Matajiri wakubwa Tanzania hawana msaada wowote kwa jamii zaidi ya kuinyonya

Wanalipa kodi na tozo mbalimbali, wametoa ajira.
Kusaidia jamii ni utaishi wao.
Hata hivyo kwa mfano mfanyabiashara Said Salim Bakhresa hupenda kutoa kimya kimya.
Hapendi matangazo anapotoa.
Ninachokumbuka yeye ndiye aliyejenga shule ya msingi Mburahati miaka 80.
Mfanyabiashara Azim Dewji ndiye aliyejenga madarasa 7 ya mwanzo shule ya msingi Kimanga mwaka 1994.
Kutoa ni hiyari lakini huwa wanatoa na wengi hawataki matangazo
 
Uvivu wa kimwili na kufikiri nao ni mzigo!
 
Vijana mnapopenda kutawaliwa na kulishwa bure kama ma gigolo.
Akulishe , akuajiri akupe mke wakati wewe unafanya nini?
 
Hampambani ndio maana unataka mgao
Wala mie sio katika wanaotaka mgao mkuu
Hapa mleta mada kazungumzia mchango kwa taifa kwa jumla, like elimu na afya. Tunaona matajiri wengi wanachangia kwenye issue za entertainment zaidi km mpira e.t.c
Na mie pia kwa kuongezea nawazungumzia wale mafukara waliokuwa hata hela ya kula kwa siku kwa ni shida wakati kuna matajiri wanakula na kusaza na kutupa kwenye dustbins
 
Hahahah!! Ngoja nicheke unaacha kuililia CCM. Unaenda kulilia jasho la MTU unajua kapambanaje kufika hapo?
All the best
 
kweli nimeamini masikini ana roho mbaya, chuki na wivu kwa tajari. kwani wewe nini kimeshinda kuwa tajiri ili uwasaidie hao masikini unao waonea huruma? usimlazimishe mtu aliyesota kutengeneza BRAND yake, aje atatue matatizo ya eti kwakua wewe huna kitu. kwani umekwatwa mikono na miguu? hata siku moja siwezi kumlaumu tajiri kwa kutokunisaidia. kila mtu AKAZE atoboe ki_MAI$HA.
 
Huwezi kuelewa kumbuka hapa tunazungumzia matajiri wakubwa ambao wanatumia miundombinu ya Umma kuanzia umeme, Barabara, maji n.k katika uzalishaji wa bidhaa zao na soko kuu la huduma zao ni Hawa Hawa wananchi masikini ambao watoto wao washindwa kuendelea na masomo kisa ada, mazao yao ya biashara hayapati soko zuri kisa Hawa jamaa wananunua mafuta ghafi ya kupikia kutoka Brazil na kuacha alizeti na mbegu zingine kama pamba na mawese sikikosa soko. Elewa mkuu
 
Huwez amin, nilikuwa nadhani una akili
 
Hivyo vitu wanatumia bure?
Hivyo viwanda vya kina Sunula na wenzake wanaonunua alizeti ni masikini ?

HAlafu wew kwenye kidogo unachopata unasaidia wangapi ? Au hata kazini kwako tu, je unafanya kazi kwa kiwango cha juu? Au doja na mvivu tu?
 
Wewe umechangia kwenye jamii?

Ajira wanazotoaa zinatosha
Mengine sio lazima hela ni zao wanazitafuta kwa kupambana na mengi, sio rahisi hadi amwage hela zake huko


Kutoa ni moyo
 
Hakuna aliyekatazwa kuwa tajiri na nadhani cha kuwauliza ni kama wanalipa kodi stahiki. Kama wanalipa then kinachobaki ni jukumu la hao wanaonunua V8 mpya Ila vyoo vya madarasa tunasubiri ufadhili wa marekani
Hili ndio la msingi benefits zinatakiwa kuuliziwa wanakolipa kodi kitu ambacho wa TZ hawawezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…