Maswali kwa Profesa Musa Assad kuhusu mkataba wa Bandari

Na zanzibar kuna mega trades zinafanyika hapo ambazo zina attract mega ships! Mwanza kuna mega ships zipi na mega trade zipi? Kigoma? Why include all hata vibandari vidogo, vina mega ships zipi na mega trade zipi? Kuna kitu hakiko sawa......
Ndugu yangu kubali kuwa hapa kuna kitu hakiko sawa. Watanganyika hawatalikubali hili.....

1. Ungelikuwa wewe mtu anakuja kuwekeza kwenye shamba lako, utakubali mkataba kama huo? Tuanzie kwenye simple analogy kama hii. Mimi siwezi, mwenye akili timamu hawezi, uwekeze kwangu na husemi utanilipa nini kutoka na uwekezaji wako? Utakaa muda gani? (watu huwa wanakodi mashamba makubwa ya mamilioni / mamia/ ya hectares/acres kulima, watakubali mkataba kama ule?

2. Mkataba huo una sifa za kuwa mkataba? soma hii article ya JF

 
Huyu anampiga Dr. Rigemeleza Nshala, mtu ambaye ana Master Degree ya Mikataba ya uwekezaji wa kimataifa katika chuo kikuu namba moja Duniani yaani Havard, na pia ni Nshomile
Mnaabudu vyeti!
Bakhresa hana cheti lkn huyo Nshala mwenyewe analipwa na Matajiri ambao hata fom4 hawaijui
 
Mnakubaliana chumbani? Mnaliondoa kwa siri? Au waliliondoa baada ya kuwa na wazo la kuuza za Watanganyika? Kuna kitu mbaya kitakuja, sidhani kama watanganyika watakubali hili kutendeka kwao......
 
Mnaabudu vyeti!
Bakhresa hana cheti lkn huyo Nshala mwenyewe analipwa na Matajiri ambao hata fom4 hawaijui
Achana na mambo ya ngekewa, watu kama hao ni ngekewa tu!
 
Huyu naye kala mlungula wa DP WORLD
 
Huyu naye kala mlungula wa @dp
 
Mkataba hauna shida yoyote. Twenye shida sisi wasomaji wa mkataba. Wewe unadhani DPW wataendeza kila Bandari kama mnavyoaminishwa na akila TL? Yaani akajenge Bandari kisorya au Lindi?? Kwani wanaosema maeneo ya kipaumbele unadhani ni yepi? Ushasikia popote duniani DPW anaendeleza na kuendesha Bandari za kuvulia dagaa tonge? Unajua baadhi ya mambo inabidi mtumie akili zenu hata za kuzaliwa basi! Believe me, tunaaminishana ujinga mkubwa sana mitaani kuliko uhalisia wa jambo lilivyo.
 
Kwa niaba ya Prof. Assad,

Jibu la swali la kwanza:
Zanzibar ni mamlaka kamili kwenye masuala ambayo si ya Muungano. Kama ni mamlaka kamili ina wajibu wa kipekee wa kuingia makubaliano na mikataba kama nchi kamili. Makubaliano haya yamefikiwa kati ya Serikali za nchi, ndani ya nchi kunaweza kuwa na serikali Zaidi ya Moja kulingana na mfumo wa kiutawala na Kila serikali inakuwa na mamlaka yake kamili.

Jibu Kwa swali la pili:
Prof. Assad ni mtaalamu wa masuala ya fedha. Mtaalamu wa masuala ya fedha jukumu lake ni kutambua fursa na Prof.Assad kaona Kuna fursa kwenye uwekezaji huu. Prof. Assad ni mtu ambaye kafanya kazi na mamlaka ya bunge na anatambua kazi ya bunge kwenye makubaliano hayo ambayo ni kazi ya kisheria imekwisha na bunge kuridhia maana yake ni Muda wa wataalamu wa uchumi, biashara na uwekezaji kumalizia sehemu ya kipande kilichobaki.

Jibu la swali la tatu:
Haimaanishi maoni ya kina Prof.Shivji, Tundu Lissu au wakili mwakubusi ni bora zaidi Kwa sababu ni wanasheria. Mbowe sio mwanasheria lakini kauchambua mkataba huo. Ni kusema kwamba kila mwenye uelewa na ufahamu anaweza kuchambua.
 
