi mitatu kabla ya kuitisha uchaguzi mwingine...
 
"PENGINE" CDF Mabeyo nimepokea speech yake ndivyo-sivyo kwenye swala la lack of proffessionalism, na pengine ujumbe aliotaka kuufikisha kwa viongozi wa umma (Makatibu na Mawaziri)
Na mimi naamini hili pia.

Remember Mabeyo pamoja na kuwa well educated pia alikuwa head wa Military Intelligence, hii michezo atakuwa anaifahamu vizuri, na kama ni kweli kuna wapumbavu walikuwa wanataka kuleta ushenzi, hapa wote wamepata ujumbe wao bila kumtafuta mmoja mmoja.
 
Hayo ni mawazo ya huyo binti Sarungi.
Kwetu sisi watanzania wa kipato cha kawaida tunamuomba mama Samia atuondolee vikwazo kwenye njia zetu za kujitafutia mkate wetu wa kila siku.
Good message, kumbe sometimes huwa una akili?
 
Mama anatakiwa awe makini sana.
Kuna team pandikizi ambayo huenda haija amini kwamba huyu ndie Rais wetu. Bado wana tafuta jinsi ya kumkwamisha.
Ushauri wangu wa bure, Mama awaondoe wote alio na mshaka nao. Aunde safu yake itakayo mtii na kumheshimu.. Walamba vitu vya ukanda wapewe mapumziko kidogo hadi wata kapo jua SSH ndie Rais wa sita wa Tanzania.
 
aanze na Bashiru,hata leo
 
Kikatiba hiyo nafasi aliyopo samia ni nafasi ya mtoto wa mzee ally hassan mwinyi kule zanzibar.

Kumbuka katiba na sheria za muungano zinaweka bayana kuwa makamo wa rais wa serikali ya jamhuri ya muungano ndie mkubwa wa serikali upande wa Tanzania visiwani......


Sasa sijui huu utaratibu tuliukorogaje hapo katikati na kuwa na makamo wawili yaani makamo bara na yule ambaye anapewa jina la raisi wa zanzibar badala ya makamo wa jamuhuri muungano.....
 
Sio rahsi kufanya hvo Kwa mkuu wa jeshi , Raisi ana nguvu hyo Ila sio rahsi , mkuu waajeshi ni mtu delicate Sana , Maghufuli mwenyewe alimwacha Mwamnyange mpak akastaaf ,na bado akamuongezea mwaka mmoja .....
 
Mabonta hawajajua kutofautisha witches and wizard ndio tatizo kifupi hapo ni jinsia ndio inasumbua tu basi hakuna jingine
 
Acha kutulisha matango pori wewe
 
Wewe ni muongo! Magufuli anaingia madarakani Mabeyo alikuwa Chief of Staff, yaani alikuwa namba mbili kutoka kwa Mwamunyange ambaye alikuwa CDF. Hivyo hakuna waliopanguliwa kumpisha Mabeyo bali alipandishwa cheo mara baada ya Mwamunyange kustaafu.
 
jikite kwenye usomaji,kuna michango mizito ya wakuu walokuzidi upeo
Hoja zipi alizoleta huyu dada?

Yani mkuu wa majeshi kusema tutatii amri zako kama amiri jeshi mkuu na kufanya kazi zao kwa mujibu wa katiba yeye anaona ni ajabu? Au alitaka asemeje? Aseme hawatamtii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…