Maswali kuhusu matumizi ya stendi mpya ya mabasi Mbezi (so-called Magufuli)

Mkuu acheni kulialia watanzania sijui tukoje.

Hizo changamoto zigeuze fursa. Kama unaona watu watapata tabu kwenda Mbezi luisi kwa usafiri wa asubuhi anzisha usafiri wa kuwapeleka wateja stand hata na kigari kidogo kila asubuhi.

Mbona tunachezea fursa hivyo. Shida yako ni fursa kwa wengine. Kuna watu wanataka uumwe ili wapate hela. Ningetamani uombe stand ipelekwe nje ya mji kabisa ili uchangamkie fursa.

Jitahidi kila kitu uwe unakirafsiri kwa Jicho la kifursa utaona Kuna sehemu nyingi hela tunazipotezea.

Mkuu hebu fikiria watu wenye hali duni, sio kila mtu ana uwezo wa kugharamia nauli ya mlolongo wote huo wa kupanda daladala mbili au tatu kabla hajafika bus terminal,

Tuache kufanya biashara kwenye roho za watanzania, matatizo ya watanzania msigeuze mtaji wa kujitajirisha, kazi ya serikali ni kuweka mazingira mazuri ya kurahisha maisha ya wananchi wake na sio kuwaongezea mizigo yao!

Nashindwa kuelewa ile slogan ya "serikali ya wanyonge!"
 
Naona watu wanachangamkia fursa kwa kujenga lodge pembeni mwa kituo, kuna mtu pale jirani amepiga kitu cha vyumba 16!kuwasaidia watu wanaotoka mbali akina Mbande ,Vikindu na wenzao, kwakweli kufa kufaana.
Anyway watu wa mbali itawa cost sana mfano Nauli ya kwenda Tanga ni 20,000/= itabidi utenge 20,000/= nyingine ya lodge na 10,000/= ya kula km una mpango wa kusafiri mapema unless umepanga kusafiri mchana.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app

Kweli mkuu, itabidi watu waongeze na gharama za kulala lodge kama hawataki kuchelewa usafiri wa alfajiri. Kweli kufa kufaana.

Na gharama za usafiri zitazidi kuwa juu sana na kupandisha gharama za maisha kwa watanzania wanyonge ambao hadi sasa tayari wanalia hali ngumu ya uchumi.

Ngoja tuone mkuu labda huenda walioshika mpini watasikia kilio cha watanzania wanyonge.
 
Lengo la usafiri wa umma ni kuwasiaidia watu kurahisisha safari zao, lakini inapoweka mazingira kuwa magumu zaidi hapo hauwasaidii bali unawaumiza!

Unajua umbali uliopo kutoka mbagala mpaka mbezi Luis?! Hapo sijagusia ndani zaidi kama charambe, matitu, chamazi, mbande, kisewe, msongola, mvuti na chanika?!

Unajua umbali uliopo kutoka kongowe, kibada , mjimwema, kigamboni, mpaka mbezi Luis?!

Unajua umbali uliopo kutoka mwandege, kisemvule mpaka mbezi Luis?!

Kote huko hakuna basi la moja kwa moja mpaka mbezi stendi kuu, lazima upande madaladala mawili au matatu kufika mbezi bus terminal,

Hapo abiria anakwenda either moshi, arusha, tabora, singida, shinyanga, mwanza ,kigoma au kagera! Aamke saa tisa usiku kuwahi daladala kutoka kisemvule, asubiri ijae, bado hujagusia foleni, ashuke kariakoo au tandika, achukue daladala nyingine hadi mbezi , mtu huyu ana watoto na mizigo tele!

Hapo utakuwa umemsaidia urahisi wa safari yake au umemtwika mateso zaidi?! Serikali iliangalie hii upya kwa jicho la tatu. Wengi tulikuwa tunategemea urahisi wa kupandia stendi ndogo na ofisi ndogo za mabasi husika ya mikoani.
Ndio mkuu kupanga ni kuchagua
 
Kuna tatizo hapo imagine unashuka saa sita usiku na daladala hakuna na una mizigo mingi mikubwa!!!
Wenye mabasi kushusha ofisi zao ilikuwa ni huduma nzuri ya kumsaidia abiria

Kinachotakiwa kitamkwe ni kuwa basi zote zipitie stendi kuu kuanzia safari au kumaliza safari ziwe na abiria au la lazima zipitie ila kusema marufuku kuwa na abiria haliko sawa

