Maswali ya kuudhi - Umeoa? Umeolewa? Unao/olewa lini? Una watoto wangapi?

Maswali ya kuudhi - Umeoa? Umeolewa? Unao/olewa lini? Una watoto wangapi?

Haya mambo uulizwe na watu wako wa karibu ni sawa sio unakutana na mtu ana watoto wake7 kama mama D halafu anakuuliza Rory una watoto wangapi? Unamwambia sina. Anaendelea umeolewa? Unamjibu hapana. Anaongeza tafuta mwanaume wewe uzae.... unazeeka[emoji41]

Hahahahaa
Acha utopolo hayo maswali ni kwa faida yako pia ikiwemo aina gani ya status upewe
 
Majibu yako ndio yanaleta aina hiyo ya ushauri
 
Acha utopolo hayo maswali ni kwa faida yako pia ikiwemo aina gani ya status upewe

Wengi wanaopenda kuuliza haya maswali ni utopolo mtupu, tena wenyewe hata hiyo status ya kuuliza hawana
 
Ili iweje sass
unajua mtu akiona mfano una huzuni kupitiliza then akikuuliza umeolewa au umeoa anajua hayo ni yako ya maisha labda uamue mwenyewe kujitoa matatizoni.
mtu akikuona una furaha kupitiliza anaweza akakuuliza swali hilo kujua chanzo cha furaha yako na inaweza ikabadilishwa baada ya tendo hilo la kuoa au kuolewa au kupata mtoto
 
Haya maswali binafsi huwa nayachukia sana japo kweli nimeolewa na nina watoto. Ni maswali too personal kumuuliza mtu mzima mwenye akili zake maamuzi yake. Ila bahati mbaya ni maswali ambayo watu wengi huwa wanapenda kuuliza bila hata kuwaza hisia za wale wanaowauliza.
Tena heri haya maswali yatoke kwa mzazi au mtu wa karibu kuliko ilivyo kawaida kwa sasa.

Watu tujue kuwa single au kuwa kwenye mahusiano ni hali tuu kama ilivyo kuwa na kitu flani au kukosa kitu kingine kwenye maisha

Mtu anaweza kuwa single hajawa tayari kuingia kwenye jukumu la ndoa, sio sababu amekosa mtu wa kuoana nae kama wengi wanavyodhani

Kuna wakati mtu anakua single lakini anatamani sana kuwa ndani ya mahusiano ila anashindwa sababu hajampata mwenye sifa anazotaka

Wakati mwingine mtu yuko single sababu hana uwezo wa kuwa na mahusiano labda ana mapungu aliyozaliwa nayonayo

Na pia mtu anaweza kuwa single sababu alishapitia mahusiano yakamvuruga na kumpa maumivu makubwa sana, kwa hiyo kwake kuwa peke yake ndio amani

Ndoa na familia ni jambo la heri kwa wanadamu lakini pia sio amri useme lazima kila mtu aoe/aolewe; na Kuwa ndani ya ndoa au kuwa na watoto sio ujanja na kukosa iwe ujinga! Hata kwenye vitabu vitakatifu kuna watu ambao hawakuwahi kuoa/kuolewa, kuna watu walioolewa/walioowa wasipate watoto, na wapo watu walioowa/kuolewa katika umri mkubwa pia.

Yote juu ya yote, mipango ya Mungu ni sahihi na mawazo yake ni mawazo sahihi kwetu.
Hawa watarajiwa hapa wanatukumbusha kumshukuru Mungu kwa maisha tuliyo nayo, kumwomba Mungu afanye kwa wakati wake

View attachment 1695876
Sasa pia huwezi jua mtu Ana kuuliza Kama umeoa au umeolewa kwa sababu labda anataka kuanzisha mahusiano au kukutongoza ili aepushe migogoro ndo Mana anakuuliza ili usione kama anakuingilia katika ndoa yako

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Ile uliza inayolenga kwenye kuanzisha mahusiano hata haina maudhi......
Maudhi yapo kwa kina wale wanakuuliza tuu bila sababu, na kuendelea kuuliza na mwisho wanakupangia
Sasa kitu hakinipi huzuni wala stress kwanini kiwatese wao?
 
Mama D tangu ileeeee juzi kati yaani bado umeudhika tu hadi leo!??? Hii ni hatare na robo
 
30+ lazima ukasirike na roho iiume kwa maswali madogo, ila ukiwa 25- huwez kasirika,utajibu na kujibika
Sio lazima kama ni maamuzi yako
Na inaudhi kama mtu anakushinikiza kwa kitu usichokiweza kukipata
 
maswali ya kukera mengine:

1. ulimwaga ndani ?

2. mbona sjaona siku zangu ?

3. naumia mapaja, we unaendelea tu ?

4. nimechoka, tulale ?
 
Back
Top Bottom