Maswali kuhusu matumizi ya stendi mpya ya mabasi Mbezi (so-called Magufuli)

Siku unasafiri utayapata majibu ya maswali yako yote.
 
Mfano wa Dodoma ni mzuri sana, Shabiby, Kimbinyiko na BM Coach wana mini terminals zao na reporting time zake ni 1Hr before departure. Kama safari ni Saa 12:00 asbh, ofisini reporting time ni Saa11:00alfajiri na departure hapo ofisini ni saa 11:30, chombo inasogea 88 ikifika 12:00 asbh mwendo mdundo. So abiria atapandia pale palipo na unafuu kwake. For the sake of wale wasafirio uelekeo tofauti na location ya stendi kuu, kama Babati, Arusha, Moshi n.k wao wanasubiria mabasi huko huko yakitoka stendi kuu wanapanda na kuendelea na safari, the same applies to wale waendao Iringa, Mbeya, Njombe n.k nao wanasubiria Iringa Road. Ndivyo kwa case ya Dar ilivyo kwa njia kuu zitokazo Kilwa Rd, Morogoro Rd, Bagamoyo Rd
 
Kwa upande mwingine hali ya usafiri wa umma kwa mji wa Dar na ushindani wa kibiashara uliwafanya wamiliki wa mabus kuanzisha utaratibu wa kuwa na baadhi ya vyombo vyao kuwa destinations zake huko pembezoni ili kuwasaidia abiria wao. Tilisho na Esther wanalaza Bus Mbagala Mbande wanayo pia yanalolala Chanika, hii imekua ni msaada mkubwa kwa abiria watokao maeneo hayo. Hustle ya kuelekea stendi alfajiri ni kubwa sana na very stressful so is kurudi nyumbani kutokea safarini na mizigo. Haya mabus yalipunguzia sana abiria wake 'mzigo' as mtu akishuka anakamata boda ya buku tu ama bajaj ya buku 2 from main road yupo kwake na mizigo yake salama salmini. This shud be maintained to ease makali wapitiayo wananchi
 
Kama ni viongozi washamba kwa nini walipewa uongozi?

Mie nadhani waliowaweka madarakani ndio washamba wakubwa 😁
 
Laiti kama baba wa taifa angefufuka leo kuna watu wangeona moto
 
Kama sijakupata hivi, kwani Stand ilipokuwa Ubungo, wakazi wa maeneo mengine walikuwa wanafanyaje?
 
Huo mradi wa stand ya mabasi ya mbezi ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

Kwanza design ya kishamba sana.. hata morogoro wamefanya vizuri..

Pili bil 50 zingeweza jenga jengo la abiria mwanza ambapo wanajenga jengo la abiria la bil 12.

Plan ya zamani ilikua ni kila kanda kuwa na stand yake,

1. Bunju
2. Mbezi
3. Mbagala

Sasa wao wanataka kila kitu mbezi..

Leo nimesikia abiria wamesha anza kuibiwa ?[emoji1]
 
Iringa
Tanga
Njombe

Ni majanga.. kwanini wanataka hizi stand kuwa biashara wakati zimejengwa kwa kodi yetu.
Huu ujinga upo Tanga,

Mnashushwa Kange, mnapandishwa daladala had mjini, Bus linaenda tupu mjini. Na vice versa

Halafu mizigo mtachukua mjini.
 
Nadhani ni mikwara tu hiyo, soon utaratibu utaendele kama kawaida
 
Stand hii hata haina hadhi ya kuitwa jina la Rais.. pia stand kwa mabasi kwa nchi za africa wanacomplicate mno.

Jengo kama lile wamejaa wachoma mahindi? Si bora wangejenga shule moja matata sana ya vipaji maalum.
 
Tangazo linasema stend za Temeke , Mbagala zinakufa hakuna kupakia..... Ofisi ni kukata tiketi tu na siyo kupakia. majaribu kuliweka Tangazo, kesho nitaliweka
Nadhani umeelewa vibaya, Tangazo halimaanishi kwamba gari ikitoka Mbezi kuelekea Mtwara hairuhusiwi kupakia abiria Mbagala la hashaaa,bali ni lazima starting point iwe ni Mbezi, na sio Mbagala.
 
Malalamiko yako hayana msingi, wakati ule stand ziko kisutu na mnazi mmoja zilipohamia ubungo nako kulikuwepo na malalamiko kama haya.
 
Huyo dreva atakuwa ni mwehu, hivyo vituo ulivyovitaja vinakuwa vya kawaida tu na wanashusha na kupakia kama daladala zinavyofanya.
 
Malalamiko yako hayana msingi, wakati ule stand ziko kisutu na mnazi mmoja zilipohamia ubungo nako kulikuwepo na malalamiko kama haya.
Kijana kwanza una umri gani? Huwezi linganisha Dar es salaam ya wakati ule in terms of idadi ya watu na mazingira, hali ya wakati ule, areawise, etc na sasa. Mazingira ya sasa hayaruhusu kuwa na stend moj for over six million people..... miaka ya 70s and 80s
angalia popolation ya wakati huo na ya sasa......

Dar es Salaam Urban
(Growth % p.a)
1957 1967 1978 1988 2002 2012
128742 272821 769445 1205443 2336055 4364541
Growth, Internal Migration and Urbanization in Tanzania, 1967-2012 Phase 2 (Final Report)
 
Kama sijakupata hivi, kwani Stand ilipokuwa Ubungo, wakazi wa maeneo mengine walikuwa wanafanyaje?
Ulikuwa unapakilia na kushuka unapotaka. Sasa hii imekatazwa, stend say za Mbagala, Temeke zimekatazwa kupakia na kushusha na ofisi za makampuni ni kukata tiketi tu na siyo kupakia abiria
 
Mbagala si watapandia mbagala. Ila magari yataanzia mbezi then watapita temeke mpaka mbagala then kimoja to mtwara.
The same to route ya moshi. Wanaanzia mbezi wanaikamata ubungo mwenge tegeta bunju bagamoyo then boom
Naona hujamuelewa uliyemquote, msome tena taratibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…