Sehemu ya nne
Ilipoishia.
Miezi michache mbele nikapewa taarifa za ujauzito Tena tofauti ya taarifa ya mimba hii ni kuwa ilikuwa ni kweli.
Baada ya huu ujauzito ndio hapo Kwa hiari yangu nikakubaliana na hali kuwa yaliyotokea ni kutokana na matendo yangu nahitaji kuwa full responsible kulea mwanamke mwenye mtoto na ujauzito.
Taarifa ziliwafikia ndugu zangu pamoja na wazazi wangu wote Kwa nyakati tofauti walinitafuta kwenye simu na kuonyesha kushangazwa na maamuzi yangu na kunitaka niachane na huyu mwanamke haraka iwezekanavyo nakumbuka baba yangu alinipigia simu na kuniambia we mpumbavu hujui kutongoza mpaka unakuwa na mahusiano na Mwanamke mwenye mtoto tena hana kazi Kwa wakati ule niliona ni matusi kwangu kumbe ulikuwa uchungu wa mzazi anayeona mwanaye akifanya maamuzi yasiyo na busara.
Sijui ni upendo au ujinga sikusikia la mtu yoyote na Kwa kuwalizisha niliwajibu kuwa sipo naye ameenda kwao kitu ambacho kilikuwa ni uongo kwani niliendelea kuishi naye huku mimba ikiwa kubwa.