Pili kuua hivyo vituo vingine vilivyokuwepo ni kuua ajira za mamia ya watu waliokuwa wakipata riziki zao kupitia hizo stendi ndogo kuanzia maduka teksi bodaboda bajaj wabeba mizigo mama lishe nk zingeachwa tu kama sehemu ya Transit kama ilivyo ndege tu kuwa stendi kuu ubungo stendi ndogo temeke Au mbagala au tegeta au kariakoo au ofisi juu ya basi nk ili kuondoa usumbufu kwa abiria .Sipati picha mtu anaishi mbagala anaenda mtwara aende mbezi kupandia gari kule wakati mfano mwenye gari ana ofisi kuu hapo hapo mbagala na basi linaanzia hapo kwenda mbezi kubeba abiria!!!!

Chukulia mfano basi zima wamekata tiketi watani zangu wamakonde wanaoishi mbagala wanaenda kwao basi linaanzia hapo hapo mbagala ofisi kuu ya basi .Kwa hiyo hao makonde wanatakiwa wapande daladala kwenda mbezi na hilo basi liende tupu hadi mbezi lipakie hao makonde kwenda nao mtwara!!! ni kituko badi watakalopanda liko mbeke yao tupu na wao wako kwenye daladala kwenda mbezi

Haya maamuzi mengine hayako sahihi
yapo sahihi, sisi tuna mazoea mabaya tu. Yani ndege inayoenda Musoma ikaanzie safari Tegeta kwakua Nyuki kuna Wakurya wengi na wanasafiri kwa wakati mmoja. Kwa wenzetu walioendelea haya hayapo. Boda boda na taksi watapata wapi hela ya kula? Mimi natokea Bunju kila safari lazima nipande boda inipeleke Ubungo ndo nipande basi kwenda ninapoenda. Au daladala mpaka Mwenge, halafu mpaka mawasiliano. Binadamu hatuna jema, watu tunataka Terminal ije milangoni kwetu. Mji ndo unatanuka hivyo.
 
Kulikuwa hakuna foleni kama sasa, it was easy to move from one point to another... sasa na hizi foleni mabasi yote yanayoingia Dar yaje Mbezi, foleni zitakuwa balaa! Nawza kitu kama hicho....
Ilo li barabara la mbezi to kibaha sijui kama umeliona
 
Kuna njia pale kibamba ccm nasikia ina pigwa mkeka inatokea tgt sijui bunju, ila kama ujuavyo makampuni mengi ya mabasi yamefungua ofisi zao so usiwe na wasi wasi, kama zaman stand ilikuwa kisutu na watu walikuwa wanatoka mbagala hadi kisutu
Nadhani ni mbezi high to machimbo to mpigi magoe to bunju via pande. Inapigwa mkeka ile aliongelea mtemvu pale akimuomba raisi.
 
Lengo la usafiri wa umma ni kuwasiaidia watu kurahisisha safari zao, lakini inapoweka mazingira kuwa magumu zaidi hapo hauwasaidii bali unawaumiza!

Unajua umbali uliopo kutoka mbagala mpaka mbezi Luis?! Hapo sijagusia ndani zaidi kama charambe, matitu, chamazi, mbande, kisewe, msongola, mvuti na chanika?!

Unajua umbali uliopo kutoka kongowe, kibada , mjimwema, kigamboni, mpaka mbezi Luis?!

Unajua umbali uliopo kutoka mwandege, kisemvule mpaka mbezi Luis?!

Kote huko hakuna basi la moja kwa moja mpaka mbezi stendi kuu, lazima upande madaladala mawili au matatu kufika mbezi bus terminal,

Hapo abiria anakwenda either moshi, arusha, tabora, singida, shinyanga, mwanza ,kigoma au kagera! Aamke saa tisa usiku kuwahi daladala kutoka kisemvule, asubiri ijae, bado hujagusia foleni, ashuke kariakoo au tandika, achukue daladala nyingine hadi mbezi , mtu huyu ana watoto na mizigo tele!

Hapo utakuwa umemsaidia urahisi wa safari yake au umemtwika mateso zaidi?! Serikali iliangalie hii upya kwa jicho la tatu. Wengi tulikuwa tunategemea urahisi wa kupandia stendi ndogo na ofisi ndogo za mabasi husika ya mikoani.
Hivi mtu wa mbezi luis, tegeta, kibaha, bunju ilikua akitaka kwenda mtwara ni mpaka aje mbagala?
 
