Shati jeupe kaanza kurusha ngumi. Amemrushia ngumi shati la maua wakati wakiwa hawatazamani, shati jeupe akiwa nyuma ya shati la maua.
Akampiga ngumi ya kisogo.
Shati jeupe alipogeukiwa na shati la maua akakoki bastola. Shati la maua akarusha ngumi ya kilevi (kwakua alikua kalewa ndiyo maana hakuiona bastola au hakujali, mi nahisi hakuiona) shati jeupe easily akakwepa, akajibu kwa low kick ambayo ikampeleka jamaa chini.
Shati jeupe anakoki tena bastola. Anainyoosha kwa shati la maua, shati la maua anakinga mkono halafu anaudaka mguu (nafikiri hapa sasa ndiyo akajua jamaa katoa bastola) kisha shati la maua anaanza kutokwa damu.
Hapa najiuliza hajapigwa risasi? Mbona hayo mateke hayatoshi kukutoa damu kiasi hicho na ukawa disoriented mpaka ukalala chini kabisa. Ama tuseme mwili wako hauwezi kuchukua adhabu.
Huyu jamaa na porn yake, boss wa klabu. Anajua kua kamera zipo, kisha akaamua amle mtu humo humo?
Visa vya watu wenye hela vinafurahisha. Ila shati jeupe ndiye kaanzisha ugomvi kwa hapa, haiwezekani kusema alikua anajitetea.