Masoud Kipanya: Jeshi la Polisi liwe fair kwa watu wote bila kujali itikadi zao za kisiasa

Masoud Kipanya: Jeshi la Polisi liwe fair kwa watu wote bila kujali itikadi zao za kisiasa

Mimi pia sipendi uonevu lakini katika hali hii ya ukandamizaji wa vyombo vya habari, habari yako imeandikwa kichonganishi. Clouds ama wanaweza kuzuia watu wao wasitoe kauli kama hizi ama wanaweza adhibiwa na mfumo wa ki-dikteta. Tufikishe ujumbe wetu bila kuweka wengine katika mazingira magumu.
Kwa Mara ya kwanza Leo Masoud Kipanya ameanzisha mjadala wenye heshima kwa Radio Clouds.

Ameanzisha mada ya kumuonya IGP Sirro baada ya magazeti kum-quote akionya wanasiasa kwa kauli ziwezavyo kuchafua amani.
Wamemhoji mbona kuna mtu kila siku anajirekodi na kurusha habari za uchochezi akiwa kavaa vikaunda suti vyake na hachukui hatua?

Jee hamuoni? Inakuwaje IGP anakuwa na tabia ya uongo hadharani ili kulinda double standard zake katika nchi.

Amekumbushwa kuwa mtu huyo anaye jirekodi na kurusha mitandaoni anatumwa na nani hadi yeye Sirro hamuoni akitukana watu tena wengine viongozi kabisa?

Jee ninani huyo anayetuhumiwa kuharibu amani lakini IGP hamuoni?
 
CCM na serikali yao wanajiharibia kila ukicha naona wanakotaka kuipeleka nchi sio kuzuri.
 
Siku CCM ikiachia madaraka, hiki chama kitakufa kama KANU, kinabebwa kila siku
 
Kwa kweli hata mimi nilimsikia Sorro akiongea kwa msisitizo utafikiri anamwonya mtu fulani upinzani.
Lakini huyu kunguni nguoni, anayetukana watu kila siku, wala hachukuliwi hatua wala kuonywa.
 
Msiba aliwatuhumu hadi Marais wastaafu kwamba ni wala mlungura...lakini hajawahi kuguswa!! Kwa kweli hili ni doa kubwa sana kwa gesi retu hiri ra porice...
 
Haiwezekani IGP atetee jinai za Musiba, Sirro ni Msomi na muumini mzuri hawezi tenda ujinga wa kitoto vile
Anashindwa hata kukemea magazeti kama haya?
fichuatanzania_-___CDyLSqCMqqb___-.jpg
 
Haiwezekani IGP atetee jinai za Musiba, Sirro ni Msomi na muumini mzuri hawezi tenda ujinga wa kitoto vile

..Umesikiliza mahojiano ya IGP ktk kipindi cha dk45 cha ITV?

..Alitumia muda mrefu sana kuwatisha wagombea wa vyama vya upinzani.

..Na kwa maoni yangu alikuwa amewalenga Chadema na Act.

..Na jambo lingine baya alilofanya ni kusema wapelelezi wa Polisi wamekuwa wakimfuatilia TL lakini hawampati.

..Yaani IGP ameanza kumtangaza TL kana kwamba ni mhalifu anayefuatiliwa na kunyatiwa na wapelelezi lakini amekuwa akiwachomoka.
 
Huyo Masudi baada ya kuona michoro yake Haina impact Basi kaamua kutumia kipindi ku preach hate.
wew sio mzima ndio maana unajiita stroke.. hampendi ukweli nyie
 
Namimi nikimsikiliza, nikabaki kimnya tu,kwamahli alipo na hoja hiyo sidhani Kama yupo sahihi
 
Back
Top Bottom