Maridhiano ya CCM na CHADEMA Ndiyo Kawaida ya Vyama vya Siasa Duniani Ilivyo?

Wewe mtoa mada kwani ni lazima kila siku sisi ndo tuwe watu wa kuiga, kwani na hao unaowasema hawawezi kuja kuiga huku?.Nadhani ifike wakati na sisi tujione kiwa tunaweza kifanya jambo letu na likaigwa na tuondokane na hizo fikra za kitumwa.
'Of course' hatuwezi kuwa "waigaji" siku zote, sasa niambie tuanze kuhimiza waje waige nini, kutekana, kuvunja sheria tunazotunga sisi wenyewe, n.k..?
 
Kinachoendelea ni wanasiasa kuungana kuwakandamiza wananchi.

Tukatae huu usanii unaoendelea maana sisi ndio tunaopoteza zaidi.

Kwani hakuna wa kuzungumzia hali ngumu za wananchi katika mazingira haya ambayo wote ni kitu kimoja.
ACHA chuki,, Mama ni Rais
 

CHADEMA sivyo unavyodhani. Risasi zilishindwa sembuse maridhiano ambayo muda wowote tunaweza jitoa.
 
Maridhiano imekuwa nongwa. Mnataka siasa za watu wasiojulikana
Duh!

Ni wapi umesoma nikihimiza hayo mkuu?
Kwani hatuwezi kufanya siasa bila huko kutekana na mambo mengine yasiyofaa?

Kwa hiyo kwa mtizamo wako ni kwamba "maridhiano" kazi yake kubwa ni kuondoa tu hao watu "wasiojulikana"?

Kwani hakuna mambo mengi makubwa zaidi ya hilo?
 
CHADEMA sivyo unavyodhani. Risasi zilishindwa sembuse maridhiano ambayo muda wowote tunaweza jitoa.
Ninakusikiliza wewe mkuu, lakini dalili zote zinaonyesha CHADEMA iliyohimiri zile "risasi" haipo tena; ishateketezwa na njia mbadala ambazo hazikuhitaji matumizi ya risasi.

Kuna watu mafundi sana wa mambo haya, kwa hiyo usije ukashangaa ukiona mwisho wa siku ile CHADEMA uliyokuwa ukiifahamu haipo tena.
 

Naona ni Kama una wasiwasi na mrengo wa Chadema ndio nikauliza ulitaka CHADEMA wafanyeje. Mama mwenyewe kasema anapata Upinzani huko CCM hata kuruhusu mikutano ilikuwa kazi. Ina maana CHADEMA wangekaza na CCM pamoja na serikali wangekaza na mwisho wa siku unajua kingetokea Nini.
 

CHADEMA hunadilika na mazingira. Kumbuka watu wengi waliihama CHADEMA wakati wa shida kuanzia Viongozi, wabunge mpaka wanachama wa kawaida. Maana ilikuwa dhambi kujihusisha na CHADEMA. Ila leo, Rais wa nchi na TBC wanaipa airtime BAWACHA kwenye mkutano wao.
 
Sioni jinsi gani "Mama angekaza", na zaidi ya hayo, usinifanye nionekane kana kwamba ninapinga hayo "maridhiano".
Nilicho wasiwasi nacho ni matokeo ya hayo "maridhiano" yanayoonekana kuimaliza CHADEMA.
 
Sawa Kabisa.

Sasa swali ni hilo la CHADEMA kwenda tena kuungana na watu hao, badala ya kukaza nati ili nasi tuondokane na hiyo hali mbovu.
Ni kipi kinachowaingiza CHADEMA kwenye mtego wa kwenda kuendeleza hayo maovu?
Anzisha chama chako ili ukaze hizo nati mkuu
 
Dah!

Ni vigumu kabisa, actually haiwezekani kulikataa hili. CHADEMA imepitia mengi sana makubwa, na ndiyo maana Mbowe kajijengea heshima kubwa aliyonayo.
Sasa inawezekana tukasema "kakwaa kisiki" pengine bila kujuwa, au kwa maksudi maalum.
 
Hata utawala wa makaburu Africa Kusini uliisha kwa mazungumzo na maridhiano, CCM hata hawajafikia kiwango cha makaburu. Mandela na ANC walikaa mezani na makaburu, hiyo kwa wengine walitafsiri ni kuungana.
Sawa Kabisa.

Sasa swali ni hilo la CHADEMA kwenda tena kuungana na watu hao, badala ya kukaza nati ili nasi tuondokane na hiyo hali mbovu.
Ni kipi kinachowaingiza CHADEMA kwenye mtego wa kwenda kuendeleza hayo maovu?
 
Sioni jinsi gani "Mama angekaza", na zaidi ya hayo, usinifanye nionekane kana kwamba ninapinga hayo "maridhiano".
Nilicho wasiwasi nacho ni matokeo ya hayo "maridhiano" yanayoonekana kuimaliza CHADEMA.
Vyama vya siasa vikimalizwa kwa siasa za mazungumzo na maridhiano ni sawa kabisa na hiyo ni sehemu ya demokrasia, ila sio kwa hofu na vitisho vya risasi, utekaji, unyang'anyi na njia nyingine haramu za binadamu wasiostaarabika.
 
Tungekuwa na ubunifu wa kiasi hicho unachokifikiri wewe hapa tungekuwa mbali sana kama nchi kimaendeleo.

Lakini najua uliyoandika hapa ni kama unajazia nafasi tu.
Wewe mkuu unaona CCM iko sawa kama ilivyo kimkakati ila CHADEMA ndio inatakiwa “ikaze” kutoruhusu dhulma na udhalimu inaotendewa na CCM (irrespective of the president in office). Sawa?

CCM bado inamiliki na kudhibiti vyombo vya dola. Watanzania hawana ujasiri wa kusimama na upinzani dhidi ya vipigo, mateso na manyanyaso ya vyombo vya dola kama ilivyokuwa katika awamu ya tano. Hawako tayari kuvuja damu kama kina Mawazo, Lissu na wengineo.

Na madhila aina hiyo toka vyombo vya dola hayapo katika nchi za kidemokrasia zilizoendelea.

Sasa ukitaka CHADEMA wakaze tu wasikubali muafaka wa aina yoyote na SERIKALI - not CCM by the way (kama mkakati wa kuendelea na siasa) maana yake, katika mazingira haya, unataka CHADEMA waachane na siasa au wajigeuze kuwa TLP and the likes. Yaani wawe completely ineffectual as a political force kama alivyotaka JPM. NDIVYO NILIVYOKUELEWA! Just be honest.
 
Kwa hili niwapongeze sana CHADEMA.. Nisiwe na maneno mengi muda utasema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…