Sababu za kweli za uchaguzi huu kuvurugika Kwa kuvurugwa ni ukosefu wa fedha za kugharamia kampeni, wasimamiaji, wahesabu kura, na logistics mbalimbali. Yaani ilikuwa tuache kujenga reli ili twende tukachaguane au tuache kuchaguana tukajenge reli. Kwasasa nchi haina fedha za kufanya yote Kwa wakati mmoja ila ni ngumu kuisema hii hadharani.
Nadhani sababu hii ingekuwa ya msingi kama ingepata mtu sahihi wa kuisemea. Nchi zetu hazipigi hatua kutokana na kujikita kwenye mambo yasiyo ya msingi kama vile uchaguzi wa kila mara, sikukuu, haki za binadamu nk. Wakati wazungu walipokuwa wanajenga uchumi wao hawakuwa na demokrasia wala haki za binadamu, China walifika pale Kwa kuachana na demokrasia, Rwanda imefika pale Kwa kuachana na democracy, waarabu wamefika pale Kwa kuachana na demokrasia.
Democracy, haki za binadamu, soko la dunia, benk ya dunia na IMF ndizo sababu halisi za pekee zinazosababisha Africa iwe nyuma