Matendo yangu ndiyo chanzo kikuu cha kukosa furaha na amani ya moyo, najuta

Matendo yangu ndiyo chanzo kikuu cha kukosa furaha na amani ya moyo, najuta

Sehemu ya nne
Ilipoishia.
Miezi michache mbele nikapewa taarifa za ujauzito Tena tofauti ya taarifa ya mimba hii ni kuwa ilikuwa ni kweli.

Baada ya huu ujauzito ndio hapo Kwa hiari yangu nikakubaliana na hali kuwa yaliyotokea ni kutokana na matendo yangu nahitaji kuwa full responsible kulea mwanamke mwenye mtoto na ujauzito.

Taarifa ziliwafikia ndugu zangu pamoja na wazazi wangu wote Kwa nyakati tofauti walinitafuta kwenye simu na kuonyesha kushangazwa na maamuzi yangu na kunitaka niachane na huyu mwanamke haraka iwezekanavyo nakumbuka baba yangu alinipigia simu na kuniambia we mpumbavu hujui kutongoza mpaka unakuwa na mahusiano na Mwanamke mwenye mtoto tena hana kazi Kwa wakati ule niliona ni matusi kwangu kumbe ulikuwa uchungu wa mzazi anayeona mwanaye akifanya maamuzi yasiyo na busara.

Sijui ni upendo au ujinga sikusikia la mtu yoyote na Kwa kuwalizisha niliwajibu kuwa sipo naye ameenda kwao kitu ambacho kilikuwa ni uongo kwani niliendelea kuishi naye huku mimba ikiwa kubwa.
 
Shisha nondo ndefu kidgo basi...
 
Hizi nyumba za kupanga zinachangamoto sana kuna jamaa yangu kawanyandua wapangaji wote wa kike alipopanga yani kosa uwe2 na ajira nzuri
 
Hamna wa kulaumu na ndio njia ya kujifunza hiyo hivyo nasema kula matokeo ya matendo yako mwenyewe.
A man without a purpose is already dead.
 
wanaume kuna haja ya kujua mfumo mzima wa uzazi wa mwabamke wako kuepuka ujinga unaoweza kuzuilika tena mfundishwe kwa fimbo mpaka muelewe
Adam ndio alituanzishia hili balaa, tusilaumiane sana K tamu.
 
Sehemu ya nne
Ilipoishia.
Miezi michache mbele nikapewa taarifa za ujauzito Tena tofauti ya taarifa ya mimba hii ni kuwa ilikuwa ni kweli.

Baada ya huu ujauzito ndio hapo Kwa hiari yangu nikakubaliana na hali kuwa yaliyotokea ni kutokana na matendo yangu nahitaji kuwa full responsible kulea mwanamke mwenye mtoto na ujauzito.

Taarifa ziliwafikia ndugu zangu pamoja na wazazi wangu wote Kwa nyakati tofauti walinitafuta kwenye simu na kuonyesha kushangazwa na maamuzi yangu na kunitaka niachane na huyu mwanamke haraka iwezekanavyo nakumbuka baba yangu alinipigia simu na kuniambia we mpumbavu hujui kutongoza mpaka unakuwa na mahusiano na Mwanamke mwenye mtoto tena hana kazi Kwa wakati ule niliona ni matusi kwangu kumbe ulikuwa uchungu wa mzazi anayeona mwanaye akifanya maamuzi yasiyo na busara.

Sijui ni upendo au ujinga sikusikia la mtu yoyote na Kwa kuwalizisha niliwajibu kuwa sipo naye ameenda kwao kitu ambacho kilikuwa ni uongo kwani niliendelea kuishi naye huku mimba ikiwa kubwa.
[emoji848][emoji848]
 
Unaandika dono dono kama mbuzi anavyo tembea akijisaidia hata haivutii kuisoma kwa sababu hujuwi kupangilia
 
Sehemu ya Tano.
Tuliendelea na maisha yetu ya kuishi pamoja bila ya baraka za wazazi kutoka upande wangu Wala upande wake mimba iliendelea kukua mpaka ilipofikisha miezi Saba Kwa bahati mbaya mimba iliharibika nakumbuka ilikuwa mwezi wa kumi tarehe 7 mwenza wangu alinipa taarifa kuwa mtoto hachezi tumboni Kwa siku mbili kutokana na kutokuwa na uzoefu na masuala ya ujauzito nilichukulia poa kumbe ilikuwa ni sign mbaya haswa Kwa kiumbe kilichopo tumboni na Kwa Afya ya mama tukakubaliana na mwenza wangu siku inayofuata aelekee hospital kucheki tatizo ni Nini.

