Maswali kuhusu matumizi ya stendi mpya ya mabasi Mbezi (so-called Magufuli)

Maswali kuhusu matumizi ya stendi mpya ya mabasi Mbezi (so-called Magufuli)

Siku unasafiri utayapata majibu ya maswali yako yote.
 
Mfano wa Dodoma ni mzuri sana, Shabiby, Kimbinyiko na BM Coach wana mini terminals zao na reporting time zake ni 1Hr before departure. Kama safari ni Saa 12:00 asbh, ofisini reporting time ni Saa11:00alfajiri na departure hapo ofisini ni saa 11:30, chombo inasogea 88 ikifika 12:00 asbh mwendo mdundo. So abiria atapandia pale palipo na unafuu kwake. For the sake of wale wasafirio uelekeo tofauti na location ya stendi kuu, kama Babati, Arusha, Moshi n.k wao wanasubiria mabasi huko huko yakitoka stendi kuu wanapanda na kuendelea na safari, the same applies to wale waendao Iringa, Mbeya, Njombe n.k nao wanasubiria Iringa Road. Ndivyo kwa case ya Dar ilivyo kwa njia kuu zitokazo Kilwa Rd, Morogoro Rd, Bagamoyo Rd
 
Kwa upande mwingine hali ya usafiri wa umma kwa mji wa Dar na ushindani wa kibiashara uliwafanya wamiliki wa mabus kuanzisha utaratibu wa kuwa na baadhi ya vyombo vyao kuwa destinations zake huko pembezoni ili kuwasaidia abiria wao. Tilisho na Esther wanalaza Bus Mbagala Mbande wanayo pia yanalolala Chanika, hii imekua ni msaada mkubwa kwa abiria watokao maeneo hayo. Hustle ya kuelekea stendi alfajiri ni kubwa sana na very stressful so is kurudi nyumbani kutokea safarini na mizigo. Haya mabus yalipunguzia sana abiria wake 'mzigo' as mtu akishuka anakamata boda ya buku tu ama bajaj ya buku 2 from main road yupo kwake na mizigo yake salama salmini. This shud be maintained to ease makali wapitiayo wananchi
 
Kama ni viongozi washamba kwa nini walipewa uongozi?

Mie nadhani waliowaweka madarakani ndio washamba wakubwa 😁
 
Laiti kama baba wa taifa angefufuka leo kuna watu wangeona moto
 
Ndio ujinga mkubwa wanaofanyiwa watu. You incur double expenses maana kama una mizigo mikubwa unajuta! Ndiyo hiyo inakuja Mbezi na foleni hizi. Unashuka Mbezi, unakwendaje Kimara na foleni hizi za Dar na mizigo! Wameweka utaratibu gani wa shuttle buses kutoka Mbezi kwenda sehemu zingine za Jiji, say Mbezi Mbagala, Temeke, Kigamboni, Mwenge etc etc etc. Ilibidi kuwe na connection za city shuttle buses to various destinations in Dar!
Kama sijakupata hivi, kwani Stand ilipokuwa Ubungo, wakazi wa maeneo mengine walikuwa wanafanyaje?
 
Huo mradi wa stand ya mabasi ya mbezi ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

Kwanza design ya kishamba sana.. hata morogoro wamefanya vizuri..

Pili bil 50 zingeweza jenga jengo la abiria mwanza ambapo wanajenga jengo la abiria la bil 12.

Plan ya zamani ilikua ni kila kanda kuwa na stand yake,

1. Bunju
2. Mbezi
3. Mbagala

Sasa wao wanataka kila kitu mbezi..

Leo nimesikia abiria wamesha anza kuibiwa ?[emoji1]
Kuna tangazo linasema safari zote zote, zitaanzia stend mpya MAGUFULI. Tangazo linazidi kusema Mabasi makubwa wakodishe mini bus kuwasafirisha abiria kuwaleta stend mpya au wawaelekeze abiria kuja Mbezi.

Sasa swali:
1. Anayekwenda Mtwara na yuko Mbagala, naye aje Mbezi? maana tangazo linasema stend zote za Temeke etc zimefutwa

2. Anayekwenda Tanga/Moshi/Arusha na yuko Tegeta aje Mbezi if not so, mabasi yaliyokuwa yanapitia Bagamoyo niliyoyataja hapo juu , mtu wa Tegeta atayapandia wapi? aje Mbezi?

3. Mabasi ya Tanga/Moshi/Arusha kupitia Bagamoyo yatachukua njia gani kukusanya watu wa Mwenge, Tegeta, Bunju then na kuendelea na safari ya kwenda Mikoa hiyo via Bagamoyo? Au wa Mwenge aje Mbezi? Wa Bunju? AU MABASI YATATOKA MBEZI NA KUJA NA MOROGORO ROAD, UBUNGO, MWENGE NA KUINGIA BAGAMOYO ROAD?

Msaada tafadhali wa maswali hayo.
 
Iringa
Tanga
Njombe

Ni majanga.. kwanini wanataka hizi stand kuwa biashara wakati zimejengwa kwa kodi yetu.
Huu ujinga upo Tanga,

Mnashushwa Kange, mnapandishwa daladala had mjini, Bus linaenda tupu mjini. Na vice versa

Halafu mizigo mtachukua mjini.
 
