Matokeo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 24, 2019: CCM yashinda kwa 99.9%, CHADEMA wapata Kijiji kimoja na Vitongoji 19, CUF nao Kijiji

Matokeo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 24, 2019: CCM yashinda kwa 99.9%, CHADEMA wapata Kijiji kimoja na Vitongoji 19, CUF nao Kijiji

Hawa ni sikio la kufa ..... kama kujifunza ingeshajifunza kitambo, hata mishipa ya aibu imesha katika, sura zao kavu mijitu na watoto zao na wake zao tena inahata wajukuu eti inahimiza watu wakapige kura!
 
Mambo yapi mazuri aliyoyafanya? Kushindwa kuajiri miaka minne, kushindwa kuwapa mikopo wanafunzi wa elimu, kushindwa kupandisha madaraja miaka minne, kuharibu uchumi na kusababisha biashara zifungwe nchi nzima,kuharibu uchumi na mzunguko wa fedha, kuwabambikia umaskini watanzania ambao hawakuwa nao, kuwabambikia watu kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, kukiuka haki za binadamu nchini, kuvunja katiba na sheria, kuharibu mahusiano ya kimataifa na wawekezaji haya ndio mambo mazuri aliyofanya?
Ulicho andikakinaitwa ukasuku, kwakua hakuna ata hoja moja yenye ukweli ata wewe unajua ilo.Watu wameajiriwa, mikopo imeongezeka,madaraja yamepandishwa, baadhi ya biashara kweli zimefungwa na zipo biashara zilizo funguliwa.
fedha ilikua lazima idhibitiwe kwakua imeonekana serikali ilikua ikikopa fedha kwenye mabenki tena kwa riba kubwa wakati ki uhalisia izo fedha zilikua za Serikali yenyewe.

Kama wao mafisadi walivyo tuhujumu kama nchi, na wao wanatakiwa Wanywee kikombe kilekile tulicho Nywea sisi wakati wanatuhujumu. JPM Baba Lao: kama uli tafuna pesa ya Serikali basi tambua itakutokea Tundu lolote katika mwili wako.
 
Huyo kwa ongea yake, sauti, na tabia ni CCM, ........ Kwa kifupi ni kuwa CCM walipanga iwe hivyo ili kutafuta ka uhalali. Wapo wengine kadha wakadha wapo mtawasikia kutoka vyama mbalimbali villivyo jitoa, watatangazwa washindi.
sasa tatizo lako nini.hatutaki mavyama ya kidikteta hapa..chama kinawaamulia wananchi mtu wa kuwaongoza..ni ujuha wa kiwango cha Kubenea jomba...wa elimu ya hapa na pale.hahahaha
 
Kweli watu wa Babati wanajielewa. Nimewasikia Channel ten taarifa ya habari wakisema kwenye katiba ya CHADEMA hakuna kifungu hata kimoja kinachosema chama kitagomea uchaguzi.

Ndio maana wao wameenda kupiga kura.
Kwani lazima wawe Chadema, waanzishe chama chao au waungemkono juhudi za mheshimiwa kama walivyofanya wengine. Mwenyekiti wa chama alishatamka hakuna mjadala!
 
Taifa linahitaji toba
Screenshot_20191125-005255.jpeg
 
Kwakipindi cha sasa hakuna chama cha upinzani chenye nguvu kinachoweza kuishinda CCM , Ata wakifanya kampeni mwaka mzima.
Shida iliyopo hakuna tena watu wanaoweza kujenga hoja kama alivyokua Dr Slahaa. Yaani sasaivi wapinzani hojazao ni kupinga yale anayofanya JPM au wanasubiri kiongozi wa serikali ahutubie wao watafute makosa kwenye hotuba ili uwe hoja.
Vyama vipo na hoja zipo shida demokrasia ndiyo imeminywa
 
Kweli umeongea taka taka
Kwakipindi cha sasa hakuna chama cha upinzani chenye nguvu kinachoweza kuishinda CCM , Ata wakifanya kampeni mwaka mzima.
Shida iliyopo hakuna tena watu wanaoweza kujenga hoja kama alivyokua Dr Slahaa. Yaani sasaivi wapinzani hojazao ni kupinga yale anayofanya JPM au wanasubiri kiongozi wa serikali ahutubie wao watafute makosa kwenye hotuba ili uwe hoja.
 
King Kisali,
Hebu acheni tathmini za kiajabuajabu
Watu watajitokeza wapi wakati 90% ya mitaa na vijiji wagombea wa CCM wamepita bila kupingwa na chaguzi hazikufanya??

Pili ni trend iliyopo miaka yote kwamba chaguzi hizi hazina hamasa mfano hai ni mimi mwenyewe nina miaka 46 hivyo nilpaswa kuanza kushiriki chaguzi hizi miaka 28 iliyopita... Lakini ukweli ni kwamba sijawahi hata mara moja kupiga kura hata mwaka mmoja tangu 1991 nilpofuhusiwa kisheria
Wala sikumbuki kuona harakati zozote kwenye chaguzi hizi. Lakini uchaguzi mkuu 2015 nilitumia laki unusu kusafiri kwenda kupiga kura nilkojiandikisha
 
Leo nimeamini kuwa hakuna CCM bila CDM! aibu ya mwaka hii.
Hatimae ccm wapigiwa kura na polisi.
 
Nilienda kituoni kufanya utafiti. Kweli inasikitisha. Turn out ndogo mno kuanzia asubuhi mpaka wanafunga. Hakuna foleni mpiga kura anajitokeza mmojammoja tena kwa kupishana madakika kibao. Muda ya mwishomwisho ni kama hakukua na wapiga kura kabisa mpaka msimamizi anauchapa usingizi.
Sio lazima pawepo na foleni ndipo idhibitike kuwa watu walipiga kura, twambie mpaka saa 10 uliona watu wangapi wamepiga kura? huo ndo utafti. Nchi zilizoendelea ni vituo vichache sana unaweza kuona foleni, lkn kwa takwimu za nchi nzima waliojitokeza ni zaidi ya % 70 labda na sisi tumeendekea.
 
artch2311,
Hiyo ni wewe tuu hata uchaguzi mkuu wapo watu mpaka wanaenda kaburini wakiwa na miaka 80 lkn hawajawahi kupiga kura na hawajawahi kuhudhuria mkutano wowote wa siasa.
 
Back
Top Bottom