Hapana mkuu MUNDENDE kuna mabasi kutoka Tanga , morogoro yanayoenda mtwara wanapanda hayo!

pia ubungo terminal mabasi ya kusini yalikuwepo mengi tu.
 
Mkuu hebu fikiria watu wenye hali duni, sio kila mtu ana uwezo wa kugharamia nauli ya mlolongo wote huo wa kupanda daladala mbili au tatu kabla hajafika bus terminal,

Tuache kufanya biashara kwenye roho za watanzania, matatizo ya watanzania msigeuze mtaji wa kujitajirisha, kazi ya serikali ni kuweka mazingira mazuri ya kurahisha maisha ya wananchi wake na sio kuwaongezea mizigo yao!

Nashindwa kuelewa ile slogan ya "serikali ya wanyonge!"
Sawa
 
Nadhani ni mbezi high to machimbo to mpigi magoe to bunju via pande. Inapigwa mkeka ile aliongelea mtemvu pale akimuomba raisi.
Zile ni siasa tu mbona hata mnyika alikuwa anapigia kelele sanaa, lkn ndio barabara hiyo bila shaka
 
Kuna tangazo linasema safari zote zote, zitaanzia stend mpya MAGUFULI. Tangazo linazidi kusema Mabasi makubwa wakodishe mini bus kuwasafirisha abiria kuwaleta stend mpya au wawaelekeze abiria kuja Mbezi.

Sasa swali:
1. Anayekwenda Mtwara na yuko Mbagala, naye aje Mbezi? maana tangazo linasema stend zote za Temeke etc zimefutwa

2. Anayekwenda Tanga/Moshi/Arusha na yuko Tegeta aje Mbezi if not so, mabasi yaliyokuwa yanapitia Bagamoyo niliyoyataja hapo juu , mtu wa Tegeta atayapandia wapi? aje Mbezi?

3. Mabasi ya Tanga/Moshi/Arusha kupitia Bagamoyo yatachukua njia gani kukusanya watu wa Mwenge, Tegeta, Bunju then na kuendelea na safari ya kwenda Mikoa hiyo via Bagamoyo? Au wa Mwenge aje Mbezi? Wa Bunju? AU MABASI YATATOKA MBEZI NA KUJA NA MOROGORO ROAD, UBUNGO, MWENGE NA KUINGIA BAGAMOYO ROAD?

Msaada tafadhali wa maswali hayo.

Wewe kwa hakili zako unadhani wakati stend ipo ubungo unadhani abiria wte walikuwa wanakaa ubungo.
Au kwa hakiri yko unadhani abiria wte wanaosafiri kwenda mtwara wte wanakaa mbagara au temeke? Kadharika wa arusha wte wanakaa tegeta au huko unako lalamikia?? Lazima tuwe na fist point moja.

Hayo mengine sasa nisisi abiria na wasafirishaji ndo watazidiana ujanja wakuwa na ofice za ziada km leo ilivyo hapo urafiki kamata. Na kariakoo.
 
Kuna tangazo linasema safari zote zote, zitaanzia stend mpya MAGUFULI. Tangazo linazidi kusema Mabasi makubwa wakodishe mini bus kuwasafirisha abiria kuwaleta stend mpya au wawaelekeze abiria kuja Mbezi.

Sasa swali:
1. Anayekwenda Mtwara na yuko Mbagala, naye aje Mbezi? maana tangazo linasema stend zote za Temeke etc zimefutwa

2. Anayekwenda Tanga/Moshi/Arusha na yuko Tegeta aje Mbezi if not so, mabasi yaliyokuwa yanapitia Bagamoyo niliyoyataja hapo juu , mtu wa Tegeta atayapandia wapi? aje Mbezi?

3. Mabasi ya Tanga/Moshi/Arusha kupitia Bagamoyo yatachukua njia gani kukusanya watu wa Mwenge, Tegeta, Bunju then na kuendelea na safari ya kwenda Mikoa hiyo via Bagamoyo? Au wa Mwenge aje Mbezi? Wa Bunju? AU MABASI YATATOKA MBEZI NA KUJA NA MOROGORO ROAD, UBUNGO, MWENGE NA KUINGIA BAGAMOYO ROAD?

Msaada tafadhali wa maswali hayo.

Uelewa wako tu kaka ni mdogo. Ila tumekuelewesha nadhani umeelewa et
 
Mbona stesheni ya reli ipo moja Dar na wote hupandia pale haijalishi unakaa mbezi, Bunju, kimara, mbagala au kigamboni
Tunapoongea maswala kama haya tuwe tunaangalia na muda jamani! Kumbuka hizo treni huwa zinaondoka mchana au jioni ilihali mabasi mengi yanaondoka alfajiri au asubuhi!

