Maswali ya kuudhi - Umeoa? Umeolewa? Unao/olewa lini? Una watoto wangapi?

mama D tumekutana mtaani nikakuelewa na mimi sitaki kutongoza mke wa mtu, nikikuuliza umeolewa nitakuwa nimekosea!? Nikikuuliza una watoto wangapi ili nijue ikitokea umenikubali, hao watoto watakuwa concern yangu nalo ni kosa!?

Nadhani shida ninayoiona hapo ni kukuuliza utazaa lini au utaolewa lini.
Hiyo ni sawa, ninaowaongelea hapa ni wale watu wanaulizaga tuu bila hata mpango. Tena wengi wanaoulizwa ni wanawake na wengi wanaouliza ni wanawake.
Hicho cha wewe kuniuliza mimi mbona mbona fresh sanaaaa
 
Hapo sawa.
 
Haya maswali binafsi huwa nayachukia sana japo kweli nimeolewa na nina watoto. Ni maswali too personal kumuuliza mtu mzima mwenye akili zake maamuzi yake. Ila bahati mbaya ni maswali ambayo watu wengi huwa wanapenda kuuliza bila hata kuwaza hisia za wale wanaowauliza.
Tena heri haya maswali yatoke kwa mzazi au mtu wa karibu kuliko ilivyo kawaida kwa sasa.

Watu tujue kuwa single au kuwa kwenye mahusiano ni hali tuu kama ilivyo kuwa na kitu flani au kukosa kitu kingine kwenye maisha

Mtu anaweza kuwa single hajawa tayari kuingia kwenye jukumu la ndoa, sio sababu amekosa mtu wa kuoana nae kama wengi wanavyodhani

Kuna wakati mtu anakua single lakini anatamani sana kuwa ndani ya mahusiano ila anashindwa sababu hajampata mwenye sifa anazotaka

Wakati mwingine mtu yuko single sababu hana uwezo wa kuwa na mahusiano labda ana mapungu aliyozaliwa nayonayo

Na pia mtu anaweza kuwa single sababu alishapitia mahusiano yakamvuruga na kumpa maumivu makubwa sana, kwa hiyo kwake kuwa peke yake ndio amani

Ndoa na familia ni jambo la heri kwa wanadamu lakini pia sio amri useme lazima kila mtu aoe/aolewe; na Kuwa ndani ya ndoa au kuwa na watoto sio ujanja na kukosa iwe ujinga! Hata kwenye vitabu vitakatifu kuna watu ambao hawakuwahi kuoa/kuolewa, kuna watu walioolewa/walioowa wasipate watoto, na wapo watu walioowa/kuolewa katika umri mkubwa pia.

Yote juu ya yote, mipango ya Mungu ni sahihi na mawazo yake ni mawazo sahihi kwetu.
Hawa watarajiwa hapa wanatukumbusha kumshukuru Mungu kwa maisha tuliyo nayo, kumwomba Mungu afanye kwa wakati wake

View attachment 1695876
Umeandika vizuri sana!
 
Kwa mtu ambaye anauwezo mkubwa wa kujua hisia za wengine huwaga hauliZi maswali hayo unless mpo kwenye interview na hata kwenye interview ni maswali ya kijinga kama kaZi haihusiani na status ya mtu ya mahusiano

Hayo tukaulizwe kwenye form ya kupata bima ya afya[emoji853][emoji853][emoji853]..

She is right kabisa but you have to be sensitive enough kujua swali hilo ni la kijinga...

Mbona umenenepa/umekonda?
 
Haya maswali binafsi huwa nayachukia sana japo kweli nimeolewa na nina watoto. Ni maswali too personal kumuuliza mtu mzima mwenye akili zake maamuzi yake. Ila bahati mbaya ni maswali ambayo watu wengi huwa wanapenda kuuliza bila hata kuwaza hisia za wale wanaowauliza.
Tena heri haya maswali yatoke kwa mzazi au mtu wa karibu kuliko ilivyo kawaida kwa sasa.

Watu tujue kuwa single au kuwa kwenye mahusiano ni hali tuu kama ilivyo kuwa na kitu flani au kukosa kitu kingine kwenye maisha

Mtu anaweza kuwa single hajawa tayari kuingia kwenye jukumu la ndoa, sio sababu amekosa mtu wa kuoana nae kama wengi wanavyodhani

Kuna wakati mtu anakua single lakini anatamani sana kuwa ndani ya mahusiano ila anashindwa sababu hajampata mwenye sifa anazotaka

Wakati mwingine mtu yuko single sababu hana uwezo wa kuwa na mahusiano labda ana mapungu aliyozaliwa nayonayo

Na pia mtu anaweza kuwa single sababu alishapitia mahusiano yakamvuruga na kumpa maumivu makubwa sana, kwa hiyo kwake kuwa peke yake ndio amani

Ndoa na familia ni jambo la heri kwa wanadamu lakini pia sio amri useme lazima kila mtu aoe/aolewe; na Kuwa ndani ya ndoa au kuwa na watoto sio ujanja na kukosa iwe ujinga! Hata kwenye vitabu vitakatifu kuna watu ambao hawakuwahi kuoa/kuolewa, kuna watu walioolewa/walioowa wasipate watoto, na wapo watu walioowa/kuolewa katika umri mkubwa pia.

Yote juu ya yote, mipango ya Mungu ni sahihi na mawazo yake ni mawazo sahihi kwetu.
Hawa watarajiwa hapa wanatukumbusha kumshukuru Mungu kwa maisha tuliyo nayo, kumwomba Mungu afanye kwa wakati wake

View attachment 1695876
Haya masuali yanaudhi sana, kule visiwa vya karafuu ndio yamekaa kitako, kwa siku unaweza kujibu hili swali mara mia moja aidha umeoa hujaoa na kwanini hujaoa utaoa lini kwanini huoi tu. Na sasa ukija kufanya hiyo nusra ya kuoa sasa maswali yanahamia kwenye mtoto, una watoto wangapi, ushapata mtoto, mkeo ni mjamzito ama vipi yaani saa zote ni ujinga kama huu.

Watu wanashindwa kufahamu hii ndoa ili mtu aoe kwa sisi waislamu inakuwaje, kuna masharti gani lakini hali gani ya kimaisha kwenda kumchukua mtoto wa watu kwao anakula na kuvaa vizuri kwa babake na mamake muda wote.

Kuna wakati ukichelewa sanaa kuoa wanaweza kusema ah huyu ni mkono wa shati au sampuli kama hizo
 
Sijui huwa wanauliza ili wapate nini
 
Hahaha dawa wakikuuliza kwanini hujazaa na wewe waulize kama wanataka uzae nao[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mimi sina shida na maswali ya namna hiyo, najibu tu bila shida japo itataegemea anayeuliza ana ujaribu gani na mimi.
 
Mimi wamenichosha mpaka inakera, kila siku ni unaolewa lini? Ina maana hujapata hata mchumba? Kama unaona hapaeleweki si uzae hata mwanao ulee,

Sasa kinachoshangaza hujawahi omba ushauri kwao jinsi ya kupeleka maisha yako, lakini ndiyo vinara wa kukupangia, ukirudi nyumbani huko mkoani ndiyo utajuta, jamani watupumzishe, maisha yana mipango yake hatupaswi kukurupuka tu..!
Kwaiyo bado hujaolewa?
unangoja nini sasa..[emoji3][emoji3]

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom