Matajiri wakubwa Tanzania hawana msaada wowote kwa jamii zaidi ya kuinyonya

Huwa wanatoa Magari ya kuzikia
 
Umesema kweli...
Nlishuhudia watoto wa Bakharesa wakiendesha Gari za kifahari hapa Bongo.

Kuna haja ya kuwakumbusha waige Mfano watajiri Mengi
Yule mzalendo walimpiga vita kwelikweli kuanzia kobazi,wahindi,waarabu hadi watawala nakumbuka yule jamaa masilingi alivyomuandama!
 
Pambana kivyako,acha kutia huruma,Dunia inahitaji kukaza na sio kulia lia,

Wewe unajua wamepitia mangapi mpaka kufika hapo?

Wewe umeisadia nini jamii? Acha kua na mawazo ya kimasikini.
Dini inasemaje kwenye kusaidia maskini?
Jee wenye uwezo mkubwa hawana mchango katika jamii kwa wale ambao hawana uwezo?
Binaadam hatuwezi kuwa sawa kihali wala kimali hilo Allah ndio Kajaalia hivyo ili kutujaribu waja wake. Ndio maana Kuna kutoa Zakka na Mtume pia Akatusisitiza kwenye kutoa sadaqa
Mission sio mtu kufa bilionea, Mission jee ulitumia vp mali yako kwenye kuwapa wasiojiweza?
Rejea kwa waislam waliotangulia na wa zama za Mtume jee walitumia vp mali yao?
 
Hao wanaolaumiwa na mleta mada,wanaisaidia sana jamii,wanajitolea sana tu,
Pamoja na hayo,huwezi kumlazimisha mtu jinsi ya kutumia hela zake.
 
Kwanza, sio jukumu Lao kufanya maisha yako yawe poa, hii dunia hauidai chochote, it owes you nothing, and it is not fare,
Matajiri ndio watoa ajira, na kulipa Kodi kubwa, ili ikanunue madawati na kujenga mashimo ya vyoo kwenye kayumba ili mtoto wako asome!
 
Hao wanaolaumiwa na mleta mada,wanaisaidia sana jamii,wanajitolea sana tu,
Pamoja na hayo,huwezi kumlazimisha mtu jinsi ya kutumia hela zake.
Ni sahih
Lkn yeye katoa kama rai tu. Na ukiangalia ni kweli. Mungu Alipotutafautishia kwenye kupata ni kwa ajili ya hawa wenye nacho wawasaidie waso nacho ili wapate malipo mema.
Ila tukiangalia kidunia tu ndio tunafeli. Na ndio kama unavosema huwezi kumlazimisha mtu kutoa
 
Mleta mada atafute vyake aache kutia huruma hapa,
Dunia ya leo inahitaji kupambana,kumsaidia mtu sio amri wala jukumu la lazima,hata wahenga walisema mtegemea cha ndugu hufa masikini,walilenga kila mtu afanye kazi asiwe tegemezi.
 
Hapa ndo west Africa wanatupiga gap...pamoja na usalama wa nchi zao kuwa Tete ila matajir+wachezaji wanajitoa sanaa kwa familia duni
Ndiyo mkuu, unashangaa mtu maiti inakataliwa kwa kutomalizia gharama za matibabu lakini kwenye jamii Kuna mabilionea wanatumia pesa kuwapa simba na yanga is that fair?
 
Nchi nyingine zipi wanatoa sapoti???
 
Ukweli mchungu jamii zao siyo za watu weusi. Circles zao za wahindi na waarabu zinaona msaada wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…