Sasa mtu anayetoka Mbagala sijui Chamazi au Kisemvule and co itamchukua muda gani hadi aje afike hapo Mbezi? Na unafikiri usafiri wa kutoka kule hadi hapo ni rahisi kihivyo?
 
Hiyo haina shida. Mradi waruhusiwe kupakia na kushusha abiria kwa vituo vyao mwisho wa siku.
Otherwise kituo kitakua ni mateso kwa watokeao Kongowe ya Mbagala, Kigamboni na maeneo yale, kwa sababu watalazimika kulala stendi ili kuwahi mabasi yaendayo njia za Morogoro na Bagamoyo.
 
Kuna tangazo linasema safari zote zote, zitaanzia stend mpya MAGUFULI. Tangazo linazidi kusema Mabasi makubwa wakodishe mini bus kuwasafirisha abiria kuwaleta stend mpya au wawaelekeze abiria kuja Mbezi.

Sasa swali:
1. Anayekwenda Mtwara na yuko Mbagala, naye aje Mbezi? maana tangazo linasema stend zote za Temeke etc zimefutwa

2. Anayekwenda Tanga/Moshi/Arusha na yuko Tegeta aje Mbezi if not so, mabasi yaliyokuwa yanapitia Bagamoyo niliyoyataja hapo juu , mtu wa Tegeta atayapandia wapi? aje Mbezi?

3. Mabasi ya Tanga/Moshi/Arusha kupitia Bagamoyo yatachukua njia gani kukusanya watu wa Mwenge, Tegeta, Bunju then na kuendelea na safari ya kwenda Mikoa hiyo via Bagamoyo? Au wa Mwenge aje Mbezi? Wa Bunju? AU MABASI YATATOKA MBEZI NA KUJA NA MOROGORO ROAD, UBUNGO, MWENGE NA KUINGIA BAGAMOYO ROAD?

Msaada tafadhali wa maswali hayo.
Wananchi wa Dar, mtavurugwa hadi mtapata akili. Hadi mtambue kuwa box la kura Lina dhamani gani
 
Hako kautaratibu kapo mikoa yote iliyijenga stendi Mpya. Kuna siku Nimeenda Iringa nako ni hivyo hivyo. Basi linaendana mjini na lina ofisi kubwa tu, lakini haliruhusiwi kwenda na abiria,mnashuka nje ya mji then mnapanda dalala.
Akili zetu watanzania huwa si za ku solve tatizo
 
Kuna tatizo hapo imagine unashuka saa sita usiku na daladala hakuna na una mizigo mingi mikubwa!!!
Wenye mabasi kushusha ofisi zao ilikuwa ni huduma nzuri ya kumsaidia abiria

Kinachotakiwa kitamkwe ni kuwa basi zote zipitie stendi kuu kuanzia safari au kumaliza safari ziwe na abiria au la lazima zipitie ila kusema marufuku kuwa na abiria haliko sawa

Pili kuua hivyo vituo vingine vilivyokuwepo ni kuua ajira za mamia ya watu waliokuwa wakipata riziki zao kupitia hizo stendi ndogo kuanzia maduka teksi bodaboda bajaj wabeba mizigo mama lishe nk zingeachwa tu kama sehemu ya Transit kama ilivyo ndege tu kuwa stendi kuu ubungo stendi ndogo temeke Au mbagala au tegeta au kariakoo au ofisi juu ya basi nk ili kuondoa usumbufu kwa abiria .Sipati picha mtu anaishi mbagala anaenda mtwara aende mbezi kupandia gari kule wakati mfano mwenye gari ana ofisi kuu hapo hapo mbagala na basi linaanzia hapo kwenda mbezi kubeba abiria!!!!

Chukulia mfano basi zima wamekata tiketi watani zangu wamakonde wanaoishi mbagala wanaenda kwao basi linaanzia hapo hapo mbagala ofisi kuu ya basi .Kwa hiyo hao makonde wanatakiwa wapande daladala kwenda mbezi na hilo basi liende tupu hadi mbezi lipakie hao makonde kwenda nao mtwara!!! ni kituko badi watakalopanda liko mbeke yao tupu na wao wako kwenye daladala kwenda mbezi

Haya maamuzi mengine hayako sahihi
You have logic
 
Back
Top Bottom