Kuna tatizo hapo imagine unashuka saa sita usiku na daladala hakuna na una mizigo mingi mikubwa!!!
Wenye mabasi kushusha ofisi zao ilikuwa ni huduma nzuri ya kumsaidia abiria


Kinachotakiwa kitamkwe ni kuwa basi zote zipitie stendi kuu kuanzia safari au kumaliza safari ziwe na abiria au la lazima zipitie ila kusema marufuku kuwa na abiria haliko sawa

Pili kuua hivyo vituo vingine vilivyokuwepo ni kuua ajira za mamia ya watu waliokuwa wakipata riziki zao kupitia hizo stendi ndogo kuanzia maduka teksi bodaboda bajaj wabeba mizigo mama lishe nk zingeachwa tu kama sehemu ya Transit kama ilivyo ndege tu kuwa stendi kuu ubungo stendi ndogo temeke Au mbagala au tegeta au kariakoo au ofisi juu ya basi nk ili kuondoa usumbufu kwa abiria .Sipati picha mtu anaishi mbagala anaenda mtwara aende mbezi kupandia gari kule wakati mfano mwenye gari ana ofisi kuu hapo hapo mbagala na basi linaanzia hapo kwenda mbezi kubeba abiria!!!!

Chukulia mfano basi zima wamekata tiketi watani zangu wamakonde wanaoishi mbagala wanaenda kwao basi linaanzia hapo hapo mbagala ofisi kuu ya basi .Kwa hiyo hao makonde wanatakiwa wapande daladala kwenda mbezi na hilo basi liende tupu hadi mbezi lipakie hao makonde kwenda nao mtwara!!! ni kituko badi watakalopanda liko mbeke yao tupu na wao wako kwenye daladala kwenda mbezi

Haya maamuzi mengine hayako sahihi
Nadhani ni mikwara tu hiyo, soon utaratibu utaendele kama kawaida
 
Stand hii hata haina hadhi ya kuitwa jina la Rais.. pia stand kwa mabasi kwa nchi za africa wanacomplicate mno.

Jengo kama lile wamejaa wachoma mahindi? Si bora wangejenga shule moja matata sana ya vipaji maalum.
Hili la Bagamoyo road nimeliwaza sana,
Mimi hua nachukua mizigo k.koo naipeleka mwenge, basi inakuja inabeba..

Sasa najaribu kuwaza kama hakutakua na basi inafika mwenge hili litakua ni pigo kwanguu,
Either kukodi cary mpk mbezi au nihamie kwenye transist za mafuso zinazoondoka usiku.
 
Tangazo linasema stend za Temeke , Mbagala zinakufa hakuna kupakia..... Ofisi ni kukata tiketi tu na siyo kupakia. majaribu kuliweka Tangazo, kesho nitaliweka
Nadhani umeelewa vibaya, Tangazo halimaanishi kwamba gari ikitoka Mbezi kuelekea Mtwara hairuhusiwi kupakia abiria Mbagala la hashaaa,bali ni lazima starting point iwe ni Mbezi, na sio Mbagala.
 
Ndio ujinga mkubwa wanaofanyiwa watu. You incur double expenses maana kama una mizigo mikubwa unajuta! Ndiyo hiyo inakuja Mbezi na foleni hizi. Unashuka Mbezi, unakwendaje Kimara na foleni hizi za Dar na mizigo! Wameweka utaratibu gani wa shuttle buses kutoka Mbezi kwenda sehemu zingine za Jiji, say Mbezi Mbagala, Temeke, Kigamboni, Mwenge etc etc etc. Ilibidi kuwe na connection za city shuttle buses to various destinations in Dar!
Malalamiko yako hayana msingi, wakati ule stand ziko kisutu na mnazi mmoja zilipohamia ubungo nako kulikuwepo na malalamiko kama haya.
 
Sipati picha basi limetoka mtwara mtu anashuka mbagala mwenye basi akifika mbagaka anaongeza mwendo anasema hakuna kushuka hapa lazima nikawashushe mbezi !l

Au basi limetoka Moshi au Arusha watu wanashuka Tegeta dereva anaongeza moto kuwa hakuna kushuka lazima nikawsdhushe mbezi maruhuni nyie hashishwi mtu hapa!!! Haturuhusiwi tumeambiwa lazima tuwashushe mbezi


Sipati picha kitakachomkuta dereva!!!!
Huyo dreva atakuwa ni mwehu, hivyo vituo ulivyovitaja vinakuwa vya kawaida tu na wanashusha na kupakia kama daladala zinavyofanya.
 
Malalamiko yako hayana msingi, wakati ule stand ziko kisutu na mnazi mmoja zilipohamia ubungo nako kulikuwepo na malalamiko kama haya.
Kijana kwanza una umri gani? Huwezi linganisha Dar es salaam ya wakati ule in terms of idadi ya watu na mazingira, hali ya wakati ule, areawise, etc na sasa. Mazingira ya sasa hayaruhusu kuwa na stend moj for over six million people..... miaka ya 70s and 80s
angalia popolation ya wakati huo na ya sasa......

Dar es Salaam Urban
(Growth % p.a)
1957 1967 1978 1988 2002 2012
128742 272821 769445 1205443 2336055 4364541
Growth, Internal Migration and Urbanization in Tanzania, 1967-2012 Phase 2 (Final Report)
 
Kama sijakupata hivi, kwani Stand ilipokuwa Ubungo, wakazi wa maeneo mengine walikuwa wanafanyaje?
Ulikuwa unapakilia na kushuka unapotaka. Sasa hii imekatazwa, stend say za Mbagala, Temeke zimekatazwa kupakia na kushusha na ofisi za makampuni ni kukata tiketi tu na siyo kupakia abiria
 
Mbagala si watapandia mbagala. Ila magari yataanzia mbezi then watapita temeke mpaka mbagala then kimoja to mtwara.
The same to route ya moshi. Wanaanzia mbezi wanaikamata ubungo mwenge tegeta bunju bagamoyo then boom
Naona hujamuelewa uliyemquote, msome tena taratibu.
 
Back
Top Bottom