Sio nimejitakia kuumia ..Unakuwa umejitakia tu kuumia. Yaani swali wakuulize wengine kuumia uumie wewe. Jifunze kupokea usichoweza kukibadili.
Well said [emoji1433][emoji1433]Mtu mwenye busara huuliza
Mungu amekubariki ndoa?
Mungu amekubariki watoto?
Mwenye busara hatotoka kujua ni kwa nn huna mtoto wala huna ndoa.
Na ni lazima akuandae vya kutosha kabla ya kuhoji hayo maswali
Kama huwezi kuwazuia kukuuliza nakushauri uizoee hiyo hali kama unavyozoea hali nyinginezo zenye kukukera. Usijinyime furaha kwa mambo ambayo yapo nje ya uwezo wako.Sio nimejitakia kuumia ..
Kila unapoenda ndo uulizwe kweli
Eti ooh kwa nn bado haujaolewa .
Do you think it's right ?
Mungu ndo anayetoa baraka hizi ..
Sasa Mimi nipo nasubiri wakati wa Bwana halafu unanijia eti ooh wewe endelea kuchagua .
Kuchagua nini kimfano ? yaani ukubali kuolewa haraka kisa upo desperate longing for Hubby ,
Kinachouma ni hayo maswali ambayo unaliuzwa tu out of nowhere , people have to respect others and not otherwise ..
Hiyo kusema hupendi kuulizwa ndio kujinyima raha kwenyewe huko. Wakikuuliza unapungukiwa nini kwa mfano?Hainyimi furaha hata ..
Kinachokera ni kuulizwa , wengine hatupendi kuulizwa maswali ya hivyo .
Kwa nini waniulize kimfano ?Hiyo kusema hupendi kuulizwa ndio kujinyima raha kwenyewe huko. Wakikuuliza unapungukiwa nini kwa mfano?
Kuna mdada mmoja age mate wangu, aliolewa now anawatoto wawili , tuliishi nae mtaa mmoja ,tukaja tengana baada ya Kila mmoja kwenda vyuo tofauti, tumekuja onana hivi kàribuni ananiuliza hivi unamtoto hata mmoja, nameambia Sina, anajibuu duuuu na haujaolewa umri unaenda tafuta ata mwanaume uzaenae mtoto mmoja.Haya mambo uulizwe na watu wako wa karibu ni sawa sio unakutana na mtu ana watoto wake7 kama mama D halafu anakuuliza Rory una watoto wangapi? Unamwambia sina. Anaendelea umeolewa? Unamjibu hapana. Anaongeza tafuta mwanaume wewe uzae.... unazeeka😎
Hahahahaa
UkimwiSwali lingine la kizushi🤗
Msijali mtaolewa tu.
Ni kweli kabisa,kwa mimi mkristo naamini kabisa kuna baadhi ya wito,au jambo ulilotumwa nalo duniani hautokaa ulikamilishe/ukamilishe vyema, mpaka ukutane na mwenza alieumbwa kukusaidia.Kuolewa tumeolewa na kuoa wameoa
Lakini je, unajua kingine ulichotumwa na muumba wako duniani? Unaijua karama au kipaji chako ulichopewa na Mungu uje ukifanyie kazi duniani?
Au unafikiri kuishi na mtu na kufanya mapenzi ndio kipaji chako? Na kama unadhani hiyo ndio karama, talanta au kipaji basi hutofautiani na kuku, mbwa, nyau, mbuzi, ng'ombe maana wao pia wanafanya hicho hicho na wanazaa watoto kama wewe
Kwa binadamu ndoa sio jukumu au hitaji la pekee linalokamilisha umwanadamu wake japo ni moja ya mahitaji kwa wanaohitaji
Ni kweli kabisa,kwa mimi mkristo naamini kabisa kuna baadhi ya wito,au jambo ulilotumwa nalo duniani hautokaa ulikamilishe/ukamilishe vyema, mpaka ukutane na mwenza alieumbwa kukusaidia.
Kwa wanaume Biblia inatuambia "apatae mke apata kitu chema,nae apata KIBALI toka Bwana (Mungu)" inamaana usipokua na mke sahihi,katika huo wito wako kuna sehemu utakwama,kwakua huna kibali kutoka kwa aliekupa huo wito.
Hivyo kama ulivyosema ni vema mtu atambue wito wake,kabla hajaoa au kuolewa.Lakini pia suala la kuoa au kuolewa ni muhimu sana,ndio maana Mungu aliumba ndoa kama taasisi ya kwanza kabisa duniani baina ya mme na mke.
Tukiongelea ukweli kabisa Mama D,ni watu wangapi unawajua ambao hawajaoa au kuolewa na hawazini?asilimia 99 watu wanazini,na bado kuoa na kuolewa hawataki.Hakuna lazima wala kulazimishwa wala sheria au shurti kwenye kuoa na kuolewa ANKO JEI.
Ila zinaa ndio imekatazwa. Kama unaweza kuishi bila kuoa au kuolewa na ukaacha kufanya zinaa Mungu anapendezwa na wewe sawasawa na wale waliooa au kuoleawa ili wasiingie kwenye zinaa
Sijui unaelewa[emoji848][emoji848][emoji848]
1Wakorinto 7: 1 - 2
Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke. Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe
Tukiongelea ukweli kabisa Mama D,ni watu wangapi unawajua ambao hawajaoa au kuolewa na hawazini?asilimia 99 watu wanazini,na bado kuoa na kuolewa hawataki.
So muda mwingine mtu anaweza kukuuliza unaoa/unaolewa lini,sio kama anataka kujua tarehe,bali anakupa indirect message kua ni bora uwe ndoani kuliko maisha hayo ya kuzini.(japo sio vema kuuliza uliza watu hivyo)
Kama mtu anaweza kukaa bila kuzini its okay,but kama huwezi oa au olewa.
[emoji23][emoji23][emoji23] hapo ndo utaonekana una stressWadada ambao hamjaolewa ikitokea mtu kakuuliza unaolewa Lin na wewe muulize Ni lini anakufa ili aache kuuliza hayo maswali...
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23] hapo ndo utaonekana una stress
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Kuna mtu alimuuliza dada flani una watoto wangapi? Akamjibu sina.
Akendelea kumuuliza hadi leo huna mtoto? Tafuta mwanaume yoyote uzae nae
Yule dada kumbe kakwazika, na yeye akamuuliza wazazi wako wapo wapi? Akamjibu sina mzazi walikufa nikiwa mdogo. Akamwambia tafuta mtu yoyote awe mzazi wako, unaishije bila baba wala mama?