Leo Jumapili, tarehe 24.11.2019 kidunia ni siku ya Ibada kwa makanisa mengi ya Kikristo.
Waumini na viongozi wao wanajisogeza karibu na Muumba wao kusafishwa dhambi zao na kuzaliwa upya.
Lakini kwa hapa Tanzania Leo pia ni siku ya kukamilisha lile zoezi la maigizo ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Ni siku ambayo haramu inahalalishwa ili mbele ya uso wa wastaarabu ionekane kuna uchaguzi unaohusisha vyama vingi (ushindani).
Kwa leo nimewakubali watanzania, meseji mliyowatumia ma director wa filamu hii inatosha kuwapa fundisho kwamba nyie siyo wa kuburuzwa.
Wamebaki wasiojitambua walioamua kuweka akili zao miguuni ili kushiriki kuhalalisha udhalimu.
Vituo vingi tangu vimefungulia vimehudhuriwa na wafuasi wa wanyang'anyi.
Kama wangeruhusiwa kuvaa sare zao za rangi ya majani ya maboga tungeshuhudia minenguo ya Konde Boy mwanzo mwisho.
Hongereni Watanzania, ujumbe mliotuma umefika, hata wakijifariji lakini roho zinawauma kwa mwitikio duni wa zoezi la maigizo lililofanyika leo