Matokeo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 24, 2019: CCM yashinda kwa 99.9%, CHADEMA wapata Kijiji kimoja na Vitongoji 19, CUF nao Kijiji

Matokeo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 24, 2019: CCM yashinda kwa 99.9%, CHADEMA wapata Kijiji kimoja na Vitongoji 19, CUF nao Kijiji

Kazi ya TV yetu pendwa ilitakiwa kutujuza ya vituoni leo
 
Huyu mchungaji Erasto ni wa wapi? Hivi kila kitu mnachosikia huko ni lazima mlete humu kama habari?
 
Huyo ni mwanasiasa na SI mchumgaji na Kama ndivyo kondoo wake wajiyafakari
 
Leo Jumapili, tarehe 24.11.2019 kidunia ni siku ya Ibada kwa makanisa mengi ya Kikristo.

Waumini na viongozi wao wanajisogeza karibu na Muumba wao kusafishwa dhambi zao na kuzaliwa upya.

Lakini kwa hapa Tanzania Leo pia ni siku ya kukamilisha lile zoezi la maigizo ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Ni siku ambayo haramu inahalalishwa ili mbele ya uso wa wastaarabu ionekane kuna uchaguzi unaohusisha vyama vingi (ushindani).

Kwa leo nimewakubali watanzania, meseji mliyowatumia ma director wa filamu hii inatosha kuwapa fundisho kwamba nyie siyo wa kuburuzwa.

Wamebaki wasiojitambua walioamua kuweka akili zao miguuni ili kushiriki kuhalalisha udhalimu.

Vituo vingi tangu vimefungulia vimehudhuriwa na wafuasi wa wanyang'anyi.

Kama wangeruhusiwa kuvaa sare zao za rangi ya majani ya maboga tungeshuhudia minenguo ya Konde Boy mwanzo mwisho.

Hongereni Watanzania, ujumbe mliotuma umefika, hata wakijifariji lakini roho zinawauma kwa mwitikio duni wa zoezi la maigizo lililofanyika leo
 
Dunia imeshafika mbali sana kwenye demokrasia, na faida za vyama vingi hazina mjadala zimeshafamika na kujulikana na hata wakina Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere.

Nilijiandikisha kupiga kura kumchagua kiongozi wangu wa mtaa lakini sikupiga kura eti mgombea kapita bila kupingwa.

Hivi ni kweli mtaa mzima hakuna mwananchi asiyemtaka kiongozi ambaye hakupingwa? Ni heri basi CCM ingeleta wagombea 2 ili wanamtaa wenyewe wachague mmoja wanaempenda.

Hatuko kwenye kisiwa hii chorus ya wanaopenda demokrasia nchi iko siku mwangwi wake utafika na kusikia mbali.

Vitendo kama hivi ndivyo vilivyoisumbua TANU na ASP wakati wa ukoloni.
 
Hii wana historia tunaita active resistance ila wkt wa kujiandikisha ilikuwa passive resistance....
General election sijui itakuwaje mwakani hizi si dalili njema....
 
Hahahaahhaha
IMG-20191124-WA0024.jpeg
IMG-20191124-WA0023.jpeg
 
Tuko kwenye roller coaster la maigizo na vituko. Eti wananchi walikuwa wanahimizwa kwenda kujiandikisha ili washiriki kwenye huu upuuzi. Yaani watu wachache wakijitoa akili na sisi wote tunapaswa kuwaunga mkono kwenye upumbavu wao.
 
Yaani ni kitu cha kusikitisha sana leo niko kanisani Padre ninayemheshimu sana eti anahamasisha waumini wakapige kura eti kutopiga kura ni dhambi najiuliza wakati watendaji wanakimbia ofisi na kukata majina ya upinzani walikuwa wapi wasikemee hayo? Watuache sisi tumekataa hatuendi kupiga kura wao wawaweke hao wateule wao wa ccm.
 
Back
Top Bottom