kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
DW na BBC walituletea kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu vurugu za October 29 zitokee. Binafsi sikuupenda upuuzi ule hasa kwa kipindi hiki ambacho taifa linajitahidi kurejea katika hali ya kawaida.
DW na BBC hawakutaka kuhoji hata mtu mmoja aliyekatwa kidole, kupoteza mali zake kwenye zoezi lile la mapinduzi au hata kuihoji serikali inafanya nini kurudisha huduma zilizovurugwa na zoezi lile la kuipindua serikali lililoshindwa.
BBC na DW watuambie kama ulaya kuna kikundi kilichowahi kuzuia uchaguzi wa nchi husika na nini kilitokea.
Nawaomba DW na BBC wawe wanatuletea kila mwaka kumbukumbu ya tukio la Hitler kuwaua wayahudi kwenye makambi ya mateso huko Ujerumani ili vizazi ambavyo havikuwepo vijue. Pia watuletee kumbukumbu za mauaji ya Nagasaki na Hiroshima kila mwaka kwasababu hizohizo za kuwajulisha watu siku hiyo.
Ni vyombo vya kichochezi ambavyo vina sifa ya kupigwa marufuku kupeperusha matangazo yake nchini.