Wakuu,
Kumekuwa na maombi kadha wa kadha ya watu kutaka kuwa verified.
Tumeona vema tuweke urahisi wa mtu kuomba kuwa verified badala ya utaratibu wa awali. Kuwa verified kwako ni kwa hiari yako. Unaweza kusoma Sera yetu ya Faragha kama una concerns zozote >
Privacy policy ambayo ina ufafanuzi wa kina.
Kwa wanaotaka kuwa verified, utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:
Utabonyeza (ukiwa kwenye web browser) sehemu imeandikwa Account, kisha fuata utaratibu huu:
View attachment 1897917
Utabonyeza "Request Verification Badge". Utaweza kuona sehemu inakuja na eneo la kuweka ujumbe wa kuwasiliana nasi ukiambatanisha na copy ya ID inayothibitisha majina unayotaka yawe verified ni yako
View attachment 1897898
Ukishatuma request, vumilia kidogo kwani itakuwa processed na ikiwa ina changamoto progress itaonekana kwako baada ya sisi kuwasiliana nawe kuhusu ombi lako.
Profile yako au ya mdau mwingine, ukipeleka cursor itaonyesha maandishi haya (mfano):
View attachment 1898044
ILANI:
1) Kwa waliokuwa verified awali, huna ulazima wa kufanya mchakato huu, lakini ikikupendeza kujaribu - UNAKARIBISHWA
2) Unaweza kuwa verified ukiwa na ID yako ya JF (not a real name) endapo tutajiridhisha kuwa ID ni mtu tunayefahamiana naye na maudhui ya akaunti yake hayashushi hadhi ya badge husika; mfano wa waliokuwa verified kwa IDs kawaida ni
Bujibuji na
Madame B.
Wanachama ambao ni VERIFIED wataonekana hapa:
Verified Members
NB: Napokea requests nyingi za kubadili majina, tafadhali fanya hivyo mwenyewe kwa kutembelea
https://www.jamiiforums.com/account/username
Asante