Matapeli wa kimapenzi mtandaoni kutoka west Afrika

Kiukweli Dstv wana channels zinazo kufanya uketi kwenye kochi ushangae .... Binafsi huwa napenda sana ile Discovery3 HD inazungumzia kesi na matukio ya mauaji tu yaan wao ni kesi tu kwenda mbele
Hii ni namba ngapi? Mwana mimi natazama dana IDx ya 171
 
Hii ni namba ngapi? Mwana mimi natazama dana IDx ya 171
Eh sorry ndio.iyoniyo discovery ID sorry nilikosea ,

Iyo ID ndio naipendaa yaan iyo usiangalie na watoto kabisaa, mle kesi za mauaji tu unaweza usitaman kwenda US
 
Nilitamani sana nilete kisa hiki wiki iliyopita. Nimetumiwa hicho kitu wiki iliyopita. Kuna mdada mzungu anajidai yuko Australia,anaitwa SOPHIE EDWARD,anadai eti emenielewa. Akanielezea habari zake kwamba ana mtoto mmoja. Anasema yeye ni doctor huko na anasafiri nchi nyingi pia. Akatuma na picha zake nyingi akiwa hospital na zingine na wenzie wazungu (nafikiri hizo walidukua mahala). Alijieleza mengi. Nikamuuliza namba yangu umeitoa wapi?. Akasema Facebook Nikamwambia mimi situmii Facebook. Nikamuuliza unataka nini sasa kwangu?
Namba yake ni +229 55 26 56 10.

Kitu cha kwanza nikawaita vijana wangu dukani nikawaonyesha kinachoendelea kutoka kwa yule mzungu. Nikawaambia kitakachofuata ni utaperi huu. Nimewaonyesha ili mjue,siku mkadhani mmepata kumbe mnaandaliwa kupigwa.

Basi tukawasiriana na yule mdada siku kama 3,siku ya 4 asubuhi akaniambia amepewa zawadi na wenzie kanisani kutoka Haiti zawadi akanipigia picha Cheni za gold pc 2 zina ile msalaba. Computer moja,TV kubwa 1,Kamara na saa 3 za gold. Akaniambia,yeye ksbb yuko busy kuna waumini wenzie wanaenda Senegal wanaenda na hivyo vitu ili akanitumie kupitia Senegal. Akanitumia namba ya simu ya huyo sister atakaenitumia. Jina anaitwa Sister Stella Dennis. Akanitumia na picha ya huyo sister mzungu,ni wale masister kabisa wa kiroma. (Nikawaambia wadogo hapa ndio lengo lao linakaribia)

Siku ya 5 asubuhi niko mazoezi yule mwenye mizigo yangu sasa akanitumia picha kupitia what's up eti yuko DHL anatuma mizigo,yuko na masister wengine wawili wa kiroma.

Picha ilipokuja kuungua ni pale huyo sister ananiambia kutuma huo mzigo ni dollar 600,kwa hiyo yeye ana hela kidogo hapo,mimi nitume dollar 300 ili kukamilisha muamala wa utumaji. Nikamwambia nikipata nitawatumia. Akasema ni jambo la haraka ksbb wanatakiwa warudi Australia then wana safari ya Haiti. Nikamjibu hiyo hela sina. Nitawarudishia hela yenu vitu vikifika.

Akaja yule Sophie ananiambia yule sister ni wa heshima sana kwa hiyo ili tusimsumbue fanya leo kumtumia hiyo hela au kesho asubuhi. Nikamjibu wewe mimi sio wa kirahisi hivyo. Halafu najua kabisa nawasiriana na mwanaume. Hasa hasa from Nigeria au Ghana au Kenya.

Baadae akatoa picha ya mdada alievalia kidoctor aliyokuwa ameiweka kwenye what'sup yake. Baada ya masaa mawili ile namba ingine nayo ikatolewa ile picha ya sister wa kiroma.

No-+229 55 26 56 10
 
Nigerians😅😅😅
kila mmoja anataka hela kwa namna yake

huyu kasingizia babake kafariki
 
Dp kali sana aisee
 
Saa nne usiku, halafu kinafuata banged abroad yani vyote vizuri sana na utajifunza mengi
Banged abroad huwa kinanisisimua sana Mkuu zaidi nmefurahishwa na Wana jf kama wewe unanifanya nizidi kupaamini mahali hapa kwa kutupa mafunzo yenye vivids na zaidi nafarijika kumbe huwa tunaungana wana jf wengi mida ile kufwatilia madini kama yale

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Mimi mdau mkubwa sana ikifka saa nne niko kwenye TV labda niwe mbali na home
 
Kiukweli Dstv wana channels zinazo kufanya uketi kwenye kochi ushangae .... Binafsi huwa napenda sana ile Discovery3 HD inazungumzia kesi na matukio ya mauaji tu yaan wao ni kesi tu kwenda mbele
Hizi story unaweza ukakaa ndani siku nzima....aisee kuna binadamu katili sana kama ted bundy
 
Hii program imenifundisha uhuru ni kitu muhimu sana.....yaani wote walokuwa banged up abroad wanakwambia biggest lesson learned ni kuwa ur freedom is everything.
 
Hata mim nishawahi fanyiwa kama hii mzigo ukafika zanzibar 😂😂😂 naambiwa nitume laki 6 na mwanaume kapewa namba yangu nikamuambia kaka chukua eti hiyo mizigo itakusaidia 😂😂😂
 
Kwenye hili nakuunga mkono asilimia 100% kuna mtu namfahamu alipgwa milion zaidi ya milion 20 kwa kitu hiki hiki ulichosema.

Pesa, uaminifu wa muda mrefu n.k.

Na yeye pia alichukua mkopo .

Ningeandika hapa ila hizi verified id shida kidogo
 
Watu kama hawa pitia madalali.

Ukiingia kwa hii style wanakulipua.
 
Kuna mke wa mtu nitampiga muda sio mrefu ,nishamwambia mm ni unemployed na Sina Hela ila amekomaa tu kuniganda kosa nna maneno matamu na ya kumfariji ukizingatia ana mgogoro wa ndoa na mmewe,nikipiga lako 5 natembea
 
Duuh mchizi alinogewa, miaka miwili yote aisee
 
Daaa hata YOUTUBE zipo video zikioneshq chain nzima aisee nimependa sana hiki kipindi
 
Kuna mke wa mtu nitampiga muda sio mrefu ,nishamwambia mm ni unemployed na Sina Hela ila amekomaa tu kuniganda kosa nna maneno matamu na ya kumfariji ukizingatia ana mgogoro wa ndoa na mmewe,nikipiga lako 5 natembea
Cha muhimu kuwa makini usije ukalambwa wewe maana cha wizi usije shikwa utajuta
 
Hata mim nishawahi fanyiwa kama hii mzigo ukafika zanzibar [emoji23][emoji23][emoji23] naambiwa nitume laki 6 na mwanaume kapewa namba yangu nikamuambia kaka chukua eti hiyo mizigo itakusaidia [emoji23][emoji23][emoji23]
Ahahaaaaa....! WaNigeria hao. Ila huyu Get Rich anajua mengi huyu
 
Kuna scammer mmoja wa Urusi alifanya harusi ya $500,000 kwenye golf court.

Scammers wa Bongo kuna la kujifunza hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…