Siku iliyofuata Mimi nilielekea kazini na mwenza wangu akaelekea hospital mchana ulipowadia nikiwa kazini mwenza wangu alinipigia simu huku akilia na ndipo aliponieleza kuwa hospital wamempa taarifa kuwa kiumbe kimefia tumboni na wamempa rufaa kwenda hospital ya Mkoa Kwa ajili ya kukitoa kiumbe tumboni ilikuwa ni siku mbaya kwani sikuwa nimejiandaa Kwa chochote hususani kwenye pesa Kwani hospital ya Mkoa ilikuwa wilaya nyingine ambayo sina mtu ninayefahamiane naye na pia gharama za matibabu na mtu wa kumwangalia mgonjwa na mtu atakayebaki kumwangalia mtoto nyumbani. Haraka sana nikaomba ruhusa kazini kuelekea nyumbani Ili kusolve changamoto zangu na kitu Cha kwanza kufanya nilipofika nyumbani ilikuwa kukagua suruali zangu zote Ili Japo nipate nauli ya kunifikisha mjini kwani Mwenza wangu alikwisha tangulia hospital. Siku ya kufa Nyani miti yote uteleza pesa niliyoambulia ilikuwa ni Tanzania shilling 200 ikabidi nianze kuumiza kichwa napataje pesa na hapohapo Sina historia nzuri Kwa wakopeshaji wa ule mji.

Nilikuwa Nina laptop aina ya hp nikaiweka kwenye begi na nikaanza safari Kuelekea Kwa wakopeshaji Kwa bahati nikamkuta mkopeshaji nikamuelezea yaliyonikuta na kumuomba anikopeshe Shilling laki Moja na nusu Kwa dhamana ya laptop mwanzo alikataa ikabidi nibembeleze mpaka akukubali kunipa Kwa riba ya asilimia 30 ndani ya mwezi mmoja.

Ilikuwa saa 8 mchana chapu Kwa haraka nikapanda gari kuelekea hospital ya Mkoa ni mwendo wa masaa mawili saa kumi nikawa nimefika nikanunua chakula nakuaanza kuelekea hospital nilipofika walinzi wakanizingua kuingia kisa sio muda wa kuona wagonjwa ikabidi nijiongeze kiutu uzima akaniruhusu NIlitembea Moja Kwa Moja mpaka wodini nikamuona mwenza wangu huku tumbo likiwa Bado kubwa nikamuuliza vipi akaniambia manesi wamemwambia hawawezi kuitoa Kwa vile mimba ni kubwa na njia pekee nikusubiri uchungu ili ije itoke yenyewe ikabidi niende Kwa manesi Ili wanipe utaratibu inakuwaje wakanielezea kilekile walichomueleza mwenza wangu Kwa vile Mimi sio mtaalamu wa uzazi ikabidi tufatishe kile walichosema. Ishu nyingine ikawa ni nani atabaki na mwenza wangu kumhudumia hospital lakini mwenza wangu akaniambia kuwa alishampigia rafiki yake yupo njiani anakuja kikubwa nimuachie pesa ya matumizi nikaingia mfukoni nikamuachia elfu hamsini na tukakubaliana kuwa Mimi nirudi nyumbani kumwangalia mtoto kwani alikuwa kamuacha Kwa jirani na atakuwa ananijulisha kinachoendelea.

Nikarudi nyumbani nikamchukua mtoto Kwa jirani ikanibidi niwe namhudumia mtoto kumuogesha kumpa chakula huku ikifika asubuhi namuacha Kwa jirani na kwenda hospital kuangalia maendeleo ya mgonjwa hatimaye zilipita siku tatu na siku ya nne kabla sijaamka mwenza wangu akanipa taarifa kuwa wamefanikisha kuitoa mimba asubuhi nikadamka mapema kuelekea hospital kumchukua Ile nafika nakabidhiwa kiumbe kimefunikwa kwenye shuka na kuambiwa kuwa alikuwa mtoto wa kiume ikanibidi nimuulize nesi kuwa siwezi pata sehemu ya kukizika kiumbe palepale hospital akaniambia hawana utaratibu huo inabidi tuende nacho hapo Sasa kichwa kikaanza kuwaka nakipeleka wapi nilipo nimepanga na utaratibu wa ule mji hakuna makaburi ya pamoja kila mtu anzika kwake Sasa Mimi Sina Uwanja nakizikia wapi hichi kiumbe na nani nitamuomba hakubali nizike kwenye eneo lake nikachukua kiumbe nikakiweka kwenye begi nikavaa mgongoni nikamwambia mama mtu pamoja na rafiki yake watangulia nyumbani mimi nafanya harakati za kupata eneo la kuzikia...
 
Kwenye Begi!
20220623_044046.jpg
 
Back
Top Bottom