Fine, uko sahihi, hawawezi kujenga bandari za dagaa. Lkn mkataba unasema hivyo.....lakes and oceans ports! If that is not the case, then mkataba wa udanganyifu! na mkataba wa udanganyifu ni batili!
 
Fine, uko sahihi, hawawezi kujenga bandari za dagaa. Lkn mkataba unasema hivyo.....lakes and oceans ports! If that is not the case, then mkataba wa udanganyifu! na mkataba wa udanganyifu ni batili!
Nimekuuliza swali, je umeshaona hayo maeneo ya kipaumbele?
 
Huu mkataba ni wa miaka mingapi?
 
Swali No. 2 is the best of all. Natamani sana kusikia jibu lake akilitoa Prof. Assad.
 
Maswali ya kipumbavu na ya kitoto,umeambiwa mara kadhaa Kuna sheria 2 tofauti za Mamlaka ya Bandari Zanzibar na Tanzania Sasa sijui unatakaje Bandari za Zenji ziwepo.

Pili kwani unampangia Mwekezaji choice yake?
Tusimpangie Na Bandari ni zetu? Kwanini yeye (mwekezaji) ametupangia masharti kibao kupitia Wazanzibari?
 
Kwani mwenye shida na uwekezaji ni DP au nyie?
Ushawahi kusikia sauti ya watanzania kupitia Bunge lao au majukwaa mengine ya kijamii kwamba tunahitaji Bandari zote za Tanganyika zibinafsishwe?
Kama Sssi tunas hida ya uwekezaji kwanini Serikali ya awamu ya 5 ilivutana misuli na Barrick Gold ili kupata win-win situation? Msijitoe ufahamu.
 
Ndio
 
Nimekuuliza swali, je umeshaona hayo maeneo ya kipaumbele?
Kumbuka by that token (ya kipaumbele chake) na kwa mkataba ulivyo hakuna tema mwingine wa kuzigusa bandari hizo (exclusive rights), hivyo anaweza kukaa miaka 200 bila kuziendeleza...na mtu asiziguse kama tukitaka wenyewe kuziendeleza........ Mkataba huuu ni hovyo kabisa!
 
Jibu la Profesa Assad limeumiza mioyo ya jamaa waliowekeza kwenye upotoshaji mwingi na ubaguzi wa chini kwa chini.

Bandari ya Zanzibar ilishafanyiwa uwekezaji mwaka mmoja kabla ya hii ya huku bara. Bandari ya mpigaduru ilipata mwekezaji na mpaka muda huu atakuwa pengine keshaanza kazi. Pia DP World ni mmiliki wa mali zilizopo DRC na Rwanda hamiliki chochote kule Zanzibar hivyo hana sababu ya kuitaka bandari yao.

Kaongea kama mwanazuoni na katoa maoni ya jumla baada ya mwandishi wa habari kumuuliza maswali, sawa sawa na hao wengine walivyoyatoa maoni. Na hiki alichokisema sio mara ya kwanza kwake kukitamka anapohojiwa na waandishi wa habari, ni kweli kielimu tupo chini sana. Uwezo wa taasisi zetu inakuwa na matokeo duni kwa sababu ya utendaji mzima kuwa duni na hakuna anayejali.

Na pia ni kweli bandari zetu zinapungukiwa katika maeneo hayo aliyoyataja, haihitaji kuwa mbobezi wa sekta fulani kuona kuwa usomi wetu mwingi umejaa ubabaishaji. Na huyu ni CAG mstaafu ameongea kwa uzoefu wake wa jumla wa sekta nyingi alizozifanyia ukaguzi.


Prof Assad kuongelea upungufu wa bandari, anayo mamlaka hayo kwani ni mojawapo ya taasisi alizozikagua mara nyingi na pia akawa anatoa muhtasari wa kazi ya ukaguzi iliyofanyika.

Kuyapokea maoni ya kitaalam aliyoyatoa wakati ule akiwa CAG hakuna tofauti yoyote na kuyapokea maoni hayo hayo anayoyatoa leo hii akiwa mstaafu.

Anayo mamlaka ya kimaadili ya kuikosoa jamii yetu kwa uzoefu alionao kama mhasibu mbobezi.
 
Huu ndo usomaji mbaya wa mkataba huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…