Maswali kuhusu matumizi ya stendi mpya ya mabasi Mbezi (so-called Magufuli)



Mkuu hebu fikiria watu wenye hali duni, sio kila mtu ana uwezo wa kugharamia nauli ya mlolongo wote huo wa kupanda daladala mbili au tatu kabla hajafika bus terminal,

Tuache kufanya biashara kwenye roho za watanzania, matatizo ya watanzania msigeuze mtaji wa kujitajirisha, kazi ya serikali ni kuweka mazingira mazuri ya kurahisha maisha ya wananchi wake na sio kuwaongezea mizigo yao!

Nashindwa kuelewa ile slogan ya "serikali ya wanyonge!"
 


Kweli mkuu, itabidi watu waongeze na gharama za kulala lodge kama hawataki kuchelewa usafiri wa alfajiri. Kweli kufa kufaana.

Na gharama za usafiri zitazidi kuwa juu sana na kupandisha gharama za maisha kwa watanzania wanyonge ambao hadi sasa tayari wanalia hali ngumu ya uchumi.

Ngoja tuone mkuu labda huenda walioshika mpini watasikia kilio cha watanzania wanyonge.
 
Ndio mkuu kupanga ni kuchagua
 
yapo sahihi, sisi tuna mazoea mabaya tu. Yani ndege inayoenda Musoma ikaanzie safari Tegeta kwakua Nyuki kuna Wakurya wengi na wanasafiri kwa wakati mmoja. Kwa wenzetu walioendelea haya hayapo. Boda boda na taksi watapata wapi hela ya kula? Mimi natokea Bunju kila safari lazima nipande boda inipeleke Ubungo ndo nipande basi kwenda ninapoenda. Au daladala mpaka Mwenge, halafu mpaka mawasiliano. Binadamu hatuna jema, watu tunataka Terminal ije milangoni kwetu. Mji ndo unatanuka hivyo.
 
Kulikuwa hakuna foleni kama sasa, it was easy to move from one point to another... sasa na hizi foleni mabasi yote yanayoingia Dar yaje Mbezi, foleni zitakuwa balaa! Nawza kitu kama hicho....
Ilo li barabara la mbezi to kibaha sijui kama umeliona
 
Kuna njia pale kibamba ccm nasikia ina pigwa mkeka inatokea tgt sijui bunju, ila kama ujuavyo makampuni mengi ya mabasi yamefungua ofisi zao so usiwe na wasi wasi, kama zaman stand ilikuwa kisutu na watu walikuwa wanatoka mbagala hadi kisutu
Nadhani ni mbezi high to machimbo to mpigi magoe to bunju via pande. Inapigwa mkeka ile aliongelea mtemvu pale akimuomba raisi.
 
Hivi mtu wa mbezi luis, tegeta, kibaha, bunju ilikua akitaka kwenda mtwara ni mpaka aje mbagala?
 
Hivi mtu wa mbezi luis, tegeta, kibaha, bunju ilikua akitaka kwenda mtwara ni mpaka aje mbagala?
Hapana mkuu MUNDENDE kuna mabasi kutoka Tanga , morogoro yanayoenda mtwara wanapanda hayo!

pia ubungo terminal mabasi ya kusini yalikuwepo mengi tu.
 
Sawa
 
Nadhani ni mbezi high to machimbo to mpigi magoe to bunju via pande. Inapigwa mkeka ile aliongelea mtemvu pale akimuomba raisi.
Zile ni siasa tu mbona hata mnyika alikuwa anapigia kelele sanaa, lkn ndio barabara hiyo bila shaka
 

Wewe kwa hakili zako unadhani wakati stend ipo ubungo unadhani abiria wte walikuwa wanakaa ubungo.
Au kwa hakiri yko unadhani abiria wte wanaosafiri kwenda mtwara wte wanakaa mbagara au temeke? Kadharika wa arusha wte wanakaa tegeta au huko unako lalamikia?? Lazima tuwe na fist point moja.

Hayo mengine sasa nisisi abiria na wasafirishaji ndo watazidiana ujanja wakuwa na ofice za ziada km leo ilivyo hapo urafiki kamata. Na kariakoo.
 

Uelewa wako tu kaka ni mdogo. Ila tumekuelewesha nadhani umeelewa et
 
Mbona stesheni ya reli ipo moja Dar na wote hupandia pale haijalishi unakaa mbezi, Bunju, kimara, mbagala au kigamboni
Tunapoongea maswala kama haya tuwe tunaangalia na muda jamani! Kumbuka hizo treni huwa zinaondoka mchana au jioni ilihali mabasi mengi yanaondoka alfajiri au asubuhi!

Sasa mtu anayetoka Mbagala sijui Chamazi au Kisemvule and co itamchukua muda gani hadi aje afike hapo Mbezi? Na unafikiri usafiri wa kutoka kule hadi hapo ni rahisi kihivyo?
 
Hiyo haina shida. Mradi waruhusiwe kupakia na kushusha abiria kwa vituo vyao mwisho wa siku.
Otherwise kituo kitakua ni mateso kwa watokeao Kongowe ya Mbagala, Kigamboni na maeneo yale, kwa sababu watalazimika kulala stendi ili kuwahi mabasi yaendayo njia za Morogoro na Bagamoyo.
 
Wananchi wa Dar, mtavurugwa hadi mtapata akili. Hadi mtambue kuwa box la kura Lina dhamani gani
 
Hako kautaratibu kapo mikoa yote iliyijenga stendi Mpya. Kuna siku Nimeenda Iringa nako ni hivyo hivyo. Basi linaendana mjini na lina ofisi kubwa tu, lakini haliruhusiwi kwenda na abiria,mnashuka nje ya mji then mnapanda dalala.
Akili zetu watanzania huwa si za ku solve tatizo
 
You have logic
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…