Maswali ya kuudhi - Umeoa? Umeolewa? Unao/olewa lini? Una watoto wangapi?

Maswali ya kuudhi - Umeoa? Umeolewa? Unao/olewa lini? Una watoto wangapi?

Utadhani ukizaa anakusaidia kulea fyuu zao
Jasmoni Tegga sio kila mtu anaweza kukuongelea personal life yako. Ingekua wazazi au watu wa karibu mbona powa tuu
Sasa unaniluza nimeolewa? Nina mtoto? Halafu vyote nakujibu hapana.... unaendelea zaa wewe, unazeeka!
Unataka nizae bila mipango?
 
Si ili ajilinganishe..., aanze kukushauri.

Ujue binadam wengi wanapenda kukuweka kama uko kwenye shida hivi ndo anakushauri cha kufanya.

Ili iweje Sasa !? Wakati kila mtu na maisha yake
 
Si ili ajilinganishe..., aanze kukushauri.

Ujue binadam wengi wanapenda kukuweka kama uko kwenye shida hivi ndo anakushauri cha kufanya.
[emoji16][emoji16] if ningekuwa nashida siningemueleza tu
 
Ona hawa nao
Screenshot_20210206-163101_WhatsApp.jpg
 
Haya maswali binafsi huwa nayachukia sana japo kweli nimeolewa na nina watoto. Ni maswali too personal kumuuliza mtu mzima mwenye akili zake maamuzi yake. Ila bahati mbaya ni maswali ambayo watu wengi huwa wanapenda kuuliza bila hata kuwaza hisia za wale wanaowauliza.
Tena heri haya maswali yatoke kwa mzazi au mtu wa karibu kuliko ilivyo kawaida kwa sasa.

Watu tujue kuwa single au kuwa kwenye mahusiano ni hali tuu kama ilivyo kuwa na kitu flani au kukosa kitu kingine kwenye maisha

Mtu anaweza kuwa single hajawa tayari kuingia kwenye jukumu la ndoa, sio sababu amekosa mtu wa kuoana nae kama wengi wanavyodhani

Kuna wakati mtu anakua single lakini anatamani sana kuwa ndani ya mahusiano ila anashindwa sababu hajampata mwenye sifa anazotaka

Wakati mwingine mtu yuko single sababu hana uwezo wa kuwa na mahusiano labda ana mapungu aliyozaliwa nayonayo

Na pia mtu anaweza kuwa single sababu alishapitia mahusiano yakamvuruga na kumpa maumivu makubwa sana, kwa hiyo kwake kuwa peke yake ndio amani

Ndoa na familia ni jambo la heri kwa wanadamu lakini pia sio amri useme lazima kila mtu aoe/aolewe; na Kuwa ndani ya ndoa au kuwa na watoto sio ujanja na kukosa iwe ujinga! Hata kwenye vitabu vitakatifu kuna watu ambao hawakuwahi kuoa/kuolewa, kuna watu walioolewa/walioowa wasipate watoto, na wapo watu walioowa/kuolewa katika umri mkubwa pia.

Yote juu ya yote, mipango ya Mungu ni sahihi na mawazo yake ni mawazo sahihi kwetu.
Hawa watarajiwa hapa wanatukumbusha kumshukuru Mungu kwa maisha tuliyo nayo, kumwomba Mungu afanye kwa wakati wake

View attachment 1695876

Busara zitakuua mama D
 
Watu wanapenda kuuliza sana,Mimi huwa nakereka ndani kwa ndani huwa sionyeshi kama nimeboreka na huwa siwez muuliza mtu.

Kuna swali lingine ambalo huwa linatukata stimu sana sisi ambao bado tunaishi kwetu,labda mzazi anakutambulisha,akmaliza huyo mtu anamuuliza kwahyo anaishi wapi wakat anakuona hupo hapo nyumbani
 
Umeongea vzuri dada Ayo maswali yanakera Sana au unakuta umeamua zako kupungua mtu anakuuliza mbona umekonda ivyo unaumwa? Yan Kuna watu hawajui kabisa kucommunicate
 
Labda wanaona hakuna kitu kingine unaweza kufanya zaidi ya kuolewa na kyzaa ndio sababu wanakimbilia kuuliza hayo- Watu wengine wameolewa na kuoa lakini hawafaidi kuoa kuolewa huko ndio maana wanafikiri kila mtu lazima aolewe na kuzaa..bila kuziona changamoto zinazomkabili huyo mtu ambae wanamuuliza hivyo.
 
Back
Top Bottom